HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Jero tu Mtaani taabu..jamaa anaongelea elfu 5...! Unafiki na kiburi Cha Kibarua alichonacho...
Hali ni ngumu.sana kitaa..Mtu anatembea kwa miguu na bahasha kusaka kazi hana hata mia ..
Niliwahi kwenda kupeleka barua pale Caterpillar yule dada alinionea huruma akanipa nauli kwa vumbi la viatu nililokua nalo maana nilitoka Posta nikavuruga Kariakoo nikaenda pale hapo nina nauli moja tu ya kurudi wale jamaa walikuja kunipigia simu baada ya kupata kazi nilirudi kuwashukuru kwa utu wao..
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Pole , utaendaje hivyo sawa na wewe kwenye interview watumishi wa umma ni wapi na wapi pamoja na t-shirt & jeans.
 
Swala la nguo sio rahisi kama mnavyoongelea aisee life bongo ni ngumu sana tusaidiane tusilete dharau kwa wasiojiweza...
Watu wananunua nguo ngumu na viatu vigumu sio kwa fashion ili kuvuta tu muda mpaka mambo yaende sawa mimi siwezi kumlaumu mtu hana kitu fulani na huku kazi hana...
Uko sahihi kabisa mkuu, lakini serikalini hakuna atakayemsikiliza, ndiomaana hapa wanatumia njia ngumu kumueleza ukweli ndio huo!
 
Swala la nguo sio rahisi kama mnavyoongelea aisee life bongo ni ngumu sana tusaidiane tusilete dharau kwa wasiojiweza...
Watu wananunua nguo ngumu na viatu vigumu sio kwa fashion ili kuvuta tu muda mpaka mambo yaende sawa mimi siwezi kumlaumu mtu hana kitu fulani na huku kazi hana...
Hoja unayo nzuri tu.Lakini,kuna wale wenzangu na mimi ambao mavazi si shida kuyamiliki.Changamoto yao ni aina gani wavae.Zamani zile zangu za utineja hadi early 30s nilikuwa sipendi tu kuvaa suruali za vitambaa,mashati ya kawaida(viscose kwa mfano)na viatu vya kawaida kiofisi.Nilipenda jeans,kadeti ngumu,ma-timberlands n.k.Leo hii nimekubaliana na hali.Mvi nitetee!
 
Back
Top Bottom