Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Hahahhaa, watumishi wa serikali naona mikopo inawaumiza kweli, hii ni kwa sababu tu hamzijuwi mbilinge na mishe za mtaa. Mke wangu mimi naye anaendelea kulipa mkopo wa pesa nyingi ambazo alikopa, akafungua duka na kununua pikipiki kadhaa. Wakati anaenda kukopa hakuniomba ushauri wowote, lakini mimi niliziona forms za mkopo...skumuuliza kwa sababu ni non of my business.

Alipoingiziwa pesa akaja kunambia amechukua mkopo wa pesa kadhaa anataka kufungua duka la rejareja anaomba nimsaidie kupata wasambazaji wa bidhaa kwa bei nzuri na kumsaidia hesabu jioni. Skuwa na hiyana, nikamwambia Duka la rejareja sina uzoefu nalo, lakini to what I know linahitaji usimamizi wa karibu sana muda wote uwepo dukani, na wote ninaowafaham mimi waliofanikiwa kwa biashara hiyo wanashinda dukani full time, yeye akanijibu ameshaamua, na ana maono makubwa sana mbele juu ya biashara hiyo.

Basi nikamsaidia kupata wauzaji wa bidhaa ninaowafaham akajaza mzigo dukani, suala la kusimamia hesabu nilimwambia akomae yeye mimi muda wangu uko tight afanye yeye mwenyewe (nikweli sikuwa na muda, na skutaka kujihusisha na biashara nisiyo na uelewa nayo), akanunua na pikipiki nne mishe zikaanza. Haukuisha mwaka anaomba nimwongezee pesa ya pango la duka!!!

Pikipiki zote ameshauza kwa kugombana na madereva. Wakati huo sisi wazee wa mishemishe tunazama na kuibuka, ukigeukia huku unatandikwa ukiinuka unacharaza biashara zinakwenda na mikopo tunachukua yakushiba vilevile, nyumba za kukopea zipo na tunaendelea kkujenga, ukiona mkopo huu biashara unayofanyia imezingua unawauzia benki nyumba pesa unahamishia kwenye biashara nyingine kunakuchwa kunakucha mishe zinaendelea.

Nyie watoto wa mama mmezowea kuingiziwa pesa kwa mwenzi wengi wenu mnaishi kwa ndoto bila kujua kukaza, japo wapo wengi pia ambao tunapigana nao vikumbo mjini wanakomaa na wanafanya poa sana tu!
 
Hii mada imenigusa kidogo.... Inaonekana wadau wengi wanachukua mikopo withno gud plan.... Mkopo sio wakujengea nyumba au kuanzia biashara, mkopo ni mtam sana kwa ajili ya kuendeleza bzness, chukua mkopo kulingana na mahitaji ya biashara yaako kwani pesa ikizid mahtaji ndo hapo utakaponza kuitumia hovyo.

Kabla yakukopa fanya bzness kwa kpato kidogo ulichonacho ili upate uzoefu wa hyo bznar, mfano wewe ni wakala wa mpesa anza hata na mtaji wa laki7 mzunguko wako ndo utakwambia ukope shngapii...
 
Mkuu nimecheka mnoo . Dah mie kunajamaa ananishawishi niingie bitclub lakin moyo unagoma
 
bado hujamalizia ilikuaje huo mkopo wa mkeo
 
mkuu kuna jamaa mmoja alikuja pia kunipump sijui D9 inaleta usenge gani nikamwambia sina muda hata wa kukusikiliza we endelea na mambo yako... siku si nyingi nikasikia jamaa anatembea anaongea barabarani peke ake ..
 
Hebu nipe namba za huyo dada yako nimfunze adabu.
hahahaaaa babu bwana

unajua ndugu wengine ukitaka kufanya nao kazi au biashara wanakuwa hawaelewi umeptaje pesa mpaka mkaanza kuingia partner wao wanachojua ni kula tu hizo pesa pasipo kufanyia kitu chochote kwani haziwahumi hawajui kuwa mtu unatafutaje pesa kwa jasho hata mm ningemchapa viboko huyo sista hahaaa
 
Watu kama nyie mkipigwa pesa mi huwa hata siumii.
 
Mmmmh hatar nipe link Mkuu ya huo Uzi nipite nao Mdogo Mdogo kuna mengi ya kujifunza


Stay strong mkuu
 
Wakuu hembu kwa anayeijua KUNET naomba anidadavulie mama yangu mzazi wamemshika kweli kweli na masemina yao .
 
Wafanyakazi wengi, Mkopo wa kwanza huwa wanakosea...wapo wengine makosa hayo, huendelea kuyafanya hata baada ya makosa ya Mkopo wa kwanza.

Biashara na kazi inahitaji plans iliyoenda Shule, na unapo anza Biashara kopa hata kwa rejesho la mwaka mmoja tu...ili makosa au hasara utako ipata kwenye Biashara yako kwa Mara ya kwanza, after a year utakuwa umeshajifunza mengi na hutarudia tena...then kopa tena kwa mwaka moja...baada ya kukomaa ktk Biashara....ndpo sasa unaweza kuongeza loan period hata 2-3yrs...ili uendelee kupata experience...
 
Wakuu hembu kwa anayeijua KUNET naomba anidadavulie mama yangu mzazi wamemshika kweli kweli na masemina yao .
mwambie aingie kichwa kichwa apigwe pesa. watanzania huwa hawasikii mpaka wanapomaliza kutapeliwa.
 
Kuna jamaa m1 alichukua kama mkopo benki moja sijui kiasi gani. Ananunua kiwanja kibaha akajenga kufika katika linta hela ikakata. Akakosa hata hela ya kodi alipopanga cz makato yalikuwa makubwa hakubalikiwa na kiasi cha kumtosheleza na alikuwa ameoa. Kelele za mama mwenye nyumba ikabidi mkewe akasirike arudi kwao Moshi. Yeye ikabidi ahamie kibaha hivyo hivyo.

Sasa balaa hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa mtihani. Ikawa mtoro kazini. Anaenda Mara 1 au 2 kwa wiki kazini. Kesi za utoro zikazidi akasimamishwa kazi. Jamaa kapagawa. Maana hana kitu kabisa. Mkewe wameachana na naskia aeolewa na mtu mwingine. Naskia yuko bagamoyo analima vibarua.
 
bahati unayo tu.

Ila pole... bado una mtaji wa million 4 ulipo... umiza ndonga utaiona braza
 
Kuna mshkaji wangu mmoja miyeyusho sana nikikumbuka nashindwa kumwelewa aliwaza nn..
Iko hv jamaa alikuwa amepungukiwa budget ya harusi yake alichowaza ni kuniomba hati ya kiwanja changu ili apewe mkopo na taasis flan ya fedha,ofisi yake haikuweza kumsponsor kwani alikuwa still under probation,nakumbuka nilimwangalia huku nikiwaza mengi na kumpa jibu rahisi tu HAIWEZEKANI.

Akaenda akapambana kivyake harusi ikafanyika kibishi...alipotoka tu honeymoon kakuta kibarua kimeota nyasi.
Niliwaza kimoyomoyo je ningeendekeza ushkaji nikampa hati yangu ili tu apate mkopo wa kuolea angekuja na stori gani,?

Nadhani kuna haja ya kuanzisha darasa kwa wakopaji wapate elimu tuelewa in deep lengo la uwepo wa mikopo ili tufunguke akili zaidi tusiingie kwenye mikopo kichwakichwa na kuambulia stress
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…