Tuliopitia Vita Na Chuki Makazini Tushirikishane Hapa

Ni stori ndefu, umeshawahi kuchukiwa bila sababu....basi from day one huyu HR alinichukia tu...Huyu HR wengi wanamwogopa,ana jina hapa,Neno lake ni sheria..akisema umekosa inatakiwa ukubali.
Sasa hapa staff wengi ni waoga,wanajipendekeza kwake mpaka na wazungu.
Mimi ni mtu ninayosimamia misimamo yangu siyumbishwi kabisa japo Corona imenitoa kwenye reli.
Baada ya miaka mingi kuona siingi 18 zake akajaribu kuunga urafiki baada ya miezi kadhaa nikaona haiwezi..nikaendelea na mfumo wangu wa mwanzo.
Nikaletewa boss,mapambano yakawa makubwa..Mwaka mimi na boss wangu hatuzungumzi...baadae tulimaliza tofauti zetu tukawa kitu kimoja...
Boss akanikubali sana,nikawa promoted
Miezi 7 sijaongezwa mshara wala sijapokea barua...
Nikaona wananitania,nikaanza tafuta kazi, simu zikapigwa kwa HR kama mimi ni staff wa hapa..
Akawa ananisiribia..mwezi wa nane nikaongezwa pesa na barua nikapewa.

Vita ikaanza upya kati yetu (mimi na boss wangu) na HR...

Tarehe 29 mwezi uliopita tukamfata mzungu,tukamweleza hali halisi...tukaona mzungu hana sauti.

Nikamwambia boss wangu hapa hamna kazi,na draft resignation letter, tarehe moja nawapa.

Usiku wake mzungu ananiita ananionesha boss wangu kashamtumia email ya ku-resign. Kaniwahi.

Leo hapa nimeshaandika yangu....
Nawaza ni wakati gani wa kuituma.

Nataka niondoke kwa wema tu,
Tuki-resign sote kwa pamoja itaonekana lengo ni kuikomoa kampuni.



Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Aisee kumbe nyie jamaa wa maofisini mnapigia mengi. Dah mmefanya nione bora hii kazi yangu ya bodaboda
Kila kazi ina changamoto zake kwa sababu Watanzania ni wale wale. Boda boda mnamchukia pia mwenzenu ambaye anapata wateja wengi mnaanza kusema ni mchawi, na nyie mnaanza kwenda kwa waganga. Basi inakuwa ni mwendo wa waganga tu! Hela yote inaishia huko kwa waganga halafu pikipiki ni ya hesabu.
 
Mie nashukuru sijafukka huko kwa waganga
 
Kabla sijanunua 'farasi' wangu, kulikuwa na bodaboda mmoja niliyekuwa ninamtumia mara kwa mara. Siku 1 nimefika kijiweni kwao, boda mwingine akaniita ila moja kwa moja nikaenda kwa boda niliye na ukaribu naye. Yule boda mwingine akanza kuropoka kuwa yule boda niliyemfata ni mchawi na wote wanajua.

Huyu boda nilikuwa nikikaa na kuongea naye unaona ni mtu mwenye malengo na anafanya kazi yake kwa umakini. Ila alikuja kuugua ugonjwa wa ajabu hospitalini haueleweki. Alizikwa mwaka juzi.
 
Hapo umechemsha kampuni huwezi kuikomoa Kwa kuondoka wewe. Labda uitie loss...

Unaporesign ni kwa faida zako binafsi na si kumkomoa yoyote yule
 
Re-sign tu kama ulishaamua. Hakuna Cha hasara
 
Nilkuwa nafanya mishe zangu za kitaa nikanunua gari...
mungu ni mwema nikapata na kazi nikaanza kaz huku namilik gari wacha weee idara nzima tulio kuwa na gari tuko 4
boss hana gari aisee nilijuta maneno kibao mara naringa mara mvivu kazn
 
Nilikuwa nafanya kazi somewhere kuna safari ikatokea tulitakiwa tuende maboss walivyosikia kuna safari ya nje ya nchi wakaanza kuleta ndugu zao na watu wao wa karibu kumbe manager anawachora tu alikuwa mzungu na ni organisation ya nje international company wakaanza kuambiwa watafute passport wakaanza mchakato mda ulivyokaribia,

inapelekwa list majina yetu hayapo na sisi ndio wakongwe yapo majina ya wageni tu mzungu akakataa akatoa list yake akasema nataka hawa waende kweli tukaanza mchakato tukaondoka kumbe mabosi hawakuridhia wakatuwekea kinyongo tulivyorudi tukaundiwa zengwe tukaondolewa Kazini wakadai tulikuwa tuna ringa na tunajifanya much know tukakubali matokeo tukaondoka kila mtu akapata chaka jingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! inasikitisha sana aisee,roho mbaya haijengi kabisa,kwa style hii,hayo maendeleo yatakujaje sasa?
Poleni sana mkuu.
 

Hizo lines za mwisho ume conclude vema sana. Privacy and Confidentiality.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…