Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.
Dah mpe pole sana mkuu!! Kwasababu hana mtu jitahidi uwe nae karibu maana kwa upweke anaweza hata kuwa chizi asee!! Pia kama ukiweza mpe tafu jitahidi umuinue hata aanze biashara...mpe sapoti mkuu!!!

Niko kwenye hard time ila nilivyosoma hii naona namdhihaki Mungu kwa kujiona nna hali ngumu daaah!!
 
Utaibiwa hutasahau
 
Samahan ndugu yangu sina maana mbaya ivi kwa mfano uo mshahara wa 197 000 kabla ujakatwa kodi yyt unalipwa sh ngap
 
Unalipwa sh ngap
 
Baada ya kuchoka mishahara ya wahindi niliamua kujiajiri, nikawa nafanya biashara ndogondogo maisha yanaenda, nilikuwa nachukia Mikopo Sana, baada kuingia Kwenye biashara hukuhuku nikaona bora niingie Kwenye vikundi vya wanawake pamoja na Vicoba, nilikuwa na Vicoba vitatu na vikundi vinne vyote nilikuwa na vihudumia naweka tu Pesa sikopi.

Baada ya story za Mikopo za wanachama wenzangu Sasa na Mimi nikaona acha nikope bank nifungue biashara yangu moja ya uwakika nikakopa mil 10 marejesho miaka mitatu, Pesa yote niliingiza Kwenye mzunguko wa biashara mwaka wa kwanza marejesho yalienda Safi Kabisa mwaka wa pili matatizo yakaanza biashara zikafa nikabaki na shamba la korosho na msimu Kama mnavyojua mwaka kwa mwaka. ikawa ikifika tarehe ya rejesho nakopa Kwenye kikundi napeleka bank ikafika wakati vikoba vyote vitatu na vikundi mpaka wanachama wananidai Huku rejesho bado halijaisha la bank.

Nikavuna korosho nikasema Pesa Itanisaidia kupunguza madeni, mwanaume niliyekuwa naye akanishauri usilipe Pesa yote madeni zungushia biashara Huku unalipa madeni kidokidogo. Pesa nikampa mpenzi tuzungushe biashara akanidhulumu ikafika wakati sina hata mia mfukoni marafiki wote wamenikimbia bank nadaiwa, kila kona na madeni Sina kazi Sina biashara nilala ndani Kisa madeni ya watu ya riba mitaan sitaki kukumbuka nilisota nakusota. Ndugu Zangu ikabidi wajichangishe kulipa Mkopo WA bank iliyobaki maana ilibaki miez michache niliiweka dhamana viwanja vyangu viwili. Wakaona bora wanisaidie kuliko vipigwe mnada wakati nilibakisha kidogo.

Hii Mikopo mingine ya vikundi, vikoba na mitaani watu walinidai mpaka walikaa kimya na kuchoka maana Sina kitu Niko mweupeeeee. Baada ya kuumalizika Mkopo WA bank nikauza kiwanja kimoja nikalipa lipa madeni ya mitaani nikabakiza Pesa kidogo nikaaza na moja biashara

Sasa hivi sitaki kusikia Mikopo, vikoba Wala vikundi maana kwa wanawake wengi humo Ndio Huwa Chanzo cha matatizo na wahanga ni wengi maana humo watu wana ushawishi wa ajabu, Kama Sina najua Sina ila Sina Deni na mtu kuliko huna alafu udaiwe utatamani ufe kwa muda. Mikopo inaumiza .
 
Izo zinakua imani tu imagine ww bila kurubuniwa na mtu yyt unaamua kuweka nyumba dhamana umeshindwa kulipa kuna mtu atakua amekuonea zaidi upambane na hali yako
 
Ahsante sana trust no one aisee hasa ndugy coz huwezi kumfunga wala kumpeleka polisi
Kuna mmoja tunafanyanae kaz,likizo ilipokaribia akachukua loan 4m kwamba akifika hom arekebishe nyumba ya wazazi wake,alipoikamata 4m hata likizo akaahirisha kwenda hom,akabaki mjini akazitumbua zote zikaisha bila kununua hata kochi Mpya getoni kwake[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Dah, maneno mazito sana ndugu yangu, umetoa somo zito sana hongera
 
Mpaka dakika hii inaonesha tayari jamaa kashakufanyia shiriki, hali ya kutokuwa huru na mali yako kwa mazingira kama haya, ni dalili tosha kuwa kuna shiriki imefanyika. Fanya mpango ujikwamue kwenye shiriki hiyo Mkuu.. Pole sana..
 
Pole zake hiyo jamaa, Kukopa si mbaya tatizo nidhamu ya kukopa ndiyo tatizo
 
Kama huna usimamizi wa moja kwa moja baba hiyo pesa itapotea kopa mkopo wa muda mfupi kwanza at least 1yr ufanye hizo biashara ujue hasara na faida zake then next year uchukue pesa nzur uiboreshe hiyo business au uachane nayo

Trust me hutajuta
Asante mkuu,your advice will be considered...
 
Wakubwa mi nimeshaprocess mkopo kwa ajili ya kununua nyumba ya jamaa yangu aliyeshindwa kufanya marejesho ya mkopo wa bank fulani hivi daa moyo wangu kama umeanza kwenda mbio nahisi na mimi katibia nitaanza kuishi kama shetani hivi.Si unajua jamaa nae kakaza balaa
 
Ila mishahara wanaolipwa wachezaji hauna siri!hivi kwa nn?
Mishahara inajulikana haswa kada za serikali but kuuanika mitandaoni unaweza ukaonekana kama una kaakili ambacho hakijakaa vizuri.Ndivyo ilivyozoeleka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…