Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Mtu mweusi akipata kazi anawaza anaiba vipi. Kuna Transporter ana chinese trucks saizi kaanza kufunga mfumo wa gesi sasa madereva wazoefu walikuwa wanapata pesa kwa kupiga Diesel. Mtu akiambiwa week hii peleka gari workshop ikafungwe gesi anaacha kazi hawataki gesi
Hebu angalia yaani wanampangia maisha mtu mwenye mali yake

Kuna siku cousin yangu aliita usaili wa madereva garage
Madereva wakajitokeza, wakiwa wanasubiri kuitwa wakawa wanaongea zao
Hapo alikuwa amekaa mtoto wa boss akiwasikiliza na kucheka kwa story zao
Basi akaja dereva mtarajiwa akakaa nae basi kwa ukiherehere akawauliza waliomtangulia akasema jamani kuna upigaji lakini hapa au ni ka mshahara tu?
Yule dogo mtoto wa boss akaenda kumtonya anaefanya interview
 
Kuna mhindi mmoja ana Coaster zake za daladala, siku gari imeharibika dereva analalamika anamuambia Boss tunapambana sana wewe hutujali nikiacha kazi hapa hii gari itapaki na kuozea nje.

Mhindi akamwambia najua nyie mnavyoniibia akamtaja jamaa hasa wewe mpaka route unachepusha na hesabu unaleta ileile, na ukiacha hapa kazi hautopata Boss wa kumuibia na akakuvumilia kama mimi
Kama Boss muhindi acha anyooshwe ila ninavyojua ukiona mfanya kazi anakusifia kama boss inabidi ujitafakari sana.
 
Huo ni utapeli wala sio udalali, nishafanya kazi sana na madalali,
Nina appartments napangisha madalali nawaambia kabisa bei wakiniletea mteja nawalipa kiasi flani na pia wanautaratibu wao mteja akilipa anawalipa fedha ya udalali kodi ya mwezi 1.
Aidha nilishawapaga madalali kazi ya kuniuzia gari nikawatajia bei wakaitangaza bei ya juu kulipo ile niliyowatajia kimbembe kikaja kwenye malipo mteja anataka kuingiza fedha kwenye akaunti , nikamkubalia nikampa akaunti nikamtajia bei akabaki anashangaa mbona bei niliyoambiwa ni kubwa kuliko unayoniambia, nikamwambia bei yangu ndio hiyo na ndio nataka uweke kwenye akaunti yangu.
Mind wale madalali nilishakubaliana nao wakiniletea mteja wa bei hiyo nawapa kiasi flani.
Wale madalali walimind sana nikawajibu sinaga dili za wizi kama vipi ondokeni na mteja wenu .
Mteja akadhira akaondoka baadae akanitafuta kivyake tukafanya biashara wale madalali hawakupata kitu kutokana na tamaa zao manake mteja mwenyewe aliinunua gari akaipeleka mkoani hata hawakujua kama nilimuuzia yeye.
Madalali sometimes hovyo wanapandisha bei ya vitu wanasababisha visiuzike kwa mapema
Safi sana watu wote wakiwa kama wewe hawa madalali majambazi watanyooka.
 
Yaani umelenga humohumo.
Na kama unataka kupanga nyumba, jua wanakuja madalali kama 6 hv.
Hiyo madalali kuwa wengi unakuta dalali wako wa kwanza hana nyumba so chain inaanza kila anayepigiwa kama hana nyumba anampigia mwenzie ndio unakuta wanafika mpka sita....mdalali me nawapaga nusu ya hela ninyolipa kodi nikivurugwa mpaka robo.
 
Mzee wangu kila mtu ana-past zake hizo ndio past zangu tena wala sio mbaya kivile ni vile wabongo wa JF ni malaika wanaishi mbinguni.
Kuna majizi humu mpaka wa silaha, ila akichangia utafikiri ustadh
Kweli wengi wanajipamba tu na kupinga na katu hawasemi ukweli
Kama wote tungekuwa wema humu kama wanavyojiweka watu basi tusingesikia mauwaji wala ujambazi wala umalaya maana tungekuwa tuko na maisha kama Ulaya vile
 
Hiyo madalali kuwa wengi unakuta dalali wako wa kwanza hana nyumba so chain inaanza kila anayepigiwa kama hana nyumba anampigia mwenzie ndio unakuta wanafika mpka sita....mdalali me nawapaga nusu ya hela ninyolipa kodi nikivurugwa mpaka robo.
Hela robo🥺🥺
We jamani, utaua watu na familia zao ujue
 
Sometimes madalali (mawinga) Ni muhimu sn ili ufanye biashara,hasa kwa majiji na maeneo mengn yenye mzunguko na ushindan mkubwa sn WA biashara Kama dar n.k

Unapowakwepa madalali, uwezi Kuuza na utasingizia sn unarogwa Ila hamna Hata uchawi.

Ni hivi
Mtu anapokuletea mteja sio kwamba hakuyaona maduka mengine, Bali anajua Kuna namna flani anafaidika na Wewe kuliko akimpeleka mteja kwingine.

Nna biashara ya hardware na electronics. Ila udalali wangu naufanya Sana na mafundi (mafundi electronics,umeme na maji na ujenzi)

Kwenye biashara zangu Huwa nna Bei mbili, Bei ya mteja na Bei ya fundi Kwa Kila bidhaa inayouzwa.

Mafundi nawauzia Kwa Kila bidhaa Kwa Bei ya JUMLA Hata kama wakinunua kwa reja reja.

Hii hunisaidia kupata wateja wengi maana fundi akileta order labda ya laki 5 Hadi mil 1 hakosi total elfu 50 Hadi laki kutoka kwny punguzo analopata Kwa kila bidhaa mteja aliyonunua.

Binafsi inanisaidia Sana,
maana Hata nikichelewa kufungua, mteja kwangu haruki,ntapigiwa sim na fundi nije chap kumhudumia, maana kwingine fundi akimpeleka mteja anaondoka mikono mitupu.

Anabaki kusubiria Ela yake ya ufundi kwny Kazi itakayofanyika.

Fundi Yuko radhi cement itoke k'koo mpk chanika ili mradi TU anauhakika Kila mfuko ukiuza,kwake anaingiza 500 yake.

Boss ukihoji Kwann cement itokee k'koo na Bei ni Ile ile, utaambiwa maduka ya mbagala na chanika wanauza cement feki , iliyoexpai au haitimii kg 50.

Sasa kama boss wee,
Either ufuate ushauri wa fundi wako ujenge kitu imara fundi wako aishi au uokoe gharama fundi wako alale njaa.
 
Back
Top Bottom