Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Kulikuwa na DOS (Disk Operating System) ili kompyuta iwake unaweka floppy disk. Mwaka 1987.
 
picha tulikuwa tunascan hard copy kiongozi
 
Wazee wa BASIC programming language waje hapa.
Mambo ya REM, MOV, GO TO, ...
Na wa Pascal Programming language hawaja sahaulika, FORTRAN pia wamekumbukwa.
 
Mitaa hiyo ushanichanganya, huku kama Tv tu zimeanza kua common miaka ya 90s mwishoni,sijui computers wangapi walikua wameziona,sio tu kutumia..
Ndo maana nikasema nimeanza kutumia kompyuta kabla ya 99% ya wanaJF wote.

Enzi hizo hata UDSM sidhani kama kulikuwa na kompyuta hata 2…..

Home computers za Amstrad ndo kompyuta za kwanza mimi kuanza kuzitumia shuleni kwenye assignments na nyumbani kucheza games.

Amstrad ilikuwa ni kampuni ya Uingereza iliyokuwa inatengeneza vifaa vya umeme vya nyumbani/ majumbani.
 
Yawezekana baadhi wametumia hizo kompyuta za zamani kwakua location uliyopo ilisapoti kutumia hizo kompyuta.

So siyo kila atayesema katumia DOS mkajua ni kikongwe. Ni vile tech ilichelewa kumfikia
 
Kweli ilikua hustle,poleni wakongwe,kuna documentary inaitwa The triumph of the nerds,story ya Bill Gates, Steve Job,na Co founders wa Apple, computer zilikua tofauti Sana,kuanzia Hardware hard softwares
picha tulikuwa tunascan hard copy kiongozi
 
Duh mzee Umetumia Amstrad πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… wewe Ni wakishua sana maana Hiyo kitu ilikuwepo Tangu miaka ya 80 sema Ilipunguzwa Na ikaanza kupotea Miaka ya 90 mwishoni..

Mi Nimetumia IBM Baadae nikaanza kutumia Gate way
 
Hata zingekuepo Kuna "computer operator" enzi hizo??

Kuna Rafiki yangu Mama yake alikua anafanya kazi UDSM,bi mkubwa aliniambia miaka hiyo mkiingia Computer room lazima kuvua viatu,na ole wenu mpige kelele,mnatolewa...
 
Yawezekana baadhi wametumia hizo kompyuta za zamani kwakua location uliyopo ilisapoti kutumia hizo kompyuta.

So siyo kila atayesema katumia DOS mkajua ni kikongwe. Ni vile tech ilichelewa kumfikia
Free DOS CD inatolewa bure hadi kesho kila ukinunua computer mpya hasa yenye Intel processor.
Siyo used computer.
 
Duh mzee Umetumia Amstrad πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… wewe Ni wakishua sana maana Hiyo kitu ilikuwepo Tangu miaka ya 80 sema Ilipunguzwa Na ikaanza kupotea Miaka ya 90 mwishoni
Hapana, wala siyo wa kishua.

Ni vile tu ukiwa mtoto mara nyingi unaambatana na wazazi wako kule ambako pilikapilika za maisha zitakowapeleka.

Utayokutana nayo huko yatategemea na wewe jinsi ulivyo.

Mimi kwa asili ni mtu mdadisi sana. Pia niko observant sana. Halafu nina kumbukumbu nzuri.

Kwa sababu Amstrad ndo ilikuwa brand ya kwanza ya kompyuta ambayo nilikutana nayo, ndo maana mpaka leo bado naikumbuka licha ya kampuni iliyokuwa ikizitengeneza kufa.
 
Hata zingekuepo Kuna "computer operator" enzi hizo??

Kuna Rafiki yangu Mama yake alikua anafanya kazi UDSM,bi mkubwa aliniambia miaka hiyo mkiingia Computer room lazima kuvua viatu,na ole wenu mpige kelele,mnatolewa...
Wakati nasoma high school kulikuwa na Comp Lab ya msaada.
Ulikuwa huingii na viatu wala kitu chochote utaleta vumbi utaua computer.
Au viatu vitaleta vumbi lenye virus kumbe computer virus ni software tu ..🀣🀣🀣🀣
 
Hata zingekuepo Kuna "computer operator" enzi hizo??

Kuna Rafiki yangu Mama yake alikua anafanya kazi UDSM,bi mkubwa aliniambia miaka hiyo mkiingia Computer room lazima kuvua viatu,na ole wenu mpige kelele,mnatolewa...
Nakumbuka miaka ya kati ya 90, UDSM kulikuwa na computer lab moja tu.

Ilikuwa pale karibu na kituo cha basi mkabala na tawi la benki la NBC.

Hayo masharti ya kuingia humo yalikuwepo kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…