Tunaendelea.................πππ
Nikawaza kujiua ila nafsi ukasema nijiue kwa faida
Kumbuka benk wameuza nyumba cha juu kikabaki kama milion 3 hivi
Nikawatafutia wananngu na wife nyumba ya kupanga nikalipia miez 9 milioni moja nikampa wife apambane
mfukoni nikabaki na m1 huwa mambo yakiwa magumu huwa naamini kwenda kwenye mkoa au sehem wasipo nifaham
Baada ya kuiweka sawa familia ni huyo nikakwea roli hadi mkoa x nikalipia gest siku ya pili nikatafuta wenyeji uzuri wa mi ni mcheshi nikazama vilabu vya pombe za machicha aka komon
Nikawaagizia watu pombe uzuri hazina bei basi nikaanza tafuta data za huo mkoa kwa watu nikapata siku ya tatu wakanitafuta chumba nikalipa
Nikanunua jamvi na shuka nikatandika chini tayari kwa maisha mapya
Zangu jion ilikuwa kwenda vilabu vya pombe japo umri haukuendana na hizo mambo ila nilisha jizila lengo na nia ni maisha
Na yote ili kupata data wapi nianzie
Nimekaa kama wiki nikapata kazi ya kubebelea kifusi kwenetololi kujaza kwenye msingi wa nyumba kuna miamba ilini unganisha niwale wa vilabu
nikapiga kama siku tano nikajipatia laki tatu
nikanunua jiko na mazaga ya ndani kama ya mwezi hivi
Sijakaa sawa nikapata dili la kupasua mawe kwaajili ya kujengea msingi nikapiga
Kuna siku narud toka job nakutana na mama mmoja hivi alikuwa amepata ajali ya gari yaani alikosa njia akaingia mtaroni kilikuwa kifuku
haikuwa ajari kubwa ila kwa wamama ni kubwa nikawa nimeitoa wana tukamsaidia kutoa gari mtalon
And the day yule mama tulizoeana sana na anatokea nikubali siku moja nilipo mpa story yangu akanionea huruma ndipo alipo nipa mchongo wa pesa haramu dili la pesa bandia
Kwa vile sikuwa na chaguo nikazama
Akanipa masharti na kunionesha kazi inavyofanyika so ulinivutia sana nikasema kuliko kuua watu ngoja nipambane na serikali nikifa ndio kifo ambacho nimekichagua cha faida
Akaniahid kunipa m3 za mtaji na sio kwamba anafanya yeye hapana ila yeye ana watu huko na mbele na wapo kikazi yaan ipo hivi ukiwa njiani a m7 ukiipeleka wale miamba wanakutolea m21 ile saba og yakwao
Asee nikajikuta ndani ya mwezi nina milioni 45 mana ni mwendo wa kuiweka kwa wakala au bank kisha. Kutoa kurudi tena kwa mainjinia
So nikajikuta
Nikaingia kulima bangeeee na heka 8 uzuri connection ikiwepo tena ya matajiri wakubwa nikavuna nikapata kama m150
Sikuishia hapo na hakuna mchongo nilio utosa ni mwendo wa bulu bulu
Kuja piga hesabu miaka miwili nikawa na m345 nikasema ningejiua ingekuwaje
Katika hayo mambo sio kwamba sikukutana na sheria nimefungwa sana mpaka polisi wanaamua wakugeuze kitega uchumi so unachopaswa kujua ogopa
Sana mtu ambaye amejikatia tamaa ya kuishi au mtu ambaye kajiambia liwalo na liwe huyo ni sikio la kufa labda mumuue
nakumbuka nilifanya hizi misheni
Miaka mitano then nikahamia rasmi kwenye uuzaji wa mbao na ualimu wa shule za msingi
saivi napiga kelele na watoto wa shule ndoto zangu zimetimia nimetulia so kifikra nina maadili makubwa kibao kimwili nimeacha yote
Kwa sasa sioni la maana hapa duniani coz vyote nimefanya siwezi ijua kesho yangu ila nimejifunza mengi kupitia haya maisha
usikate tamaa
Haijalishi huna gar mtoto wala nyumba
Pamba ukiona hapa panizingua hamia pangine kulala njaa sio ishu ishu je inatimiza vipi ndoto zako nimemaliza
Nb sihamasishi uvunjwaji wa sheria hiyo ni story yangu tu
Karibu njombe tupigwe baridi ni mimi mwalimu mr pipaββββ