Tulilalamika sana siasa kuingilia Utendaji. Sasa tumeanza kuvuna matokeo yake

Tulilalamika sana siasa kuingilia Utendaji. Sasa tumeanza kuvuna matokeo yake

Wa kulaumiwa ni CCM
Yalianza kama masikhara ila sasa tuvumilie kuvuna matunda yake.

Kuanguka kwa Tanzania ni suala lililochukua muda kidogo. Tuliopata nafasi ya kuonya, tulionya ili kulikomboa Taifa ila hakuna yaliyofanyika na matokeo yake ndo haya tunayoyaona leo.

Ilianza kwa kuanza kutoa nafasi za utendaji Serikalini za Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa Makada wa Chama cha Mapinduzi.

Tuliopewa macho ya rohoni tulionya kuwa suala hili lilikuwa linaenda kuharibu sehemu nyeti ya Utumishi nchini kwa sababu watu hawa ni watu wanaopaswa kupatikana kwa merit kutokana na kuwa sehemu muhimu ya maamuzi nchini hivyo ni vizuri masuala ya competence, integrity, experience na exposure kuzingatiwa kwenye teuzi zao ila kwa kuwa CCM waliamua kupuuza maoni ya wenye akili walitupuuza kwa maslahi yao ya muda mfupi.

Haikuishia hapo. Siasa ikaingia hadi kwenye majeshi na vyombo vya Ulinzi. Kubadilishwa kwa Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa zaidi ya mara 4 ndani ya miaka 3 ni kielelezo kingine kuwa Siasa ilianza kuingia huko.

Kupandishwa vyeo kwa maofisa wa Polisi wanaoonekana kuzungumza mbele ya vyombo vya habari masuala yanayowafurahisha wanasiasa nako kuliendelea kuonesha kwa namna gani siasa imeingia kwenye vyombo vyetu hivi.

Matokeo ya haya:
1. Sasa Tanzania imepoteza nafasi yake ya kuwa Think Tank na Main determinant wa Siasa za Maziwa Makuu. Nafasi hii wamechukua Rwanda na Uganda baada ya kufanikiwa kupenyeza mamluki wengi kwenye mfumo wa Tanzania. Sasa Rasmi Rwanda anaenda kuichukua Mashariki ya Congo.

2. Mfumo wa Maamuzi wa Tanzania umeshakuwa fully penetrated na Majasusi wa Bahima Empire. Inasemwa sehemu nyeti zote zimeshakuwa Penetrated. Hadi sasa Naibu PM wa TZ ni product wa Bahima Empire. Na onasemwa BOT, Hazina, Mipango kote wamejaa wao.

3. JWTZ kuanza kuwa Jeshi la Kisiasa na kupoteza nafasi yake kama Jeshi Bora na linaloheshimika Afrika Mashariki. Jeshi hili saivi limekuwa Jeshi la Maonesho, kupenda sifa badala ya Jeshi la Mikakati na Mipango Kabambe. Kichapo walichokipata huko Congo hadi saivi Malawi wameamua kuondoka ni kielelezo tosha.

4. Kukwama kwa mipango kabambe ya maendeleo ya Taifa. Hii ni kwa sababu nafasi za DED, KM na RAS zimeshikwa na makada wa Chama cha Mapinduzi ambao wao kazi yao ni kuangalia uhai wa Chama cha Mapinduzi ila sio mustakabali mzuri wa Taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Watu hawa hawawezi kufanya analysis ya masuala ya msingi zaidi ya kuangalia siasa na Chama chao ambacho wanaamini bila hicho wasingekuwepo hapo.

Kwenye haya maamuzi mengi sasa yamekuwa yakifanywa kwa mtazamo wa kisiasa na sio kwa ajili ya kuijenga Tanzania imara Kiuchumi na Kimaisha kwa miaka mingi ijayo.


5. Kuibuka kwa watu ambao kazi yao ni kuwalamba miguu Viongozi na Kuwasifia huku wakilipwa fedha ambazo ni kodi za wananchi. Watu hawa wanaharibu vijana kwa kuwaonesha kuwa maisha ni kuwa Chawa na inawezekana usijishughulishe na kufanya kazi kwa bidii ila ukawa chawa wa kiongozi na maisha yakaenda.

6. Kuendelea kushuka kwa kiwango kikubwa na cha kutisha masuala ya Utawala Bora na Utawala wa Sheria. Hili linapelekea wananchi wenye mawazo tofauti kutekwa, kuuwawa na wengine kupotezwa bila hatua zozote kuchukuliwa.

Matukio ya Soka, Ben Saanane, Mzee Kibao na Sativa ni mfano mdogo tu wa wapi tumefika kama Taifa.

Poleni sana Watanzania.

Kilaaniwe CHAMA CHA MAPINDUZI.

Tupambane kufa na kupona tupate KATIBA MPYA.
 
Walio ndani ya CCM wenye kutaka Katiba mpya ni wengi kuliko wasioitaka,

TUNDU Lissu aanze tu, watamalizia wengine.
Sasa wameshajua ni kitu gani alimaanisha Mwalimu Nyerere alipotoa tahadhari kuhusu Katiba !!

Wameshazijua nguvu za yule aliyepewa na Katiba akitaka kuzitumia inakuwa ni patashika nguo kuchanika hata huko Chamani kwao 😳 !

Watu huwa wanapatwa na vigugumizi vya ghafla kwa kuziogopa Nguvu za Kiti ambazo wanazijua na wanajua nguvu hizo anatembea nazo kila mahali mpaka hapo kwenye kikao chao nguvu zile zimejaa tele kama pishi ya mchele ! 😅😅😂😂

Wanajua mtu akijichanganya tu kwa kuleta ujuaji au kiherehere ajue itakula kwake 😅😂 !!
Locuta causa finita 🙏🙏🙏 🙌
 
Magufuli atabakia kuwa tatizo kwa muda mrefu
Magufuli ndiye aliyewafumbua macho watu kuziona na kuzijua nguvu alizopewa Rais wa Nchi katika Katiba yetu iliyopo !

Maana Nyerere alipoonya kuhusu nguvu za Rais zilivyo kwa mujibu wa Katiba watu wengi hata hao wakubwa hawakumuelewa Mwalimu !

Lakini baada ya Magufuli kuzionyesha nguvu zile japo kidogo tu sasa nadhani baadhi yao ambao wanaendelea kukutana na hizo Nguvu hata sasa watakuwa wameanza kuamini ule wasiwasi aliouonyesha Mwalimu kuhusu Katiba ile 😳 !
 
,MAPATO YA KWENYE SIASA YAPUNGUZWE. YAENDANE NA UHALISIA WA UCHUMI WA NCHI NA WANANCHI NA SIO KUPIGA DEALS KAMA SASA!!
Hili ni la mhimu sana. Sio sawa daktari, mwalimu, na wataalamu mbalimbali walijopatia maarifa kwa gharama kubwa, na wanatimiza majukumu nyeti, walipwe 600,000~3,000,000, wakati wapayukaji wakijolipa 18,000,000.
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.




Siungi mkono hoja
Unachotakiwa kukifahamu kwanza kabisa ni kwamba kukitokea mabadiliko yoyote ya utawala wa chama kuondolewa madarakani sio kwamba eti watumishi wote wa Serikali na taasisi zake watakuwa wamepoteza kazi zao !

Watumishi wote wa ngazi zote wataendelea kubaki kwenye ofisi zao kama walivyokuwa kabla ya Uchaguzi !

Watakao badilika ni wanasiasa tu na porojo zao za siasa lakini wataalamu na watendaji wote watabaki ni wale wale under new administration !

Ofisi yeyote utakayokwenda baada ya kung’olewa Chama kilichoshindwa Uchaguzi utawakuta watumishi ni wale wale waliokuwepo siku zote kasoro yule wa Majukwaani ndiye atakayekuwa amebadilika kwenye hiyo ofisi uliyokwenda , !
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.




Siungi mkono hoja
Hii comment ni ya kijinga kiwango cha PHD. It's garbage from a dustbin (DustBin).
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.




Siungi mkono hoja
Tumia akili kufikiria,
 
Nyumbu wa Chadomo Huwa mnajijaza upepo sana sijui Kwa nini 😁😁

Ndio maana mnapuuzwa na Nchi inazidi kusonga.

Hao uliowataja wanakuja hapa Tanzania siku sio nyingi kupata miongozo au hujui?
[/QUOT
Nyumbu wa Chadomo Huwa mnajijaza upepo sana sijui Kwa nini 😁😁

Ndio maana mnapuuzwa na Nchi inazidi kusonga.

Hao uliowataja wanakuja hapa Tanzania siku sio nyingi kupata miongozo au hujui?
Acha ujinga basi
 
Zanzibar wana GSO. HII ni idara ya kuidhinisha ajira baada ya usaili wa kitaaluma kukamilika.

Idara inaangalia utiifu kwa CCM.

Inasikitisha sana, Zanzibar ndio kumezidi hasa, kila kitu uwe mwanachama wa CCM
 
Kweli kabisa.

Tuombe Mungu watokee kama Traole JW na TISS
Labda Kagame au Malawi watupige tupime uzalendo wetu kama watakuwa sawa na wakati wa Nyerere. Lakini tofauti kubwa ya kipato cha chini na viongozi/watawala wetu inaua uzalendo. Mfano: Kiongozi analipwa mioni 5 kwa mwezi na kima cha chini laki 4 kwa mwezi,, uzalendo utatoka wapi.
 
Huko Jeshini ndio hamna kitu sababu siasa imeingia jeshi limekuwa sio kuandikishwa bali limekuwa ajira. Ahahahahaaa.

Cha ajabu ndani ya jeshi ni ccm na ccm ni Jeshi, yaani hata ukitamka neno au jina la Tundu Lissu utafuatiliwa na wanojiita usalama ndani ya jeshi na utaundiwa mizengwe.

JWTZ ni jeshi la ccm, na ikitokea vita hata na rwanda tunaweza pigwa kama paka aliyekula mayai.

Kipindi cha 2016 hadi 2021 wanajeshi wengi walisingiziwa kujihusisha na siasa au kumtukana magufuli. Iwe ni kwa kusoma story au ku comment ujumbe huko kwenye mitandao ya kijamii.

Jeshi limeozaaa kabisaa.
Kwa hali hii, siku tukivamiwa,, serikali itathubutu kututaka tujitolee kulipigania Taifa letu kama wakati wa Nyerere ?
 
Back
Top Bottom