Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Suala la wizi hapa kwetu linakatisha tamaa. Watu si waaminifu na biashara zinakufa hivyo. Mauzo hayapatikani kwa sababu aliyewekwa anapandisha bei
 
Mara nyingi pesa zisizo za jasho Huwa haziwezi kukuimarisha kiuchumi.

Utaishia kulewa, kuvaa Nguo, kula kwa anasa na kushughulikia wanawake.

Hii inatokana na fikra kuwa hata kesho utapata pesa Tena, kumbe sivyo!
akili ya mtu, wengine hujiwekeza pesa hizo kwa uwoga wa maisha ya kesho wengine huzitumbua kwa kuamini kesho watapata tena
 
Hebu angalia yaani wanampangia maisha mtu mwenye mali yake

Kuna siku cousin yangu aliita usaili wa madereva garage
Madereva wakajitokeza, wakiwa wanasubiri kuitwa wakawa wanaongea zao
Hapo alikuwa amekaa mtoto wa boss akiwasikiliza na kucheka kwa story zao
Basi akaja dereva mtarajiwa akakaa nae basi kwa ukiherehere akawauliza waliomtangulia akasema jamani kuna upigaji lakini hapa au ni ka mshahara tu?
Yule dogo mtoto wa boss akaenda kumtonya anaefanya interview
Duh 😁😁😁
 
Sio powa kaka....watu wanaropoka tu.
Ukifata maandiko unalaza familia njaa kabisa lazima ule kwa haki, lakini ukiona unaminywa sana lazima upigane ugawane kidogo na mwenzako.....japo wanasema faida iwe robo tatu ya mtaji.

Mfano uza product 10,000 na ulinunua 7,500.....2,500 ni faida yako ✅✅✅✅

Ukija kwenye udalali basi ale 1,000 mpaka 2,000 means product isiuzwe zaidi ya 12,000 isizidi hapo.

Sio kuuza 18,000 sijui 25000 product ya 10,000 hii ni dhambi wandugu,

sikatai mimi nimewahi fanya udalali lakini nilizingatia hizi standards.....
 
Bwana bwana miaka ya 2018-2020 kuna goli(duka) la magodoro nilikuwa nauza maeneo ya kinyerezi location ya duka haikuwa mbaya ilikuwa nzuri sana opo road kabisa na wanunuaji wengi walikuwa kipato cha kati.

Sasa bwana ilikuwa akija mteja ni lazima apigwe udalali kama bei ya kuuza ni tsh 200,000 basi godoro ningeliuza tsh 230,000.Ilikuwa godoro halitoki bila mimi kupata hata tsh 15,000 minimum

Nakumbuka kuna mzee mmoja mshabiki wa liverpool alikuja akanikuta nimelala akaniuliza "godoro 5 kwa 6 inchi 8 bei gani" mimi kwa wenge la usingizi nikaropoka tu "laki nne" wakati godoro bei yake ni tsh 210,000 yale ya kitambaa tunaita kashata.

Yule mzee bwana akaingia kwenye kiraumu chake akivuta kibunda cha milioni akanichomolea laki nne akaniuliza "na usafri vipi hakuna kirikuu??" nikamwambia "bodaboda mbona inabeba nalifunga freshi utanipa tsh 20,000 ya usafiri"...mzee akalipia usafiri akanielekeza kwake nikaita boda nikampa tsh 2000(hiyo sehemu gharama yake ni buku) kwahiyo nikawa nimepiga mshindo wa tsh 208,000.

Nilijifunza kitu kuna watu wana hela kiasi kwamba hata ukiwapiga ni sawa na unajiibia mwenyewe imagine hiko kilikuwa kipindi cha anko MAGU.

Jana nilikuwa maaneo ya BL park nachek game ya aseno nikamuona yule mzee niliyemdalalia tsh 200k bado anadunda tu wakati mimi bado najitafuta hahahaha.

Najua mpo wenzangu wengi ambao mmepiga sana mishindo ya udalali(Genji) na bado life ni vita karibuni.
Hauwezi kuendelea kwa fedha za dhuluma ,udalali ni udhulumati tu.
 
Back
Top Bottom