HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
We Mpumbavu usikute jeans yake na T. Shirt zina bei kuliko hata suruali na Shati ambazo Utumisi wana recommend avae
 
Ni sawa kabisa

Kabla ya interview unatakiwa kujua manners za potential recruiter. Na mwajiri hapo ni serikali na ana taratibu zake
 
mostly vijana wenye vijitabia vya aina hii, ni wale wanao toka familia bora...yani hata bila hiyo kazi, mama ake huwa anampa pesa za matumizi kila week/mwezi na anakaa nyumbani misosi bweleleeeee!!!!!! atawezaje kuwa serious kwenye maombi ya kazi?
 
Kazini ukishaingia unaweza kuvaa ila siyo kwenye Usaili
watoto maisha bora hao mkuu, anakaa nyumbani kwao, ukutani flat kali la nchi 70...geto kwake mama ake kamuwekea ps5 kali, afu dogo akilia tu kidogo mama ake anamkunjia laki kadhaa za matumizi....ndani misosi bweleleee yani dogo hajui msoto wala njaa....unadhani atakua serious na usaili huyo!!!????
 
Vijana wa sasa kama vichaa , huko chuo wanavaa kama vibaka , manguo makubwa ...Vijana kila kitu kina utaratibu wake , usiendekeza demokrasia , hayo manguo yenu ya mtumba ynaenda kukukosesha kazi .
 
usaili chukulia serious ,
Siku hizi ukiwa na 20k hukosi hata Suti ya kuchemsha ukikosa sana AZIMA ,

Bottom line : HATA UWE NA AKILI NYINGI KIASI GANI KAMA HUNA NIDHAMU NI BURE KABISA
 
Ulitakiwa uchapwe bakora 3 za kwenye makalio kama adhabu siku ingine usinge rudia huo UJINGA.
 
Na huku mtaani hapachekeshi 🤓
Cc: Mbaga Jr
View attachment 3653080
😁😂

Juzi kati nimepiga zangu konyagi ile nimetoka natembea

Njia nyembamba kwa mbele jamaa kasimama katikati ya barabara anachati anachati Hana habari kabisa na jezi ya Simba na kitumbo tumbo chake

Nikatembea nikampiga kikumbo ki makusudii aka Anza kulalamika nikamwambia njia nyembamba kama unataka kuchati au kuchezea simu simama pembeni TULIA maliza jambo lako endelea na mishe zakoo

Tukakoromeana tuka achana kimjini mjinii
 
Ila itakuwa ulijizima data tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…