Tulioacha wake zetu kwa sababu ya usaliti waliotufanyia tukutane hapa

Pole sanaa mwamba.... Hapa kale ka kauli ka kataa Ndoa naona kanafanya kazi
 
Sema hao wanyarwanda kama tabia zao kama wabaya tu [emoji16][emoji16]
 
Wanawake wengi kabla ya kuolewa wanakuwa na shauku ya kuitaka ndoa na kuomba kwa machozi, wakiingia kwenye ndoa wanajisahau wanachukulia poa, wakiachwa wanaanza kulia tena warudi kwenye ndoa.
Wanatushinikiza sana tuwaoe tukiwa nao kwenye mahusiano wakishapata cheti cha ndoa wanaanza kuibomoa

Wakiibomoa wakaachika wanarudi tena nyumba za ibada kuomba warudiane au kuolewa tena
 
Mkuu alikuonea sana. Mimi nikisalitiwa nitaona ni sawa tu maama niko bize na misafara ya Tundu Lissu tunachanja mikoa hadi mikoa mke wangu napiga Gori moja tu nasepa kwenye Harakati za kukomboa Nchi.

Wewe mwenzangu unapiga mabao matatu na gari kali juu na bado unasalitiwa tena mtu anabeba Mimba kabisa akiamini atakudanganya huku akimtia moyo aliyempa Mimba kwamba hutajua.

Kwakweli dunia haiko fair kabisa.
 
Stori ya Jamaa imenigusa sana.

Mimi mwenyewe nahisi mtoto mmoja sio wangu.

Maama ni mweupe japo kwao wana ka rangi kidogo ila wa kwangu anawazidi wao. Sasa Hybridi ya mtu mweusi na Maji ya kunde inawezekana vipi kuzaa mweupe??

Nimesubiri mieze isogee ili nione rangi kama itakuja kukaribiana na yangu lakini naona dogo anazidi kuwa mweupe.

Kwakweli katika harakati za maisha sisi wanaume tunakutana na mengi.

Mbowe alifungwa mimi nimeambulia kupigiwa mke.
 
Bro unauma sana
 
Pole Sana mkuu, haya mambo wanaume tunapitia.
Wengine mpk watoto wakaandikwa kwenye magazeti wana baba watano.
Ukiuliza unapelekwa mahabusu.
Leo hii kiko wapi?
Mwanamke hana senti kumi ananiita mpaka Baba nimsaidie🤣🤣🤣.
Huyu Mwanamke alichoma vyeti vyangu vyote vya shule, chuo
Nyumba nikahama nikaacha kila kitu.
Polisi mara tatu nimelala huko kwa ajili yake.
Yaani mtu unatoka kino mpk nikahamia mtoni kwa aziz ally kumkimbia.
Mama yangu kwa uchungu miaka ile ni mjeshi alitaka tuende tukamfanyizie.
Tunajipanga Mwanamke huyu hapa.
Kanifata home shetani yule.
Maza kumuona kalainika Msamehe muelewane.
E bana nimesamehe kurudi kwangu kaleta tena Polisi.
Ruka ukuta nikatimua
Ndo kuenda kwa aziz ally kuanza life upya.
Badae kumbe alikua anachepuka na kinyozi bishoo mmoja hivi Sinza.
Nilimfata yule kinyozi ,
Kwanza nyoa nywele.
Badae we si flani?
Ndio. nifuate.
Anatetemeka,Bahati nzuri tulimalizana fresh nikamwambia huyu mkeo kuanzia sasa nakuachia.
Ndio yakaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…