Kuna siku ilinipata hiyo kadhia nikitoka Dar kwenda Zanzibar, tulipanda zile Azam Sea Link ( sio speed boat) ni ya mizigo, magari na abiria wengi zaidi ila Mara nyingi inasafiri usiku.
Tulifika Unguja saa tisa usiku na tuliruhusiwa kushuka Kwa vile kulikua na magari ya BoT ya kusafirishia pesa kwenye hiyo meli.
Turudi kwenye hoja ya mleta Uzi.
Zile meli Mara nyingi zinapakia abiria na kushusha eneo la bandarini, sio huku kwenye speed boat. Hapo inabidi wahusike maofisa wa usalama, TRA, Bandari na wenye chombo wenyewe, ina maana ikiwa mojawapo ya maofisa kati ya hao hapo juu hawatakuwepo, ni nadra sana mizigo na abiria kuruhusiwa kushuka usiku.
Flying Horse siku hizi safari zake ni Unguja - Pemba.
Hitimisho, kama una haraka na hauwezi kuchukua mwewe, Bora usubirie boat ya saa moja inayofika saa tatu kasorobo. Vinginevyo ukubali kubaki kwenye chombo hadi papambazuke.