Tulilalamika sana siasa kuingilia Utendaji. Sasa tumeanza kuvuna matokeo yake

Alipotoa hoja akapigiwa makofi mengi sana hiyo ilikuwa ni kiashiria kwamba wajumbe wameikubali hoja !
Lakini Mwenyekiti alipoikataa hiyo hoja The same wajumbe wakapiga makofi mengi mengi sana kuliko walivyompigia mtoa hoja wa kwanza 😅😅🤣 !

Hapo unaweza ukaona who are these so called Wajumbe 😳 !!
Du!!!!!....
 
Yalianza kama masikhara ila sasa tuvumilie kuvuna matunda yake.

Kuanguka kwa Tanzania ni suala lililochukua muda kidogo. Tuliopata nafasi ya kuonya, tulionya ili kulikomboa Taifa ila hakuna yaliyofanyika na matokeo yake ndo haya tunayoyaona leo.

Ilianza kwa kuanza kutoa nafasi za utendaji Serikalini za Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa Makada wa Chama cha Mapinduzi.

Tuliopewa macho ya rohoni tulionya kuwa suala hili lilikuwa linaenda kuharibu sehemu nyeti ya Utumishi nchini kwa sababu watu hawa ni watu wanaopaswa kupatikana kwa merit kutokana na kuwa sehemu muhimu ya maamuzi nchini hivyo ni vizuri masuala ya competence, integrity na experience kuzingatiwa kwenye teuzi zao ila kwa kuwa CCM waliamua kupuuza maoni ya wenye akili walitupuuza kwa maslahi yao ya muda mfupi.

Haikuishia hapo. Siasa ikaingia hadi kwenye majeshi na vyombo vya Ulinzi. Kubadilishwa kwa Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa zaidi ya mara 4 ndani ya miaka 3 ni kielelezo kingine kuwa Siasa ilianza kuingia huko.

Kupandishwa vyeo kwa maofisa wa Polisi wanaoonekana kuzungumza mbele ya vyombo vya habari masuala yanayowafurahisha wanasiasa nako kuliendelea kuonesha kwa namna gani siasa imeingia kwenye vyombo vyetu hivi.

Matokeo ya haya:
1. Sasa Tanzania imepoteza nafasi yake ya kuwa Think Tank na Main determinant wa Siasa za Maziwa Makuu. Nafasi hii wamechukua Rwanda na Uganda baada ya kufanikiwa kupenyeza mamluki wengi kwenye mfumo wa Tanzania. Sasa Rasmi Rwanda anaenda kuichukua Mashariki ya Congo.

2. Mfumo wa Maamuzi wa Tanzania umeshakuwa fully penetrated na Majasusi wa Bahima Empire. Inasemwa sehemu nyeti zote zimeshakuwa Penetrated. Hadi sasa Naibu PM wa TZ ni product wa Bahima Empire. Na onasemwa BOT, Hazina, Mipango kote wamejaa wao.

3. JWTZ kuanza kuwa Jeshi la Kisiasa na kupoteza nafasi yake kama Jeshi Bora na linaloheshimika Afrika Mashariki. Jeshi hili saivi limekuwa Jeshi la Maonesho, kupenda sifa badala ya Jeshi la Mikakati na Mipango Kabambe. Kichapo walichokipata huko Congo hadi saivi Malawi wameamua kuondoka ni kielelezo tosha.

4. Kukwama kwa mipango kabambe ya maendeleo ya Taifa. Hii ni kwa sababu nafasi za DED, KM na RAS zimeshikwa na makada wa Chama cha Mapinduzi ambao wao kazi yao ni kuangalia uhai wa Chama cha Mapinduzi ila sio mustakabali mzuri wa Taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Watu hawa hawawezi kufanya analysis ya masuala ya msingi zaidi ya kuangalia siasa na Chama chao ambacho wanaamini bila hicho wasingekuwepo hapo.

5. Kuibuka kwa watu ambao kazi yao ni kuwalamba miguu Viongozi na Kuwasifia huku wakilipwa fedha ambazo ni kodi za wananchi. Watu hawa wanaharibu vijana kwa kuwaonesha kuwa maisha ni kuwa Chawa na inawezekana usijishughulishe na kufanya kazi kwa bidii ila ukawa chawa wa kiongozi na maisha yakaenda.

Kwenye haya maamuzi mengi sasa yamekuwa yakifanywa kwa mtazamo wa kisiasa na sio kwa ajili ya kuijenga Tanzania imara Kiuchumi na Kimaisha kwa miaka mingi ijayo.

6. Kuendelea kushuka kwa kiwango kikubwa na cha kutisha masuala ya Utawala Bora na Utawala wa Sheria. Hili linapelekea wananchi wenye mawazo tofauti kutekwa, kuuwawa na wengine kupotezwa bila hatua zozote kuchukuliwa.

Matukio ya Soka, Ben Saanane, Mzee Kibao na Sativa ni mfano mdogo tu wa wapi tumefika kama Taifa.

Poleni sana Watanzania.

Kilaaniwe CHAMA CHA MAPINDUZI.

Tupambane kufa na kupona tupate KATIBA MPYA.
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Siungi mkono hoja
 
Andiko Bora kabisa hili. Nipo mkoa Fulani Kwa kazi Fulani, huyu Boss anasema oogh huwezi kwenda kufanya KAZI huko Hadi tukupatie Afisa Mawasiliano maana tunataka kila sehemu CCM alimaanisha Serikali, itajwe kila kwenye shughuli
 
Huyo CDF mwenyewe anawaogopa wanasiasa kama sio CDF.

Yanayosemwa kumuhusu sio mazuri. Ajirekebishe na asimame kwenye nafasi yake kama CDF na sio kupelekeshwa pelekeshwa na wanasiasa. Aangalie wenzake kina Twalipo, Mwamunyange, Mabeyo na Mboma walivyokuwaga.

Pia Majenerali wamekuwa watu wa kujali maslahi na sio kuboresha jeshi letu. Jeshi letu halipaswi kupoteza nafasi yake kama Jeshi Bora zaidi katika kipindi chake.
Yule mabasi ya kijani yamedhihirisha yasemwayo
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Siungi mkono hoja
Haya Mawazo ya ajabu mno mno
 
Huu ni ukweli mchungu lakini utabaki kuwa ukweli tu, nakumbuka wakati ule CDF alipoonya kuhusu wahamiaji haramu kujipenyeza hadi kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi katika serikali yetu wengi waliponda na kumkejeli. Ukicheka na nyani utavuna mabua.
CCM wameharibu Nchi, sasa hivi chochote kinachofanywa ni Kwa maslahi ya CCM ibaki madarakani
 
Magufuli alifanya kwa ukubwa ujinga alioanzaga kuufanya Kikwete

Kuna ujinga mkubwa sana huwa unafanywa kumuondoa huyu jamaa kwa mauchafu yote ya nchi hii, inathibitisha udogo wa IQ za watanzania, tupo kama kuku yani, unateseka kwa njaa mwaka mzima ukija kupewa debe la mahindi siku ya mwisho na yuleyule aliyekutesa unasahau yote na kumuona ni malaika!
 
Magufuli ndiye aliyeingiza watendaji wengi nje ya mfumo bila kuzingatia uwezo. Magufuli ndiye alitengeneza compromise na Ofisi ya Taifa ya ukaguzi kwa kumwondoa Assad kwa nguvu
Yes Magufuli alifanya kwa sehemu kubwa haya ila mwanzilishi alikuwa Jakaya Kikwete
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Siungi mkono hoja
Hizi ni fikra mgando. Upinzani umeshakomaa vya kutosha kuweza kuiongoza Tanzania.

Kikubwa lazima tupate KATIBA MPYA kwanza maana bila hii tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.
 
Nchi hii magufuli aliikosea sana aisee!! Ni vile tu Watanzania wanapenda kuangalia vitu juu juu. Watanzania ni watu wa kuzuzuka na vitu vidogo vidogo ambavyo havina Future. Ila kwa watu wenye maono na jicho la kuona mbali watakubaliana na Mimi kwamba magufuli ametuharibia nchi.
 
Saana. Ila upuuzi huu ulianza hata kabla yeye hajawa Rais kipindi cha Jakaya Kikwete.

Magufuli alifanya tu na kupitiliza na matokeo yake ndo haya tunayaona leo.
 
Shida ni kwamba ukiiondoa CCM hatuna chama kingine ambacho kinaweza kutusimamia. Yaani madhara tunayopata kwa kutawaliwa na CCM ni machache sana ukilinganisha na madhara yatakayopatikana kama chama kingine kitashika hatamu, kitaifa. Hivyo ni bora tuendelee na hawahawa CCM na huku tukijaribu kuboresha madhaifu yao kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Siungi mkono hoja
Umewaza mbali sana mkuu ( nakuunga mkono) lkn huu udhaifu unaoonekana wa vyama vya upinzani unatokana na mfumo wenyewe hauko tayari kutengeneza /kulea chama mbadala wa ccm.
Vyama vya upinzani vinafanya kazi ktk mazingira magumu sana ya kuhujumiwa na mifumo usisahau Hilo pia, japo nimekuunga mkono kwa hoja Yako.
 
Yule mabasi ya kijani yamedhihirisha yasemwayo
Ajirekebishe. Akakae na Wastaafu wamwelekeze.

Taasisi anayoiongoza ni nyeti sana na ndo imekuwa inayotegemewa baada ya wanasiasa kuziharibu TISS na Polisi.
 
Tuweni wakweli, enzi za Magufuli watendaji wa serikali walikua wakifanya kazi, waziri wa maji kwamfano, enzi za Magufuli kweli alikomesha mgao wa maji, wa umeme as well; hospital ukienda una uhakika wa kuhudumiwa, hata kama dawa zilikua hazitoshelezi but kuna kazi ilikua inafanyika. Tutamkaumu Magufuli kwasababu ya chuki zetu but the guy showed the way and he made a lot of transformation in our government and it's organs. RIP JPM
Jaribu kutofautisha kufanya kazi kwa sifa au ili uonekane unafanya kazi na kufanya kazi kwa weredi.

Nafasi za Utendaji kama Katibu Mkuu ( Permanent Secretary) ni nafasi nyeti sana.

Mahali tuliporithi mfumo huu (Uingereza) watu hawa hawaondolewi hadi wanapostaafu. Ndo Think Tank wa Mawizara na Inachukua muda mrefu sana kumtengeneza mtu hadi anafikia nafasi hiyo.

Watu hawa ndo wanafanya tafiti kuhusu sera na kushauri kwenye maamuzi makubwa ya kitaifa kwa mamlaka. Wanatakiwa wawe watu wenye competence, integrity, experience na exposure za kutosha. Watu hawa huwa wenye exposure na ndani na nje ya nchi na huwa wanatengenezwa ndani ya Serikali humo humo.

Unapomchukua kijana au mtu kutoka Chama cha Mapinduzi ambaye hajui hata utumishi wa Umma, au katoka tu chuoni au katoka kufanya kazi Chama cha Mapinduzi tu unampa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu au DED unadhani kwenye masuala nyeti anayoletewa na anapaswa kufanya analysis kubwa na kufanya maamuzi mazito atafanya maamuzi gani?

Yanayosemwa huko Serikalini yanatisha. Ngoja tukae kimya kuwalinda wenzetu walioko huko.
 
Yalianza kama masikhara ila sasa tuvumilie kuvuna matunda yake.

Kuanguka kwa Tanzania ni suala lililochukua muda kidogo. Tuliopata nafasi ya kuonya, tulionya ili kulikomboa Taifa ila hakuna yaliyofanyika na matokeo yake ndo haya tunayoyaona leo.

Ilianza kwa kuanza kutoa nafasi za utendaji Serikalini za Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kwa Makada wa Chama cha Mapinduzi.

Tuliopewa macho ya rohoni tulionya kuwa suala hili lilikuwa linaenda kuharibu sehemu nyeti ya Utumishi nchini kwa sababu watu hawa ni watu wanaopaswa kupatikana kwa merit kutokana na kuwa sehemu muhimu ya maamuzi nchini hivyo ni vizuri masuala ya competence, integrity na experience kuzingatiwa kwenye teuzi zao ila kwa kuwa CCM waliamua kupuuza maoni ya wenye akili walitupuuza kwa maslahi yao ya muda mfupi.

Haikuishia hapo. Siasa ikaingia hadi kwenye majeshi na vyombo vya Ulinzi. Kubadilishwa kwa Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa zaidi ya mara 4 ndani ya miaka 3 ni kielelezo kingine kuwa Siasa ilianza kuingia huko.

Kupandishwa vyeo kwa maofisa wa Polisi wanaoonekana kuzungumza mbele ya vyombo vya habari masuala yanayowafurahisha wanasiasa nako kuliendelea kuonesha kwa namna gani siasa imeingia kwenye vyombo vyetu hivi.

Matokeo ya haya:
1. Sasa Tanzania imepoteza nafasi yake ya kuwa Think Tank na Main determinant wa Siasa za Maziwa Makuu. Nafasi hii wamechukua Rwanda na Uganda baada ya kufanikiwa kupenyeza mamluki wengi kwenye mfumo wa Tanzania. Sasa Rasmi Rwanda anaenda kuichukua Mashariki ya Congo.

2. Mfumo wa Maamuzi wa Tanzania umeshakuwa fully penetrated na Majasusi wa Bahima Empire. Inasemwa sehemu nyeti zote zimeshakuwa Penetrated. Hadi sasa Naibu PM wa TZ ni product wa Bahima Empire. Na onasemwa BOT, Hazina, Mipango kote wamejaa wao.

3. JWTZ kuanza kuwa Jeshi la Kisiasa na kupoteza nafasi yake kama Jeshi Bora na linaloheshimika Afrika Mashariki. Jeshi hili saivi limekuwa Jeshi la Maonesho, kupenda sifa badala ya Jeshi la Mikakati na Mipango Kabambe. Kichapo walichokipata huko Congo hadi saivi Malawi wameamua kuondoka ni kielelezo tosha.

4. Kukwama kwa mipango kabambe ya maendeleo ya Taifa. Hii ni kwa sababu nafasi za DED, KM na RAS zimeshikwa na makada wa Chama cha Mapinduzi ambao wao kazi yao ni kuangalia uhai wa Chama cha Mapinduzi ila sio mustakabali mzuri wa Taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Watu hawa hawawezi kufanya analysis ya masuala ya msingi zaidi ya kuangalia siasa na Chama chao ambacho wanaamini bila hicho wasingekuwepo hapo.

Kwenye haya maamuzi mengi sasa yamekuwa yakifanywa kwa mtazamo wa kisiasa na sio kwa ajili ya kuijenga Tanzania imara Kiuchumi na Kimaisha kwa miaka mingi ijayo.

5. Kuibuka kwa watu ambao kazi yao ni kuwalamba miguu Viongozi na Kuwasifia huku wakilipwa fedha ambazo ni kodi za wananchi. Watu hawa wanaharibu vijana kwa kuwaonesha kuwa maisha ni kuwa Chawa na inawezekana usijishughulishe na kufanya kazi kwa bidii ila ukawa chawa wa kiongozi na maisha yakaenda.

6. Kuendelea kushuka kwa kiwango kikubwa na cha kutisha masuala ya Utawala Bora na Utawala wa Sheria. Hili linapelekea wananchi wenye mawazo tofauti kutekwa, kuuwawa na wengine kupotezwa bila hatua zozote kuchukuliwa.

Matukio ya Soka, Ben Saanane, Mzee Kibao na Sativa ni mfano mdogo tu wa wapi tumefika kama Taifa.

Poleni sana Watanzania.

Kilaaniwe CHAMA CHA MAPINDUZI.

Tupambane kufa na kupona tupate KATIBA MPYA.
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), a.k.a chawa tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

Tumefika hapa tulipo kwasababu ya kuongozwa kwa tabia ya unyumbu, (unyumbu wa kisiasa)

Tunaishi kwenye jamii ya kanyaga twende yaani jamii ya bora liende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi pia unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe
 
Back
Top Bottom