HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kama vicheche waliovaa nguo fupi wameruhusiwa hapo kuna double standard
 
Interview ya kwanza ni muonekano ws mtu. Mambo mengi unaanza kuyajua hapo.
Kabisa.Tena waanze na usafi/umaridadi wa viatu.Kiatu kiwe rasmi,kisafishwe vema na kuvaliwa kistaarabu.Kwa taarifa fiche;Mara tu utokezapo mbele za watu baada ya salamu,macho ya muangaliaji uhamia kwenye viatu hata kama hajapanga kukuangalia miguuni.Kuwa mjanja!
 
Akili za Gen Z mnazijua wenyewe. Huna hela ya kununa nguo decent (kwa official events ikiwemo hizo interview) ila una smartphone? Nyie ndio mlipaswa kuwa blacklisted kabisa kwenye hizo ajira za serikali.
 
Jean,simple laba na mashati mazuri hayana umri mzee ila nasema tena life bongo ni ngumu sana mimi naona hata wanaofanya kazi hapo unakuta kiatu kimeenda upande wengine wanaweka chuma ili kisiishe..
 
Hapa umejitakia mwenyewe
 
Jean,simple laba na mashati mazuri hayana umri mzee ila nasema tena life bongo ni ngumu sana mimi naona hata wanaofanya kazi hapo unakuta kiatu kimeenda upande wengine wanaweka chuma ili kisiishe..
Toa mlungula watu wakanunue suti Sauz na Dubai. Waendeshe magari ya maana. Na kuishi kwenye majumba kama ya wabunge wa chama chenu
 
Sasa unalalama nini?
Hiki ni kizazi cha hovyo sana! Hopeless kabisa.
Iliaminika nchi hii itakombolewa vijana wakisoma, vijana wenyewe ndio hawa hata kutofautusha kati ya kijiwe cha bao na ofisi ya umma hawajui.
 
Vijana jifunzeni dress code. Sio kila nguo inafaa kwa tukio flani. Kama umeshindwa kujua dress code kwenye ofisi ya serikali ambayo imewekwa wazi ushafeli usaili tayari.
 
Sasa unalalama nini?
Hiki ni kizazi cha hovyo sana! Hopeless kabisa.
Iliaminika nchi hii itakombolewa vijana wakisoma, vijana wenyewe ndio hawa hata kutofautusha kati ya kijiwe cha bao na ofisi ya umma hawajui.
Hawa ndio wanaliwa vyooni huko makazini kwa kuendekeza tamaa na kwenye zile party za ofisini wakishalewa
 
Unabahati, ungekutana na mimi mbona ungefurahi?

Ningekununulia Safari larger 10, barudiiii na nyama choma ya kutosha
 
Gen Z, baadhi yenu mnajifanya wajuaji sana.

Hivi kila kitu lazima kibishwe? Taa nyekundu mnavuka, stendi hamtaki kutumia, taratibu na kanuni hamtaki kufuata halafu mkikumbushwa mnaita ukandamizaji nk!

Millennials sasa wameamua kuwafundisha kwa lugha mnayoielewa.

πŸ˜… Dunia ina mifumo, ina taratibu na ina kanuni; binadamu si mnyama asietumia utashi, hufanya kila kitu kwa utashi wake na kufuata taratibu zilizokubaliwa ktk jamii husika, else kakae pekeako huko wapi mbwinde!.

Kama usaili/public service imewekewa dress code, si jambo la kujadiliwa kama mnaenda beach.

Jeans na raba si tatizo kwa ujumla, lakini kama mwajiri ameweka utaratibu wa mavazi kwa ajili ya usaili, heshimu taratibu acha ujuaji!

Hongera TRC na Utumishi kwa kusimamia viwango.

Wengine mtaelewa kwa lugha ngumu.

Maana ukianza kazi ukiwa na tabia ya kubisha kila kanuni, siku ukiajiriwa unaweza kuanza hata kuwatukana abiria hapo TRC bora wameku filter out mapema!

Kuchujwa mapema kunaweza kuwa fundisho kuliko kuajiriwa halafu ukashindwa kuendana na mfumo πŸ˜… kwisha wewee

Kafanye uwinga
 
Umewapa shule swaafi ila sijui kama wataelewa. Tumekua na kizazi cha honyo sana sasa hivi.
 
Shida yenu kubwa watoto wa 2000 ni ubishi, utoto mwingi, ujasiri wa kipuuzi, kutokujali, kutokujitambua, na kujiamini kupitiliza. Mimi naamini waliwatendea haki kwa kuwaondoa mapema kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…