Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Tuliopiga sana pesa za udalali kwenye biashara na bado life gumu tukutane hapa

Sio matapeli, ila wana tabia zao wenyewe wanazijua.
Najua madalali tabia yao mbovu ni over priced ya nyumba au frem unakuta mwenye nyumba anapangisha nyumba laki tatu ila dalali anamchekecha mtu laki nne ili apate pesa nyingi ya mwenz mmoja bila kujali anavyomuumiza mwenzie kwa kipindi atakachookaa hapo.
 
Wanakuja waizi wenzio
Mimi bwana nina biashara 3 nauza vitu jumla.
Sasa kwenye duka moja alikujaga jamaa mmoja akawa kama chawa.
Nisijue wafanyakazi wakamkaribisha.

Sasa siku nakuja kujua nilimfukuza siku hiyohiyoo.

Alinilaani kishenzi kupitia wafanyakazi wangu "Alikuwa akiwapa ujumbe wanifikishie"
Ila mi naona naendelea na yeye yupo tu barabarani, nadhani ile laana ilimrudia mwenyewe.

Kwenye biashara zangu chawa na madalali SITAKI.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kuna mhindi mmoja ana Coaster zake za daladala, siku gari imeharibika dereva analalamika anamuambia Boss tunapambana sana wewe hutujali nikiacha kazi hapa hii gari itapaki na kuozea nje.

Mhindi akamwambia najua nyie mnavyoniibia akamtaja jamaa hasa wewe mpaka route unachepusha na hesabu unaleta ileile, na ukiacha hapa kazi hautopata Boss wa kumuibia na akakuvumilia kama mimi
 
Bwana bwana miaka ya 2018-2020 kuna goli(duka) la magodoro nilikuwa nauza maeneo ya kinyerezi location ya duka haikuwa mbaya ilikuwa nzuri sana opo road kabisa na wanunuaji wengi walikuwa kipato cha kati.

Sasa bwana ilikuwa akija mteja ni lazima apigwe udalali kama bei ya kuuza ni tsh 200,000 basi godoro ningeliuza tsh 230,000.Ilikuwa godoro halitoki bila mimi kupata hata tsh 15,000 minimum

Nakumbuka kuna mzee mmoja mshabiki wa liverpool alikuja akanikuta nimelala akaniuliza "godoro 5 kwa 6 inchi 8 bei gani" mimi kwa wenge la usingizi nikaropoka tu "laki nne" wakati godoro bei yake ni tsh 210,000 yale ya kitambaa tunaita kashata.

Yule mzee bwana akaingia kwenye kiraumu chake akivuta kibunda cha milioni akanichomolea laki nne akaniuliza "na usafri vipi hakuna kirikuu??" nikamwambia "bodaboda mbona inabeba nalifunga freshi utanipa tsh 20,000 ya usafiri"...mzee akalipia usafiri akanielekeza kwake nikaita boda nikampa tsh 2000(hiyo sehemu gharama yake ni buku) kwahiyo nikawa nimepiga mshindo wa tsh 208,000.

Nilijifunza kitu kuna watu wana hela kiasi kwamba hata ukiwapiga ni sawa na unajiibia mwenyewe imagine hiko kilikuwa kipindi cha anko MAGU.

Jana nilikuwa maaneo ya BL park nachek game ya aseno nikamuona yule mzee niliyemdalalia tsh 200k bado anadunda tu wakati mimi bado najitafuta hahahaha.

Najua mpo wenzangu wengi ambao mmepiga sana mishindo ya udalali(Genji) na bado life ni vita karibuni.
Easy money easy Go
 
Kuna mhindi mmoja ana Coaster zake za daladala, siku gari imeharibika dereva analalamika anamuambia Boss tunapambana sana wewe hutujali nikiacha kazi hapa hii gari itapaki na kuozea nje.

Mhindi akamwambia najua nyie mnavyoniibia akamtaja jamaa hasa wewe mpaka route unachepusha na hesabu unaleta ileile, na ukiacha hapa kazi hautopata Boss wa kumuibia na akakuvumilia kama mimi
Boss kaua Mende kwa nyundo 🤣🤣🤣🤣
 
Kuna vijana hawabebeki kwa kweli na wala hawana Soni
Unampa mshahara ajira anayopiga humo humo na akiugua unampa hela ya dawa, mzazi akiugua unampa nauli na matumizi
Na akifa unamtumia za rambirambi ila bado mnatuona mapimbi
Halafu mwisho wa siku kijana anakuja kuwa na maisha mabaya wala huwa hawajali wanafurahia tu maisha ya umasikini
Hapo ndio huwa najiuliza hivi tatizo ni ubongo au ni aina ya wehu ambao wengi wanao
 
Udalali sometime unabutua mshindo mkubwa mpaka unaogopa?! Nyumba inauzwa 30mil dalali analengesha anapata mteja kwa 45-50m kwa maana hiyo 30mil ya mwenye nyumba 15-20mil ya dalali.Pathetic
Huo ni utapeli wala sio udalali, nishafanya kazi sana na madalali,
Nina appartments napangisha madalali nawaambia kabisa bei wakiniletea mteja nawalipa kiasi flani na pia wanautaratibu wao mteja akilipa anawalipa fedha ya udalali kodi ya mwezi 1.
Aidha nilishawapaga madalali kazi ya kuniuzia gari nikawatajia bei wakaitangaza bei ya juu kulipo ile niliyowatajia kimbembe kikaja kwenye malipo mteja anataka kuingiza fedha kwenye akaunti , nikamkubalia nikampa akaunti nikamtajia bei akabaki anashangaa mbona bei niliyoambiwa ni kubwa kuliko unayoniambia, nikamwambia bei yangu ndio hiyo na ndio nataka uweke kwenye akaunti yangu.
Mind wale madalali nilishakubaliana nao wakiniletea mteja wa bei hiyo nawapa kiasi flani.
Wale madalali walimind sana nikawajibu sinaga dili za wizi kama vipi ondokeni na mteja wenu .
Mteja akadhira akaondoka baadae akanitafuta kivyake tukafanya biashara wale madalali hawakupata kitu kutokana na tamaa zao manake mteja mwenyewe aliinunua gari akaipeleka mkoani hata hawakujua kama nilimuuzia yeye.
Madalali sometimes hovyo wanapandisha bei ya vitu wanasababisha visiuzike kwa mapema
 
Najua madalali tabia yao mbovu ni over priced ya nyumba au frem unakuta mwenye nyumba anapangisha nyumba laki tatu ila dalali anamchekecha mtu laki nne ili apate pesa nyingi ya mwenz mmoja bila kujali anavyomuumiza mwenzie kwa kipindi atakachookaa hapo.
Yaani umelenga humohumo.
Na kama unataka kupanga nyumba, jua wanakuja madalali kama 6 hv.
 
Kuna vijana hawabebeki kwa kweli na wala hawana Soni
Unampa mshahara ajira anayopiga humo humo na akiugua unampa hela ya dawa, mzazi akiugua unampa nauli na matumizi
Na akifa unamtumia za rambirambi ila bado mnatuona mapimbi
Halafu mwisho wa siku kijana anakuja kuwa na maisha mabaya wala huwa hawajali wanafurahia tu maisha ya umasikini
Hapo ndio huwa najiuliza hivi tatizo ni ubongo au ni aina ya wehu ambao wengi wanao
Mtu mweusi akipata kazi anawaza anaiba vipi. Kuna Transporter ana chinese trucks saizi kaanza kufunga mfumo wa gesi sasa madereva wazoefu walikuwa wanapata pesa kwa kupiga Diesel. Mtu akiambiwa week hii peleka gari workshop ikafungwe gesi anaacha kazi hawataki gesi
 
Back
Top Bottom