Baba yangu mzazi, mzee isaki alikuwa mlinzi kanisani. Ule ulinzi kwamba siyo mgambo wala askari ni raia tu, miaka ya nyuma uaminifu wako ulikubeba.
kazi hiyo aliifanya zaidi ya miaka arobaini. Akamwambia mchungaji wa lile kanisa, nguvu zimeisha nataka nipumzike, mchungaji hakuona kama serious issue, ikabidi mzee aendelee na kazi huku anangojea aletewe mtu wa kumwachia kazi.
Mwaka 2001, pasaka jtatu kuamkia jnne, waliingia wezi,
Wakamuulia baba yangu, ndani ya kanisa, pale madhabahuni damu yake ilijaa pale hadi tunaenda kwenye ibada ya mazishi iko pale, ilikuwa huzuni kubwa. mzee alikuwa mpole sana.
Walikamatwa vijana ila mama akasema sitaki kesi, mzee wangu wameshamuuwa, waachieni Mungu anajua.
Walikufa vijana wengi pale kwetu wakiweweseka tulimuuwa yule mzee kanisani. Wengine hadi wazazi wao na ndugu zao walikufa.
Wezi hawafai.
So sad.
R.I.P. Paradise Baba na Mama!
Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani huyo Rasta marehemu atakuwa Lule, walikuwa wajaluo wale, walikuwa na nyumba opposite na barabara ya kwenda Nyasaka karibu na kwa Masubo.Dahhh....
Nimemkumbuka marehemu Rasta flani pale alikuwa anavuta bange na kuiuza aiseeeee....
Nakumbuka mdogo wake Rasta pia aliitwa Paul alifariki mkuu...
Dahh, yule mama mwenye iliyokuwa Baxtan alijikuta anapoteza wanawe wote wakiume
Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi kamili mkuu, walikuwa na mdogo wao aliitwa Dora na dadaake nimemsahau binti flani mfupi sana....Nadhani huyo Rasta marehemu atakuwa Lule, walikuwa wajaluo wale, walikuwa na nyumba opposite na barabara ya kwenda Nyasaka karibu na kwa Masubo.
Kuna watu wabishi mpaka kero yani.Utadhani alikuwepo !! Wakati mkono nimemuonyesha...kuna watu wabishi humu
sent from toyota Allex
Matajili wameloga hawaibikiPesa inanukia cjui huwa wananusa hawa jamaa...
Mbona hatuskii wakienda kuvamia kwa matajiri wakubwa au viongozi..au kule hazinukii
Nawe upo nyuma
Man nliishi hapo nyuma ya comfort hotel, sipasahau ingawa daily npo hapa comfort nakunywa bia
Wana hapa comfort nawasoma sana wakiingia jf, tutafutane
Ndo sebuleni kwangu pale confortWana hapa comfort nawasoma sana wakiingia jf, tutafutane
Hahaha Mzee wako alikua ni noma...Hivi kwa nini wanaliita jiwe la Fatuma?ilikuwa ni majira ya usiku mnene miaka ya 99 nikiwa mdogo katika mji wa tarime
mvua ikiwa ya rasharasha ikipiga mara vishindo vikali vya kuvunjwa ukuta vinasikika kila mtu anatahamaki ni kitu gani hicho
kuchakata akili kumbe ni majambazi yanatumia jiwe la fatuma kuvunja geti pamoja na ukuta
kulikuwa na frem ya duka pembeni ya ukuta mangi akaanza kupiga yowe wale jamaa wakamwambia atulie kama uji otherwise wakiingia wanaanza na yeye
usiku nikamuona mzee wangu kaamka kabeba upinde na mkuki
akawaamsha wanaume wawili wakaenda hadi getini kusubiri majambazi wavunje waingie wale nao sahani moja asee wale majambazi hawakutarajia ambush ile ile fatuma imedondosha geti tu wanakutana na mvua za mishale na mikuki hahaha
hawakutarajia iyo ambush
mzee wangu alikuwa shujaa sana r.i.p
Me imenibidi nitoke njee nikague kama mageti yamefungwa vizuri yani ni balaa. Tuombe ulinzi wa Mungu tuu.Hii ni thread yangu ya kwanza kusoma comments zote. Inatisha sana hasa kusoma hizi post mida hii ya usiku wa majambazi. Poleni sana wote mliokutwa na haya matukio yaliyopelekea hadi kupoteza maisha kwa baadhi ya wapendwa wetu.
Mwenyezi Mungu atulinde usiku huu na siku zote
Amina.
Tatizo tunajenga kimaskini Sana, ukisikia mwenzangu na mie anajenga, mara nyingi itakuwa nje ya mji, hapo ndo Shida inaanza,Hivi mbona almost wote mliivamiwa mmejenga tu kuhamia unakutana na majambazi?
Kujenga kunaanza kuogopesha sasa
Sent using Jamii Forums mobile app
Hauna tofauti na wale wanaobisha kuwa hakuna uchawi. Siku yakupate ndipo utajua ukweli ni upi. Hao majambazi wenyewe skills za kutumia silaha wanatofautiana. Njoo kwetu nikuoneshe mmoja aliyevamiwa baani kwake (tena hata hapana hadhi ya kuitwa baa) jamaa walikosa huko walipokuwa nwanaenda. Walikuja hapa na kuanza kurusha rissi hewani mfululizo (zilipigwa zaidi ya risasi 10). Acha kubisha ndgu. Pia majambazi hupiga risasi sio chini ya mbili kwenye tukio (moja hupigwa iwapo kuna yowe zinapigwa, hivyo wanawatisha raia) moja ni kuzuia watu kusogea eneo la tukio na nyingine wanapiga wakati wanaondoka ili kuwatisha watu wasiwanyatie.Acha utani hamna kituo cha polisi kinafungwa.
Mecco sasa hivi wapo vibaka tu uhalifu wa namma hiyo haupo tena.
.
Huwezi kupiga risasi kiholela holela au kuvamia Mecco, Igoma, National kwa kifupi katikati ya mji ukatoka salama ninaandika nikiwa nauhakika wa 100% sehemu zote zilizokuwa na matukio ya kuvamiwa na majambazi zimedhibitiwa ukija hutoki Mecco, Kishiri, Katoro, Tarime, Kahama, Lunzewe na Geita
Kudadekimwaka 2013 niko zangu chuo,nilikuwa nasoma night maana kuna kikazi nlikuwa nakifanya mchana,
Nmetoka zangu chuo saa 3 usiku niko hoi,ni mmoja ya wale vijana ambao si maskini sana lakini mpenzi sana wa kubadilisha mavazi na kujipenda nisiyependa kujichanganya.
Basi nmerudi zangu nmechoka hatari na siku hyo dada yangu mtoto wa baba yangu mkubwa alikuwa ndo ameetoka kupewa mkopo wake wa almost 30m sema alichukua kama 2m nyingne akaiacha kwenye a/c yake.Basi mi sku hyo mapema tu kwenye saa 5 nkalala zangu,sasa majira ya kama saa 8 nkasikia mlio mkubwa mno akili yangu ikanambia hapa itakuwa ni transformer ya mtaani imebutuka ghafla kidogo tena naskia buuu na kishndo cha mlango kuanguka hapo sasa ndo nkashtuka na kujua sasa tumeingiliwa.Waliingia ndani kama 10 wengine wanaweza kufika hata 20 walikuwa nje na silaha na wengine na mapanga,walivyoingia kituo cha kwanza ni chumba cha wanawake,wakavunja mlango ote wakawalaza chini,then ndo wakaja na kwetu sasa ote tukawekwa barazani,dah nakumbuka walisafisha nyumba maana walibeba mpka raba zangu,lakini cha ajabu hawakutupiga hata kofi,na walivyoingia walikuwa wanajua taa zinawashwa wapi na kila chumba anakaa nani,basi majirani wakataka kutoka wakaambia atakayetoka tu anakula shaba ya kichwa,basi mwisho wa siku wakaiba mikufu ya dhahabu,pesa then wakaondoka dah hakuna siku niliyojiona mjinga kama siku hyo,mwenye nyumba alikasirika mno maana mpka alikuwa analia basi,majirani ndo wakatoka wakawa wanatupa pole pale,kuna baadhi ya vitu walishindwa kubeba hvyo waliviharibu tu kama Tv kubwa ya chogo na hata vioo vya gari walivunja kama kukomoa tu na tv walilibamiza chini.Ilivyofika asubuhi saa 12 tukaenda polisi kitunda tukakuta kituo bado hakijafunguliwa wakati tunasubiria tunaona wanakuja watu wngine wamekatwa na mapanga wanavuja damu,kumbe kila walivyoondoka kwetu kila waliyekutana nae njiani alikuwa anaporwa vitu vyake na kuchezea mapanga,pale polisi tulikaa mpka saa 1 ndo wakaja polisi cha ajabu hawakutupa hata uzito wa kusema waje eneo la tukio kukagua na mengineyo mengi yalitokea nisingependa kuyaandika basi mzee kwa hasira akaamua kuipotezea kesi but siku ile ile tukawapigia ndugu simu na kuwaelezea kilichotokea walikasirika mno,akapigiwa simu marehemu babu yetu mzaa mama akaja alivyoambiwa alikasirika mno.Kikafanyika kikao kidogo nakumbuka kulikuwa na ndugu walokuja kutuona tu sku hiyo si chini ya 30,na kilikuwa kipindi mvua inanyesha.Basi mzee akawaambia wale ndugu mpka saa 8 mchana kila mwenye mtoto kati ya wale waliokuwa pale na yupo dar basi anahitajika amlete pale kabla ya hiyo saa 8,na kweli kwenye saa 8 ote walikusanywa then ikaanza kusomwa dua ndani ya nusu saa kwanza mvua ikakata then tukatoka nje ote dua ikaendele dua inasomwa watoto wanaitikia,dua inasomwa watoto wanaitikia lakini kadri dua ilivyokuwa inasomwa ndivyo radi zikawa zinazidi haliyakuwa mvua imekata na jua limechomoza majirani wakawa wanatuangalia tu tunachofanya maana ilikuwa tunafanyia barabarani kabisa ya nyumbani,akaletwa mbuzi akachinjwa alafu akaachwa bila kichwa kumalizwa,unaambiwa mbuzi alikuwa anaruka zaidi ya nusu saa mwsho kabisa akafa akifa amesimama yah ndiyo alikufa akiwa amesimama kabisa huku shingo inaninginia baada ya dua tukamwachia mungu atupe majibu yake,lakini tukaambiwa kilichoibiwa kimeibiwa hvyo hata kikirudishwa haturuhusiwi kukipokea.
Kilichofata usiku ule ule majirani zetu wawili ambao siku ya tukio walikuwa mwanza walichomana visu vya moyo nakufa ote,Asubuhi kuna mzee mmoja jirani yetu ambae pia siku ya tukio alikuja kutupa pole alipata maumivu makali ya kichwa na kujipiga kichwa ukutani mpka mauti,inshort mpka siku ya 5 baada ya tukio walikuwa watu 10 ambao nawajua mtaani maana ilikuwa ni aliyeiba,aliyeshiriki,ote mungu awaadhibu naam ilikuwa ni adhabu mpka leo ukisahau simu yako barabarani unaikuta.
Hyo ndo experience yangu ya kuvamiwa na majambazi japo kuna baadhi walikuja kuomba msamaha na kurudisha vitu na hata kutoa fidia lakini hatukuweza kuvichukua au kuweza kusamehe tena japo roho ziliturudi ila ndo hvho vifo viliendelea ndani ya siku 10 mfululizo i hope kama binadamu unaweza kujua tulikuwa katika mtihani gani japo tulifanya kwa hasira ambayo iligeuka huzuni
asante mungu yalipita
Sent using Jamii Forums mobile app
Msalimie Kamanda MachotaHome Boy kabisa wewe. Mi bado nipo pande hizi Mzee