Tukutane hapa tunaozichukia simu kubwa, tunapendelea zaidi simu ndogo tunazoweza kuzimudu kiganjani kiurahisi

Tukutane hapa tunaozichukia simu kubwa, tunapendelea zaidi simu ndogo tunazoweza kuzimudu kiganjani kiurahisi

Hicho kama kitochi tu, kwa sasa tupo zama za simu janja (smartphones) na ndizo zinazohusika hapa.

Waptrick umenikumbusha mbali, nakumbuka shuleni 2007 nilikuwa na rafiki ni mtoto flani wa jaji ana nokia nzuri, nikimwazima simu naweka vocha ya jero hapo nashusha ngoma mbili tu,
Hii chai vocha ya jero😅
 
Hii chai vocha ya jero😅
Hakuna vifurushi enzi hizo kwenye internet unabanikwa mzima mzima na salio utaloweka. mb 1 shilingi 100 na mp3 ina mb 2 hadi 3

vifurushi vya data vimeanza nadhani miaka ya 2012 kuja mbele huku mwamko wa internet ulivyaonza kukua, wengine mambo ya net ni tangu enzi hizo tunazamia internet cafe .
 
Japo simu ni swala binafsi. ila ukubwa na udogo wa kimahitaji unatofautiana kulingana na matumizi ya mhusika wa simu hiyo. mfano wapenda kuchati_ simu ndogo, slim na portable. wanaopenda movie_ simu kubwa, big screen etc
 
Aisee nimetumia Iphone 5s miaka 6😂😂 simu ikishakua kutype hadi utumie mikono miwili siwezi.
 
Yaani siku hizi ukienda madukani simu nyingi sana za kisasa (smartphones) huwa ni kubwa kwa umbo, yani urefu tu ni kama mkebe na hii ni kero kwangu, binafsi napendelea zaidi simu ambazo zinakaa fresh kiganjani walau zikizidi sana basi iwe ni sentimita 14 na nusu kwa urefu,

Simu kuziweka mifukoni imekuwa hadi uwe na mfuko mrefu kiasi watu hulazimika kuzibeba mikononi na pindi unapotumia inakulazimu utumie mkono wa ziada ama kuishusha na kuipandisha kwa kiganja.

Hakika kwa sasa matoleo ya simu yanazidi kuongeza ukubwa na hili ni tishio kwetu tunaopenda vipotabo
Matumizi ya simu kufanyia kazi nyingi yameongezeka sana kuliko miaka ya nyuma; sasa hivi watu hutumia simu kama Komputa kwa kufanya kazi zao mbalimbali na hii ndio imefanya screen ziwe kubwa. Kama simu yako ni ya kupiga, kutuma meseji na kusikiliza muziki, naungana na wewe kuwa unastahili screen ndogo.
Kimsingi kampuni za simu zinatoa matoleo yote (ndogo na kubwa) ili kila mtu anunue anayopenda
Mfano: ukisikia Iphone 12 (hiyo ni ndogo), ila ukisikia Iphone 12 pro max (hiyo ni kubwa)
 
Simu kubwa mara simu ndogo mara mnasema kibamia mara mtasema hampendi "tango" dushe kubwa.
Watu wa dunia hivi kila kitu kwenu ni issue.
 
Nachukia simu ndogo kwa kweli. Nikitumia simu ndogo hata nafsi inanisuta [emoji18][emoji18]
 
Nikitumia simu kubwa Sana mwisho 6.4, sasa hivi nipo 6.2 S21...sipendi simu kubwa.
 
Back
Top Bottom