Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Ya moto sana
 
kuna siku bwana kuna kazi ilitoke homee ya ufundi mimi ndo nkawa saidia fundi fundi nlimpiga udongo mpaka alikimbia kazi akurudi tena na vifaa akaachaa vipo mpaka leoo kibegi chake chenye vifaa mkono bao,pima maji tukamba kamba na kijikoo hahaaaaa
 
Hii kazi nliifanya 2019 kipind nimemaliza chuo huku Ramani hazisomi Hapo Udsm kuna magorofa mawili marefu karibu na sehemu flan wanauzaga vitu mbali mbali hasa vitafunwa wanapaita kariakoo ,ilikua chini ya Suma jkt kwa siku Tulikua tunalipwa 15000, ..Ila mziki wake Sio pouwa ...Yan unabeba mchanga kutoka chini kupeleka floor ya 11 dah hii yan ilikua inachosha hatari baada ya mwezi nlizeeka na kuchakaa kabisa , Pia kuna hostel za Ardhi zinajengwa Kule makongo ...Tulianza kwenye kuchimba mashimo ,Hadi kumwaga zege ya foundation Dah ..Nashukuru Mungu nlikuja kupata kazi nkaachana na haya mateso ya saidia fundi ...Coz kiafya Sio nzur kabisa yan ilichukua muda mwili wangu kurudi kawaida ...
 
Estim construction company,mwaka 2009,posta tumepig mijengo kadhaa karibu na ghorofa la Benjamin mkapa mpaka leo siwezi kuwasahau wahindi wale,zege halilali,unatoka na ndoo ya litre 20 ghorofa ya Kwanza mpaka ya tano...kibarua mshahara 3700 per day na inaishia kwenye daladala na msosi wa maharage mabovu na chapat mbili kwa wasambaa pale manzese,asubuh unaamka hata mkono haunyanyuki kwa maumivu na mabegani cement ya Pakistan imekuunguza mabega full madonda,na muhindi kashasema atakayelala Hana kaz na huna kweli...unasindikizwa na muhindi nyuma Ana fimbo na matusi juu,mengine hata hayajawahi kupotea akilini nawatukanaga jamaa zangu tukigonga mvinyo wanaishia kucheka tu hawaelew ,maisha haya acha tu ila hawa jamaa posta waliifanya Kama kwao bombay walivyotawala sijui kwa Sasa maana nilikimbia hadi mji aisee! Ila muhindi mmoja alikuwa shoga akataka nimkule aliponikaribisha kwake akataka nimpge bomba Mara akaitwa na Bibi yake anayeishi nae humo ndani nikaiba laptop,simu tatu na wallet yenye pesa nying ndio chanzo Cha kusepa na kuacha kabsa ile kaz one day nitaweka hii story full,

Kama mpaka Sasa hawa wahindi wapo na wanaendelea serikali iwasaidie vijana wake.
 
Aseee
 
Mara yakwanza hii kazi nililipwa mia tano sikwenda kesho yake nikatafuta kazi sehemu nyingine hii kazi sio ngumu kama wengi wanavoisemea ugumu niwakaida tatiZo wengi hawajakulia mazingira yakazi ngumu changamoto yakazi hizi malipo mara nyingi huwa nimadogo halafu pia upatikanaji wahicho kidogo nayo nimtihani wengi utaona namna anavoizungumzia nikwakuwa hakuwa naulazima wakuifanya binafs sikuwa nachaguo lingine nemevumilia nikajua ufundi kidogo nikapata eneo nanikajenga mwenye nashukuru mungu
 
Duuh aisee haya Maisha Mungu atusaidie
 
Fundi anaangusha mwiko makusudi, halafu utasikia Dogo okota mwiko huo.

Halafu unakuta Dogo una degree na fundi darasa la saba.

Na wakati wa kuondoka unatakiwa uoshe vyombo vya fundi sasa ole wako utangulie kunawa kabla ya fundi.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sijafanya saidia fundi..ila nimebeba tofali zile ndogondogo na kuzifyatua nyingi sanaaa.
Kazi ya kuchimba kichuguu,kuponda udongo halafu kukimbiza folama sio mchezo asee. Ndio maana kiuno kimekaa tenge
 
Sijafanya saidia fundi..ila nimebeba tofali zile ndogondogo na kuzifyatua nyingi sanaaa.
Kazi ya kuchimba kichuguu,kuponda udongo halafu kukimbiza folama sio mchezo asee. Ndio maana kiuno kimekaa tenge
Nimefanya sana hizi kazi Shule ya Msingi.
 
Ile kazi ni ngumu mkuu, sema inategemeana na speed ya fundi mwenyewe,
Kingine utaiona rahisi Kama huna malengo mengine ya kimaisha
Mkuu kuikubali kazi ile sio kwamba unakuwa huna malengo mengine ila ilibidi niikubali nikiamini hiyo pia inaweza kunipeleka hatua nyingine wapo walioipenda nawakapata mitaji nasasa wanamaisha mengine kilakitu kinaanza naimani kazi yoyote nafikiri chakwanza uipende ukishaipenda inamaana utaifanya kwabidii naukishaifanya kwabidii ndipo unaweza kuona kama inamanufaa au la
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…