Hilo ndio tatizo kubwa na la msingi, na halijaanza kupigiwa kelele leo.. Zamani zile za Flying horse bandari ya Zenji ilikuwa inafungwa saa nne usiku kwahiyo inabidi chombo kiondoke bandarini na kwenda kupaki huko katikati ya bahari mpaka saa tisa alfajiri ndio kianze safari ya Dar.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bank karibu zote muda ukiisha ukiwa ndani huduma zinaendeleaCRDB waliwahi kufunga mlango tukabaki mimi na wahudumu tu na muda ulikuwa umeshaisha. Walicheza na tatizo langu hadi likaisha. Akaunti ilikuwa inakubali kutoa pesa tawi moja tu tena kuna mhudumu ndio alikuwa anaipatia.
Mimi nadhani ni kwaajili ya usalama, usiku sio salama kushusha!Sijui mkuu, wanasema ndio utaratibu. Niliongea na baadhi ya abiria wakasrma walishangaa kuona inaondoka Zanzibar saa 9:43. Kawaida unaambiwa Boat inaondoka saa 3 usiku ila ukipanda inakaa mpaka saa 6 au 7 usiku ndio inaondoka ili ifike Dar saa 12 asubuhi. Nilizan ni kwa ajili ya ukaguzi lakini tuliposhuka tulitokea yanapotokea magari na hamna mtu anakagua mtu.
Wewe sio tu ni lofa bali mfu.Zanzibar to Dar masaa 6? Utakuwa ulipanda ngalawa lofa wewe!
Acha ushamba, kuna siku utajua kuwa bank hazifungwi saa 10.30 bali saa 2 usiku.ππHii Chai asubuhi hii.
Sasa kuna mthenge nyuma hapo anasema chai, sijui kama hata ana akaunti. Mimi akaunti ilikuwa na shida, sasa wao benki wakawa wanawasiliana na kitengo fulani kipo mjini. So milango ikafungwa nikabakia mimi tu hadi wale jamaa walivyorekebisha.Bank karibu zote muda ukiisha ukiwa ndani huduma zinaendelea
Mliambiwa dp world anafanya local?Dar to Zanzibar?Usitetee vitu vya ajabua ajabu,
Kwa nini bandarani hawafanyi kazi masaa 24?
DP World hawajaanza kufanya kazi??
Soma thread yote kabla ya kumshambulia mtu...Hapo bandarini hakuna wahudumu na maafisa usalama muda wote ambao wangeona kuna boti imefika ila haishushi abiria wakaulize shida ni nini?! Huu ni ufanyaji kazi wa wapi??
Wewe utakuwa na wajomba zako wanaofanya kazi bandarini unawatetea.
Mkuu tuongee ukweli,kazi inakua bandarini haijafunguliwa mda huo,so inabidi msubiriKuna boat ya kutoka Zanzibar saa tatu usiku inatembea mwendo mdogo sana inaingia Dar saa tisa usiku. Abiria hamruhusiwi kuteremka Hadi ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.
Ni boat nzuri na ya kisasa, sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona... Sijui wahusika hawajaliona hilo
Huo mfano wako ni wa USA au usa river?maana hata huku bongo ni hivyo hivyo,muda wa kufunga unahusu walio nje sio ndaniWanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkonoπ
Nafikiri iko hivi ..kule Zanzibar wafanyakazi WA mamlaka husika mwisho Saa nne ndo maana wenye hiyo meli wakalazimisha waondoke Saa tatu badala ya Saa sita ili wawe cleared na mamlaka za Zanzibar...halafu wakishatembea masaa kadhaa wanawahi kutoka huku...ndo maana wanakaa na abiria majini....kama wangeruhusiwa kutoka Zanzibar saa sita wangefika huku asubuhi...kusingekuwa na shidaJe, inawezekana muda huo wa usiku hakuna boti na meli nyingi za abiria zinashusha, hivyo wanaona ni hasara wafanyakazi kukesha wakati abiria wanaowasili ni wachache?
Meli ya mizigo inaruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria?Soma thread yote kabla ya kumshambulia mtu...
Umeambiwa meli ya mizigo na sio boat na huo ndo mda wake wa kawaida .....why ushambulie mtu kabla ya kupata facts?
Kwenye usalama kupitia mabasi ya abiria hapo ndipo tunafeli sana, yaani nimeondoka mpanda saa 11 na kuja na basi uku dar hakuna askari alieingia ndani kukagua zaidi ya askari wa tochi (trafiki) kumalizana na kond wake chini.Nikawa najiuliza inamaana jasusi au mtu akivuka toka nchi jirani akitokea mpanda ni kazi raisi kwake kuja makao makuu ya nchi dodoma na kuja sehemu nyinginw ya nchi.Wanazungumzia usalama wakati bus likifika huo muda linashusha Nchi hii ina mambo ya ajabu sana na bila jamaa kuandika hivyo tusingejua kuwa bado tupo kwenye giza...
Anataka afike mapema alale zake.We kuweza???Ndiyo maana zamani hizo boat ilikuwa zinakaa sehemu usiku zinaelea hadi saa sita usiku ndiyo zinaanza safari ili zifike Dar alfajiri..
Halafu hata huyo nahodha wa boat ni mpuuzi kwanini asikadirie speed anayotembea ili afike asubuhi badala ya kuingiza watu usiku mkubwa?.
Sasa ni hivi, bandari zote za Zanzibar na Tanzania bara wanatakiwa wafanye kazi masaa 24, uvivu na kupenda kulala sana ni sumu kwa maendeleo.Nafikiri iko hivi ..kule Zanzibar wafanyakazi WA mamlaka husika mwisho Saa nne ndo maana wenye hiyo meli wakalazimisha waondoke Saa tatu badala ya Saa sita ili wawe cleared na mamlaka za Zanzibar...halafu wakishatembea masaa kadhaa wanawahi kutoka huku...ndo maana wanakaa na abiria majini....kama wangeruhusiwa kutoka Zanzibar saa sita wangefika huku asubuhi...kusingekuwa na shida
Mbona unaongea Kwa hisia zako?Meli ya mizigo inaruhusiwa kufanya biashara ya kubeba abiria?
Kama meli ya abiria inaruhusiwa kubeba na abiria basi ilipofika bandarini tu maafisa wa bandari walipaswa kushituka angalau ndani ya nusu kwamba kuna meli imetia nanga ila abiria hawashuki.
Kwanza ni kosa kubwa mno la kiusalama kuwaacha watu bandarini masaa matatu ndani ya chombo bila kujua wanachofanya huko ndani au wana hali gani.
Zinatakiwa Kwa mujibu wa Nani?Sasa ni hivi, bandari zote za Zanzibar na Tanzania bara wanatakiwa wafanye kazi masaa 24, uvivu na kupenda kulala sana ni sumu kwa maendeleo.
Wewe biashara yako unafanya usiku kucha mkuu??πππIla masikini tuna vituko. Hivi na huu umasikini na unemployment ya kutisha, tunapata wapi ujasiri wa kulala usingizi? Kabisa?
Personally naamini hakuna biashara inayostahi kufunga usiku. Waajiri watu wapokezane/wapeane shift.