Tulienda shule kufanyaje kama hata hizi kazi za muda wanapewa watumishi wa serikali

Tulienda shule kufanyaje kama hata hizi kazi za muda wanapewa watumishi wa serikali

Je umuhimu wa Degree zetu upo wapi huku mtaani, tunasota na tunahangaika na mabahasha kutafuta ajira huku serikali ikiweka ahadi kede kede ambazo hazitekelezeki

Haya hata hizi kazi mbalimbali za muda ambazo zingekuwa hata kifuta machozi kwetu Kwa kupunguza machungu ya kukaa mtaani bila ajira nazo sasa hivi wanapewa watumishi wa serikali je sisi tukale wapi yani tumesoma na bado tunaishi Kwa stress hii sio fair kabisa ni muda sasa wa serikali kuona ni namna gani hawa wasomi ambao hawana ajira wanaweza kupewa fursa mbalimbali huenda zikaenda kuwa sehemu ya kupata mtaji kwao na kufanya shughuli zao nyingine bila kuitegemea serikali tenaView attachment 3114078
If you want a peace start a war!!
 

Attachments

  • FB_IMG_1728023755203.jpg
    FB_IMG_1728023755203.jpg
    52.1 KB · Views: 2
Umeandika utadhani wote wameona tangazo.
Labda tu niwasaidie ambao hawatoelewa ni hivi serikali imetangaza nafasi uandikishaji wa majina ya wapiga kura serikali za mitaa na kigezo namba moja ni uwe mtumishi wa umma.

Nikirudi kwenye hoja yangu ni kweli kwenye mfumo kuna shida sehemu japo mimi sijawahi kuwakubali upinzani hata siku moja na moja ni kama hii wamelala vibaya mno.
Nilitegemea muda kama huu wawe wameshafika mahakamani kuweka pingamizi au kuingia hata barabarani kupinga hii hatua lakini walivyo wehu na vichaa wote kimya mitaa vitongoji na vijiji wakichukua ccm wataanza kulia lia hapa poor upinzani.
Hata wewe unaweza kwenda mahakamani ukastopisha hiyo issue haliitaji daktari hiyo.
 
Kwani wanalipa hela kiasi gani mpaka zinakutoa roho?
 
Hata wewe unaweza kwenda mahakamani ukastopisha hiyo issue haliitaji daktari hiyo.
Chief mimi siwezi maana mimi ni mwanaccm na kadi yangu inasoma yaan kwa aina hii ya upinzani niangaike nao?
 
Mstaafu anaweza pata hizi kazi ila sio jobless wa mtaani mwenye degree😅
 
Back
Top Bottom