Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Bwana bwana miaka ya 2018-2020 kuna goli(duka) la magodoro nilikuwa nauza maeneo ya kinyerezi location ya duka haikuwa mbaya ilikuwa nzuri sana opo road kabisa na wanunuaji wengi walikuwa kipato cha kati.

Sasa bwana ilikuwa akija mteja ni lazima apigwe udalali kama bei ya kuuza ni tsh 200,000 basi godoro ningeliuza tsh 230,000.Ilikuwa godoro halitoki bila mimi kupata hata tsh 15,000 minimum

Nakumbuka kuna mzee mmoja mshabiki wa liverpool alikuja akanikuta nimelala akaniuliza "godoro 5 kwa 6 inchi 8 bei gani" mimi kwa wenge la usingizi nikaropoka tu "laki nne" wakati godoro bei yake ni tsh 210,000 yale ya kitambaa tunaita kashata.

Yule mzee bwana akaingia kwenye kiraumu chake akivuta kibunda cha milioni akanichomolea laki nne akaniuliza "na usafri vipi hakuna kirikuu??" nikamwambia "bodaboda mbona inabeba nalifunga freshi utanipa tsh 20,000 ya usafiri"...mzee akalipia usafiri akanielekeza kwake nikaita boda nikampa tsh 2000(hiyo sehemu gharama yake ni buku) kwahiyo nikawa nimepiga mshindo wa tsh 208,000.

Nilijifunza kitu kuna watu wana hela kiasi kwamba hata ukiwapiga ni sawa na unajiibia mwenyewe imagine hiko kilikuwa kipindi cha anko MAGU.

Jana nilikuwa maaneo ya BL park nachek game ya aseno nikamuona yule mzee niliyemdalalia tsh 200k bado anadunda tu wakati mimi bado najitafuta hahahaha.

Najua mpo wenzangu wengi ambao mmepiga sana mishindo ya udalali na bado life ni vita karibuni.
Ujafa na ukimwi

Madalali weñgi wamekufa sana na vih
 
Piga kwa sababu hata wewe kuna mahali unapigwa hivyo hivyo.

Kuna dawa juzi nimeenda kuchukua inauzwa tsh 1,000 ila yule dada mfamasia akasema 12K, nikacheka nikamwambia dada mi mwenyewe mfamasia tena mfamasiala haswa nipe bei nilipie nichukue changu, kwa aibu sana akaniuliza unahitaji ngapi, nikatoa 10K nikamwambia kata 3 nipe chenchi. Akarudisha 7,000 yangu nikasepa. Ningekua sijui bei ningepigwa.

Huu ni wizi huyo muuzaji alikuwa anataka kukuibia wala sio udalali huo

Mkuu ulichokuwa unafanya ni wizi wala sio udalali.
Udalali ni hali inahusisha mtu wa kati kupata kitu .
So bei ya bidhaa inajulikana na bei ya udalali inajulikana .
So mteja anamlipa mwenye mali fedha yake na dalali anapewa commision yake.
Yaani unakabidhiwa duka uuze bidhaa wewe unapandisha bei unasema udalali? Wewe ulikuwa unafanya wizi wala sio udalali
 
Huu ni wizi

Mkuu ulichokuwa unafanya ni wizi wala sio udalali.
Udalali ni hali inahusisha mtu wa kati kupata kitu .
So bei ya bidhaa inajulikana na bei ya udalali inajulikana .
So mteja anamlipa mwenye mali fedha yake na dalali anapewa commision yake
Hapana wezi ni wakina mwigulu na samia
 
Piga kwa sababu hata wewe kuna mahali unapigwa hivyo hivyo.

Kuna dawa juzi nimeenda kuchukua inauzwa tsh 1,000 ila yule dada mfamasia akasema 12K, nikacheka nikamwambia dada mi mwenyewe mfamasia tena mfamasiala haswa nipe bei nilipie nichukue changu, kwa aibu sana akaniuliza unahitaji ngapi, nikatoa 10K nikamwambia kata 3 nipe chenchi. Akarudisha 7,000 yangu nikasepa. Ningekua sijui bei ningepigwa.
Hapa watu watajifanya walokole ila wezi kuliko uwizi wenyewe.
 
Kaka me nilitaja tu bei kwa wenge la usingizi na yeye wala hakuomba punguzo .....sasa ningefanyaje ningekataa pesa?

Sasa una piga 200k unataka ikufikishe wapi bruh 😄

Huyo alikuwa anafanya wizi , kwa maelezo yake alipewa duka la magodoro auze, magodoro yanabei elekezi , aliyemkabidhi duka la magodoro alikuwa anamlipa mshahara .
Yeye anataja bei ya juu kulipo bei elekezi .
Huo ni wizi wala sio udalali
 
Huu udalali wake mwenyewe nilikuwa nashangaa ni wa namna gani 😄
 
Back
Top Bottom