Tuliopitia Vita Na Chuki Makazini Tushirikishane Hapa

Asiyekujua hawezi kukudhuru
 
Mimi nimemwelewa . Kiukweli watu hao wanakupa at least a picha ya staff wenzako au workmates ambapo kadiri muda unapokwenda unazichanga karata zako vyema na kuji adjust accordingly
 
Nilkuwa nafanya field sehemu nikiwa chuo

Wakatuahidi tukimaliza chuo turudi tujitolee then watuajiri

Nilivorudi baada ya kumaliza chuo
Jamaa wakagundua nina kabiashara tena jiran na ofisini, wakanipga mizengwe

Nkaona isiwe shida sina cha kupoteza
 
Tulikuwa tunadai mshahara meneja alikuwa rafiki yangu sana(kwa nilivoamini) akampigia mkurugenzi ili tusikie upande wake.

Mkurugenzi akatoa majibu hayaridhishi, meneja akakata simu huku analalamika mkurugenzi kuwa na mambo ya kisenge mi nikasema huyu mkurugenzi ana mambo ya kifala sana.

Dah kumbe yule meneja hakuwa amekata simu nikashangaa mkurugenzi kanipandia hewani anawaka mixa kunitishia kwenda polisi kwa kumdhalilisha ila kilichoniacha hoi ni meneja kutohusishwa kwa chochote katika ile issue pamoja na yeye kuwa muanzilishi wa kutukana.

Mkurugenzi akaanza kunitenga sana ofisini akishirikiana na meneja nikaona isiwe kesi Mungu sio muhaya nika resign baadae.

Nilimuachia Mungu na kujifunza kutomuamini mtu. Leo yule meneja ni wakili na mimi ndo nilimpa laki ya kulipia mihuri miwili maana baadae alikuja kupitia msoto usio wa kawaida
 
Kumbe ilikuwa ni script ya manager na mkurugenzi ๐Ÿ˜…
 
Kbl sijapata transfer kuja hapa Dar nilipo sasa nilifanya kazi Arusha, hapo ofcn Arusha kulikuwa na wanawake kama 4 kwenye idara yetu kwa kifupi wote walikuwa kama maadui, wanachekeana nje lkn kiuhalisia wanachuki mno.

Siku moja mmoja alimiss place simu so ikawa namna ya kuipata ni mwingine kuipiga, one of the mdada akaipiga ile anasikilizia mlio unatokea wapi mara akaiona kuishika kumbe ameseviwa kwa jina "Nyoka".... aisee yule dada alilia wiki nzima!
Chuki iliendelea hadi wakawa wanachomeana TAKUKURU na ulozi ukaanza!

From that point nikarejea maneno ya mshua wangu aliwahi kuniambia hivi; dogo unaenda kuanza maisha yako, huko unakoenda "respect all, trust no body" hii issue naaishi popote na imekuwa ni moja ya tools zangu!!

Kwa kifupi sijawahi kutaka mazoea nje ya kazi na mfanyakazi mwenzangu yyt, tukitoka ofcn tumemaliza biashara huko.
 
Nilifanya kazi na "WAPALE" kwenye ofisi Moja

Aiseee Hawa watu ni noma sana aisee

Sitakuja kusahau jamaa ni wanafki sana

Yaani ni hatari...Wana majungu sijwahi ona...
dah mkuu. hawa watu sio nikadhani labda mimi ndoo nimewaona pekea angu. aisee hawa watu ni hatarii kufanya nao kazi. tunawaita wanawa hewa.
 
dah mkuu. hawa watu sio nikadhani labda mimi ndoo nimewaona pekea angu. aisee hawa watu ni hatarii kufanya nao kazi. tunawaita wanawa hewa.
Mkuu...nilifanya nae kaz wa kwanza ofisi Moja jamaa alikua snich kinoma
Nikamishwa idara nikakutana n mwingine
Huyu Sasa alikua moto Bora yule wa mwanzo [emoji23]

Cha ajab wote ni vidume yan full majungu...
Ofisi ya 3 ndo nkaja ku prove Hawa jamaa Wana shida yan ni vinamajungu hatari
 
Noma Sana ๐Ÿงข๐Ÿ––๐Ÿพ๐Ÿ˜…
 
Siku hiyo tupo kikaoni manager akasema 'Kuna laptops mbili zimeibiwa kuna mtu kaonekana, hizo ni tabia za kiswahili tafadhali rudisha kabla hatujakuweka wazi' kuna jamaa hua nataniana naye tukaanza tupiana vijembe juu ya huo wizi.

Ilikua Ijumaa, J3 kufika naitwa na administrator pembeni yupo manager jamaa akaniambia "Hii ni kazi na sijaenda polisi kwakua sitaki tuharibiane kazi, CCTV imeona unaingia humu ofisini siku ambayo naamini laptops zilipotea" nilishikwa na hasira ya ghafla kwa sababu kuu moja;

Mimi siyo mwizi.

Hata iweje mimi kuiba kwangu ni haiwezekani.

Nikamuambia "Bro hiki unachonihisi nacho kwangu mimi hiki is very low, tuendelee nakusikiliza" akaniuliza kwanini ulitoka floor yako ukaja hii? Now hiyo siku hiyo reception ya floor yao ilikua inawekwa stika kuna mdada akaniachia funguo akaniambia nimsaidie kufunga mlango fundi akimaliza.

Hiyo siku liva alikua anacheza na vila na alikua anaogozwa, so nikatoka kupanda hiyo floor. Nilivyofika sikuingia rooms zingine nikawa nimekaa juu ya meza ya reception napiga stori na yule fundi jinsi gani liva imeshuka kiwango.

Rooms zilizo around pale sikuingia kwakua sina haja ya kuingia. Kisha yule fundi akasema ameshamaliza ndani kabakisha nje so nifunge tu mlango nisepe. Nikafunga mlango nikamuacha jamaa anamalizia kazi zake.

Nikamuambia huyu administrator. Mpigie fundi ili athibitishe ninachosema, akasema hawezi kumpigia kwakua CCTV inaniona mimi nimeingia ofisini (CCTV inaishia kwenye kordo) nikamjibu sasa hiyo ndiyo legit reason ya kumcheki fundi ili akutajie kilichofuata baada ya CCTV ilipoishia. Akagoma.

Akaniuliza "Sasa kama CCTV ishakuona wewe ungekua mimi ungefanyaje?" Nikamuuliza "Lini ulithibitisha kwamba hazipo?" Akajibu J5 nikauliza lini ulithibitisha kwamba laptops zipo akajibu Jmosi ambayo wewe ulionekana umepanda huku.

Nikamjibu "Mimi ningekua wewe ningeanza kuangalia footages za Jmosi, J3, J4 na J5 yenyewe" akaniuliza sasa huo si mzigo nikamjibu ni kweli ila hizo zote ni siku zenye probability ya mashine kupotea. Nikanotice kinachomsumbua sasa hivi ni ameona footage hiyo moja na anataka hiyo hiyo iwe ndiyo uthibitisho, nikamuambia sijachukua nataka umpigie fundi hutaki akajibu nilishampigia nimeongea naye.

Akili ikaniambia ikiwa aliongea na jamaa this means jamaa kamuambia ilivyokua na kanotice haiwezekani niwe nimechukua so ni anajaribu tu kutafuta pa kupeleka lawama (ikiwa kweli zimeibiwa). Akamuambia manager hata hivyo kuna footage nyingine sijaiangalia twende tukaione kwanza. Akaniambia atanipa feedback.

Next day nikamuuliza manager ikiwa walienda akajibu hapana. A week later nikauliza ikiwa walienda akajibu hapana, a week later mkataba ukaisha na haujawa renewed.
 
Unasema wapare Wana majungu, unawajuwa waha wa Kigoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ