Mimi mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia, ukioa na mkeo akakucheat, deal na mkeo na sio mwanaume mwenzio.
Unakuta mwanaume unamkuta mwanamke bar au sehemu ya starehe, mwanamke ana dalili zote za udangaji ila kisa tu ana penzi zuri na ana mwili mzuri unaamua kuweka ndani.
Unaoa mwanamke kwa kumvuta na pesa zako, kipindi cha dating red flags kadhaa unaziona ila unapuuza, background ya mwanamke hairidhishi ila mtu unakaza moyo.
Kwenye ndoa kuna muda mapenzi yanaisha na hii inaweza ikatokea kwa mtu yoyote yule sio mwanamke wala mwanaume. Sasa mtu alikupendea kwa pesa, ila moyo wake ulikuwa kwa mwingine, alikunwa vyema sehemu nyingine, tegemea tu kugongewa ujue au usijue.
Ukiona unakosewa mimi nakubaliana na yule mzee, better udeal na mwenza wako na sio huyo uliyemfumania nae, wengine wamediriki kuachanisha penzi ili amuoe mtu au aolewe na huyo mtu.
Aisee hizi ndoa hiziiii, ngoja mimi nijipe muda zaidi.