mr pipa
JF-Expert Member
- Jul 26, 2021
- 3,074
- 6,472
Miaka kumi nyuma nimemaliza zangu shule naingia mtaani sina ramani ya kipi kifanyike nitoboe kimaisha
Nikaanza harakati za hapa na pale kuchimba vyoo nipo, ukuli nipo, nk piga kazi kwa nguvu zote kila mchongo ukitokea nipo
Lakini kila nikitazama malengo na kazi ninazofanya imani ya kutoboa inagoma
Nikaamua kwenda machimbo ya dhahabu asee kule nikakutana na miamba yenye bahati zao yaani yeye lengo lake kushika milion mia tano ile akipata milioni kumi ni kula bata siku tatu imekata anarudi tena job
Nikamwambia Mungu nisaidie na mimi nipate japo m5 tu nikaanzishe japo ka biashara
Basi nikaanza kupambana sana miezi 8 ikakata nakuja ambulia laki 5 hapo familia inaitaji pesa ikabidi nigawe laki 3 niwatumie
Hapo sina nguo na mademu sikuwagusa kitambo niko na haam hatari miezi nane kwa mwanaume acha tu!
Nikajikuta pesa imekata nikaanza upya nakumbuka nimesota chimbo kalibu miaka miwili
Nikawaza umri nao unaenda nikisema ni base kwenye jambo moja nitafeli nakumbuka nilikuwa na shilingi milioni moja
Nikarudi kitaa kuja kulima msimu umefika nikapata Junia za mahindi kama 30
Enzi zile ndio anajitokeza yule tajiri wa mkako basi nikapeleka kuuza kilichofuata hakuna mtanzania asiye jua yule mwamba alitufanya nini wakulima
Ikanipasa kuanza upya naingia wapi sielewi nikajikuta napanda gari naelekea mkoa x nimefika ule mkoa baada ya wiki kama tatu nikapata kazi ya kufyatua matofali ya block nikapiga
Hadi msimu unakata nikajikuta nina laki 8 nikarudi kufanya biashara ya mbao nimepambana, nikajikuta nimejenga kanyumba kakimtindo nikanunua na kapikipiki nikasema asante Mungu
Nikakopa bank kama milioni 8 hivi ili kubusti mtaji kujazia mtaji kwenye mbao ile pesa ndani ya miezi 6 ikakua mpaka ikafikia milion 30
Nikasema kwa kuwa nimekuwa ngoja nitafute soko la nje ya mkoa
Nikapatana na mfanyabiashara mwenzangu tukapata mteja Dar es Salaam
Asee ile siku sitoisahau picha linaanza tumewasili dar majira ya saa moja jioni tukiwa na mzigo wa mbao kama gari Scania mbili hivi
Tukazishusha nikapewa shilingi milioni 1 kwa ajili ya hapa na pale asubuhi tuje tupige hesabu tulipane
Ile nakuja asubuhi kwenye lile eneo hakuna kitu yaani tulipo shusha zile mbao ni peupe hata ubao hakuna
Pigia simu kwa wale jamaa hawapatikani kumbe dili lilishasukwa kitambo na yule jamaa ambaye nilifanya nae biashara mwanzo
Aisee nakumbuka natoka pale napanda gari hadi nafika home sijielewi na sielewi nini nifanye nikawa nusu mtu nusu chizi
Na vile sikumwambia mtu yoyote kilichonitokea baada ya muda watu wakahisi nimekosea masharti ya mganga
Miezi 7 imepita bank wakaja tangaza kuuza nyumba maana nilikopa tena kama m20
Hapo kila mtu kanitenga wakijua nimefilisika sababu ya hela za manyoka
Nikawaza kujiua roho ikaniambia hapana jiue kwa faida hapo ndipo nikaanza kuingia kwenye michongo hatari ........ Mwendelezo nauweka hapo kwenye comment mana ni dili haramu haramu so asanten