Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Hauna tofauti na wale wanaobisha kuwa hakuna uchawi.
My friend uchawi ni imani, mimi nazijua hadi kanuni za uchawi.

Siku yakupate ndipo utajua ukweli ni upi.
Laiti ungelijua laiti ungelijua usingeandika hivi!

Hao majambazi wenyewe skills za kutumia silaha wanatofautiana.
mmh real?

Njoo kwetu nikuoneshe mmoja aliyevamiwa baani kwake (tena hata hapana hadhi ya kuitwa baa) jamaa walikosa huko walipokuwa nwanaenda. Walikuja hapa na kuanza kurusha rissi hewani mfululizo (zilipigwa zaidi ya risasi 10). Acha kubisha ndgu.
Tafadhali utaje huo mkoa kisha utafahamu kwanini mimi nabisha.

Pia majambazi hupiga risasi sio chini ya mbili kwenye tukio (moja hupigwa iwapo kuna yowe zinapigwa, hivyo wanawatisha raia) moja ni kuzuia watu kusogea eneo la tukio na nyingine wanapiga wakati wanaondoka ili kuwatisha watu wasiwanyatie.
Ndio maana ukinisoma hapo juu nimesisitiza kabisa huu ni uzamani uhalifu wa kimazoea sasa hivi fanya hivi uone zile story mnazopiga mitaani kwamba askari watasubiri tukio liishe hutaziona dk chache tu.

Note; kuna maeneo bado yana changamoto hasa yanayopata wahalifu kutoka nje mfano ni Kigoma na Katavi wahalifu wake wengi wana bunduki za kivita hasa AK na wengine wana matoleo advanced zaidi ya AK hasa wakutoka Burundi hivyo bado hutumia njia hii lakini vijana wa JKT naona wamemwagwa wa kutosha.
 
Dereva wako ndio aliwasomesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu shusha nondo

tatizo lugha
 
Mtoa post umenikumbusha sana mitaa hiyo ya Buzuruga, Nyakato (Mecco,Sokoni,National, n.k) na Igoma.

Baba yangu mkubwa aliyekuwa mstaafu wa kitengo (TISS) alivamiwa nyumbani kwake maeneo ya MWANANCHI, eneo jirani kabisa na BUZURUGA. Mzee huyu aliwahi kuwa mtumishi wa kitengo enzi za Mwl.Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Wakati anavamiwa alikuwa na umri wa miaka kati ya 65 - 70.

Basi bwana, majambazi 4 waliingia ndani ya nyumba yake na wengine ambao idadi yao ilikuwa haijulikani walibaki nje. Majambazi 2 walimweka chini ya ulinzi hapo sebuleni, huku wengine wakienda vyumbani kuwateka na kuwaleta sebuleni Wanafamilia wengine.
Wakati majambazi wale majambazi wengine 2 wakielekea vyumbani Mzee akawacheki 'kiintelijensia' wale majambazi waliopewa jukumu la kumweka chini ya ulinzi, akaona mmoja wao alikuwa ameshika bunduki yake kishamba shamba (kwa namna ambayo mtu wa kawaida hawezi kujua kama jambazi yule alikuwa ameshika silaha yake kindezi).

Basi Mzee alimlia timing yule jambazi mmoja, kisha akaruka kwa namna ya kushangaza na kumpiga teke yule jambazi hadi akaangusha silaha na Mzee akaidaka bunduki ile kwa speed ya umeme (yule jambazi mwingine alibaki amegutushwa sana). Mzee aliitumia bunduki ile kuwashona risasi wale majambazi 2 wakafa pale pale, na akawateka wale wengine 2 ambao aliwapeleka Polisi. Kwa ufupi, ni wale majambazi waliokuwa nje tu ndo walioweza kukimbia.

Sitamtaja jina, ila kwa wakazi wengi wa eneo la Mwananchi,Mwanza (moja ya maeneo wanaoishi watu wenye fedha zao na influential jijini Mwanza) walianza kumheshimu sana Mzee wangu yule, ambaye alifariki naturally mwaka 2014.
 
Dah pole sana,mi nawashangaa mtu hukukataa kuwapa ulicho nacho sasa mapanga ya nini yani utafikiri wewe ndo mwizi wao Ndo wenye mali! walaaniwe wote wanofanya hiyi kazi ya ujambaz.

tatizo lugha
 
Dah polen

tatizo lugha
 

Hii ungeiweka vzr kidogo. r na l zingetumika sehemu zake vzr..
Drive❌
Driver✔
Mhimbili❌
Muhimbili✔
Ubarozin❌
Ubalozini✔

Na kadha wa kadha.
 
We jamaa una visa vingi, huwenda unasimuliwa na wewe...

Maana kuna kile kisa chako kwenye uzi wa nguvu za giza ulikimbia bila kumalizia ni kwa jinsi gani mlivyomrudisha yule jini aliyekutafuna masikio yako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masharobalo namaanisha wako smart muda wote huwezi kumdhania ni jambazi!....
 
Kweli majambazi wakubwa wengi ni wapole sana na ni smart ukimtathimin huwezi kukubali kuwa huyu mtu ni zaidi ya hatari.
Kuna jamaa mmoja alikuwepo maeneo ya nyumbani yani jirani tu,ila tulikuwa tunajua kuwa jamaa ni jambazi .Ila hutasikia eti katuhumiwa kwa kesi yoyote pale mtaani ,jamaa anakitambi kanawili mda wote kachomekea kama afisa fulani,utakaa mda kidogo haonekeni maeneo ya nyumbani inapita kama wiki hivi mnasikia tukio mahali fulani baada ya kama wiki mbili na yeye munamuona,alikuwa hawezi kufanya tukio kalibu,jamaa anasafiri kwenda kupiga ,nyumbani walaaaa hagusi kabisa.

Mara ya mwisho alisafiri kwenda kupiga mahali maeneo kama ya kahama kwa mwalabu fulani ,yule mwalabu alikuwa kachimba shimo ndani ,walipovamia yule mwalabu akatambaa na mfeleji unaotoka ndani mwake chini kwa chini akatokeza nje,yule jirani yetu yeye alikaka kwa nje na siraha akiwalinda wenzake waliokuwa ndani ,yule jamaa akapigwa risasi na mwalabu ,wale wengine walivyoona hivyo wakashituka mlio wa bunduki ni tofauti wakatoka nje.
Walijibizana kwa risasi sana pale na yule mwalabu.wakambeba jirani yetu wakakimbia nae damu zinamtoka hadi polini,yule jilani akawaambia wale jamaa ,jamani mimi siponi nyie ondokeni,wakamkalisha chini kwenye mti akaegemea pale,ulipokuja ule mwano unafuatilia ndo wakamkuta mzee jibaba kasharejesha roho kwa Muumba.

Baada ya siku mbili tukasikia John kafariki,ndugu wakaelezea mchongo mzima mana kazi yake ilikuwa inajulikana, ndo ikawa mwisho wa kumuona tena John pale kitaa
Ila ule ukoo wao kalibia wote walikuwa majambazi,ilikuja ikawa kila likitokea tukio la uharifu defender inatimba pale kwao kwa wale ndugu zake,wanaenda kutoa maelezo.kuna kaka yao mmoja anaitwa Hitler, kasumbua sana maeneo ya shinyanga pale.Ulikuwa ukimuuliza anakwambia kabisa mimi ni jambazi na wala siwezi kuibia masikini.ilikuwa ikitokea tukio mahali jamaa lazima asafiri mana anajuwa ataijiwa tu,yaani jamaa alikuwa anakuja kuchukuliwa na polisi wala hofu hana anapiga stori tu na polisi hadi kituoni,akionekana hausiki anatolewa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka tuliwahi kumpangisha jambazi home,polisi siku hiyo wakastukiza home saa 8 usiku aisee kilitembea kipigo sisahau halafu yule boya hakuwepo siku ile zaidi ya mkewe, jamaa ukimuona hafananii kabisa
hv hukuwahi kuwa na mwanaume jambaz ww¿ maaana mmmmh
 
Duuuh, John kanisikitisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…