Tulienda shule kufanyaje kama hata hizi kazi za muda wanapewa watumishi wa serikali

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Je umuhimu wa Degree zetu upo wapi huku mtaani, tunasota na tunahangaika na mabahasha kutafuta ajira huku serikali ikiweka ahadi kede kede ambazo hazitekelezeki

Haya hata hizi kazi mbalimbali za muda ambazo zingekuwa hata kifuta machozi kwetu Kwa kupunguza machungu ya kukaa mtaani bila ajira nazo sasa hivi wanapewa watumishi wa serikali je sisi tukale wapi yani tumesoma na bado tunaishi Kwa stress hii sio fair kabisa ni muda sasa wa serikali kuona ni namna gani hawa wasomi ambao hawana ajira wanaweza kupewa fursa mbalimbali huenda zikaenda kuwa sehemu ya kupata mtaji kwao na kufanya shughuli zao nyingine bila kuitegemea serikali tena
 
Umeandika utadhani wote wameona tangazo.
Labda tu niwasaidie ambao hawatoelewa ni hivi serikali imetangaza nafasi uandikishaji wa majina ya wapiga kura serikali za mitaa na kigezo namba moja ni uwe mtumishi wa umma.

Nikirudi kwenye hoja yangu ni kweli kwenye mfumo kuna shida sehemu japo mimi sijawahi kuwakubali upinzani hata siku moja na moja ni kama hii wamelala vibaya mno.
Nilitegemea muda kama huu wawe wameshafika mahakamani kuweka pingamizi au kuingia hata barabarani kupinga hii hatua lakini walivyo wehu na vichaa wote kimya mitaa vitongoji na vijiji wakichukua ccm wataanza kulia lia hapa poor upinzani.
 
Wao wanazani upinzani ni kuandamana tu, Pathetic
 
Mfumo wa uandikishaji uatumia BVR na Vishikwambi ambavyo ni vya bei ya juu Kwahyo wanaogopa kuwapa watu ambao sio watumishi wasije kuondoka na vifaa vya serikali ndio maana wanatumia watumishi ili wakialibu wanapakuwataftia.
Kwani siyo watanzania kwamba hawatapatikana Tena? Sema mifumo ya upigaji tu inatutesa watanzania.
 
Kwani tangu lini Mahakama za Tanzania zikatoa haki kwa vyama vya upinzani?

Anyway hapa nani mwehu Kati yako wewe na hao upinzani? maana kesi ipo mahakani na imetoka kusikilizwa trh3 September
 

Attachments

  • Screenshot_2024-10-03-17-42-46-387_com.android.chrome.jpg
    273.5 KB · Views: 7
Kama waliokopeshwa na bodi ya mikopo vyuo vikuu lkn wako nje ya ajira kuwapata inakuwa tabu itakuwa vishikwambi?
Umesema wapo nje ya ajira. Sasa hata wakiwafahamu Bado hawataipata Hela Yao maana hawana ajira. Kingine ni uzembe wao tu au ni impact ya kuongozwa na watu waliopata nafasi Kwa kujuana.
 
Mfumo wa uandikishaji uatumia BVR na Vishikwambi ambavyo ni vya bei ya juu Kwahyo wanaogopa kuwapa watu ambao sio watumishi wasije kuondoka na vifaa vya serikali ndio maana wanatumia watumishi ili wakialibu wanapakuwataftia.
Hapa mnachanganya mambo mawili kuwa kitu kimoja kuna zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura ambalo lilizinduliwa na waziri mkuu kasim majaliwa mkoani kigoma na kuna zoezi la uandikishaji wa majina ya wapiga kura serikali za mitaa.
Sasa zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura kwa kutumia BVR linajumuisha watu wte maana tangazo lilitolewa na INEC na linaenda kwa awamu.
Ila uandikishaji wa majina ya wapiga serikali za mitaa linaanza kuanzia tareh 11 mwezi huu ndilo linahitji watumishi pekee kushiriki zoezi hilo
Kumbuka zoezi hili la serikali za mitaa haitaji uwe na kitambulisho cha mpiga kura bali inahitaji jina liwepo tu kwenye orodha
 
Fvck CCM
 
Ili wale vipondo na kusaga meno??
 
Uko sawa kwa sababu elimu yetu inatuandaa kuajiliwa siyo kujiajiri
 
Mfumo wa uandikishaji uatumia BVR na Vishikwambi ambavyo ni vya bei ya juu Kwahyo wanaogopa kuwapa watu ambao sio watumishi wasije kuondoka na vifaa vya serikali ndio maana wanatumia watumishi ili wakialibu wanapakuwataftia.
Uongo huu Mkuu hii sio sababu kabisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…