Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Mlimaliza kazi saa ngapi mwamba?
 
Safi sana Mkuu sasa hivi unapiga dili gani?
 
rikiboy peleka hii kwenye uzi pendwa
 
Angalau wewe umeonyesha kushukuru sio wengine wanaponda tu.
 
Dah jengo la Benjamin mkapa likiwa linajengwa nilikuwa saidia fundi,kuna siku nilikuwa empty mfukoni nikaona njia rahisi ni kuiba misumali nikauze,ile naiweka kwenye rambo mhindi akatokea na kuanza kunivizia anikamate nilijifanya sina ujanja ghafla nikamtoka huku akiita mwizi nikafanikiwa kutoka nje ukawa ndio mwisho wa saidia fundi sikurudi tena baada ya wiki moja kupita yule mhindi(babu tumbo)nikasikia kaanguka chini kafariki.
 
Hahahahahahah[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Hahaha nimekumbuka mbali kinoma, kipindi iko Nokia Express music na waptric ndo zilikuwa zinakimbiza [emoji23][emoji23]
Daah niliwatesa Sana pale IYUNGA na hii simu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] candy shop na in dar club zilikuwa zinabamba Sana kwenye hivyo visimu[emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Kwa upande wangu kazi hii ilinisaidia kukua kiakili, pale fundi alipokwepa jukumu lake na kunikabidhi mimi alikuwa ananipa ujuzi bureee, so pale alipohitajika mtu ambae anakitu cha ziada basi lazima niwepo.

Mafundi walikuwa wananitafuta hadi nyumbani wakipata kazi, Japo nilisha achana nazo kitambo ila nashukuru Mungu kwa kunipitisha uko.
 
Picha linaanza niliambiwa pima ndoo 120 za mchanga jamaa akawasha fegi hapo bado kuchanganya na kuanza kumsogezea,nakumbuka hii siku nilivyopanda kitandani hapo hapo nikasikia jogoo anawika kwamba kumeshakucha siku nyingine inaanza.
[emoji38][emoji38] nimecheka sana..kwamba bado kuna kuchanganya + kusogeza.
 
Mlimaliza kazi saa ngapi mwamba?
Mkuu hapo nimesimulia nusu tu hii kazi ilikua na shughuli sio ya kitoto

Ilifika wakati ukaanza mzozo kati ya wanaume na wanawake kua kazi haiendi kutokana na kipimo cha zege kua kidogo hivyo round ya pili baada ya lunch tutakua tunajaza

Wamama wakawa wabishi kua hawawezi kubeba huo ujazo so ikatubidi tuongeze kipimo kidogo tukaweka koleo tatu ila sio kwa level ya kujaa

Basi kazi ikaendelea na dakika zilizokua zikijongea ndivyo nilivyoanza kuyaona mateso. Pale katikati kwenye uchanganyaji zege hatukupewa zile plastic boots kwa ajili ya kukinga cement isidhuru miguu so hapa miguu yote ilikua tayari imeshika cement na kama ujuavyo ratio ya cement ya zege inavyokuaga kali

Nikaona bora ni switch niende kitengo kingine, nikataka niende kwenye msululu kupasiana ndoo za zege lakini nikamuona mwanangu mmoja naye anataka aje kwenye kitengo changu maana zile ndoo za zege zilikua zimelowa zege kwenye mishkio kiasi cha kufanya mikono ya jamaa kuanza kuuma.

Wamama walifunga kanga mikononi kama gloves ili waweze kubeba ndoo bila kudhurika na ile cement iliyoko kwenye vishikizo vya ndoo

Nikaamua niende kitengo kimoja cha kudaka ndoo kutoka floor ya juu mbazo zimesha miminwa hivyo zinatakiwa zirejeshwe chini ili zipakiwe zege nyingine. Kwahiyo mmiminaji wa zege pembeni yake kulikua na mdau mwingine ambaye alikua na kazi ya kuchukua zile ndoo na kuzirusha chini ambapo huko zinatakiwa zidakwe na mtu ili kuzuia zisipasuke

Basi nikajitusu kwenye kitengo cha udakaji ndoo kisha site manager akaagiza kazi ifanyike kwa speed ili tuwahi kumaliza mapema. Hapo ndipo mchaka mchaka ulipoanza kwanza baada ya lisaa limoja ukatokea ukimya huku ikisikika misonyo ya ghadhabu kwa wafanyakazi hasa wamama

mmoja akasema anaenda kunywa maji akazunguka nyuma ya kibaraza akasepa mazima, wawili walisema wanaenda chooni kwa muda tofauti tofauti wote nao hawa hawakurudi so nguvu kazi ikawa imepungua

Huku namimi shughuli ikaanza kuambatana na mvua maana yule mdau kule juu alielemewa na wingi wa ndoo hivyo akawa anazitupa roughly bila kuangalia hali ya mdakaji chini mpaka ikafika muda nikawa nazikwepa zinadondoka nyingine zinapasuka.

Site manager akasikika akitoa sauti ya mamlaka akinikemea kua nisikwepe ndoo badala yake nidake vinginevyo pesa yangu itakatwa kufidia hasara ya uvunjifu wa ndoo

Zile ndoo zilikua zimeshikamana na zege kiasi cha kufanya ziwe nzito pasipo hatazege ndani yake, nikajikuta mikono imechubuka damu zinatoka nikaamua kusepa fasta kwenye hicho kitengo

kwa ufupi

Ile kazi tulitoka mida kama hii majira haya haya ya saa 2 kuelekea saa 3 usiku na bado haikua imeisha so mtasha akasema tutaendelea kesho

pamoja na hayo Boss mtata akasema siongezi pesa niko tayari nilipe pesa ya kukodi hizi machine za kuchanganyia zege zukae hata wiki mbili

nilivyofika geto nilishindwa kuoga bafuni maana mikono yote ilijaa vidonda vibichi vilivyosababisha nishindwe kuvua nguo. Kwa jinsi mikono ilivyokua damaged nilishindwa unauma nilishindwa kula hata ugali kwa mikono nilitumia kijiko napo kwa shida sana

Nlienda kuoga mtoni kwenye kibwawa cha kuzuga nilijitupa kwenye maji hivyo hivyo nikiwa niko complete nguo hadi viatu. Na nilienda kulala hivyo hivyo na viatu

kesho yake tulifanikisha kumaliza kazi majira ya saa nane tukapewa mpunga wetu bila usumbufu nakumbuka nusu ya ile hela nili spend kununua madawa ya kujiuguza
 
Picha linaanza niliambiwa pima ndoo 120 za mchanga jamaa akawasha fegi hapo bado kuchanganya na kuanza kumsogezea,nakumbuka hii siku nilivyopanda kitandani hapo hapo nikasikia jogoo anawika kwamba kumeshakucha siku nyingine inaanza.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji119]
 
Nakumbuka tulivyobebeshwa tofali mzee sitamani kurudia kaz ya aina hiyo 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…