Usituku
Usitukumbushie maumivu na madudu ya uchaguzi wa 2020 we mama. Bado tuna hasira na uchafu ule. Haiwezekani mtumie mabilioni ya kodi za watanzania maskini kisha mvuruge na kupora haki Yao ya kuchagua viongozi wao. Na kibaya kukiuka katiba ya nchi ambayo mlishika biblia takatifu mkaapa kwa Mungu kwamba mtailinda na kuifuata. Ee Mungu Mwenyezi ikupendeze kutoa hukumu za haki kwa wote wanaotufanya watanzania kuwa watoto na wajinga. Tupo tayari kuomboleza Ee Mungu tunakuomba utujibu kwa haki kwasababu Wamelinajisi agano lako nawe Mungu.Spika Tulia amesema wanaoamini nguvu ya dola ilitumika 2020 kuwaingiza wabunge wa CCM bungeni ni imani tu na hakuna mtu ameona mahali. Amesema nchi hii ina utaratibu wa kwenda mahakamani kuonesha imani yako inaposimamia na maeneo mengi watu wanafunguliwa kesi za ubunge na wapo walioondolewa huko nyuma.
Amesema kuhusu yeye na jimbo la Mbeya, amewataka waandishi waende Mbeya waone mpango wa wananchi wa Mbeya mjini.