Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Pole sana.
 
Pole sana.
 
Haah unaogopa nn wakati ni pikipiki yako.
 
Mwenzenu mi kabla sijachukua mkopo baba alinishauri niwe natuma pesa kwa ajili ya kupata kiwanja na ujenzi baadae, sasa kidume nikajipinda, kila mwezi nilikua natuma laki mbili na yeye aliniambia kiwanja kinauzwa M2. Sasa miezi ilikatika naulizia kiwanja najibiwa pesa hazijatimia hahaha ikabidi nimuulize mama, jibu ni kwamba "Pesa zinatafutiwa mchele ila kapanga akipata pesa atakuja kukufanyia maarifa" duh! Nilikata tamaa ya kiwanja ilikua mwaka 2013. Hiyo ya kwanza;

Ya pili, ilikua mwaka 2015 nilichukua mkopo wa M13, milioni 6 nilizivuruga sikujua hata nilitumia nini, zilizobakia nilimtumie baba aninunulie kiwanja na kupiga japo foundation. Na hapa niliula na chuya, alinunua kiwanja chenye foundation zilizobakia akamalizia nyumba yake nikaahidiwa deni kwamba atakuja kunilipa, ila baba ni baba siwezi kumdai tena na najua silipwi kala mali yake mwenyewe.

Mwisho kuna mpango mwengine nataka nije nifanye kwa siri halafu nine nikwambie, mpango wenyewe ni kuja kununua japo banda la M25 maana nikimshirikisha atakuja kunilamba tena.
 
Alikili zako pia haziwez kukusaidia asa sijui iyo kaz unafanyaje, toka lini na wapi umeona biashara binafsi unafanyiwa na mtu haupo makini wewe ni mzembe.
 
Nilichojifunza mimi,usikope ili kununua kiwanja au kujenga nyumba ambayo haizalishi bali kopa na wekeza kwenye kitu kitakachokuwa kinazalisha ili mkopo ujilipe wenyewe
Ndo hapo sasa kwakuwa ni mtumishi unawekeza unamuweka msimamizi anakuingiza mjini mchana kweupeee
 
Nimepitia kwa makini sana michango ya wachangiaji wengi kwenye uzi huu.

Kutokana na uzoefu wangu na wachangiaji wengine, kukopa pesa ufanye biashara ikisimamiwa na ndugu au rafiki ni kujitakia kuishi kama shetani.

Watu hutofautiana uwezo na access ya kukopa. Wengine humu nimeona wanauwezo wa kukopeshwa million 10 wengine 20 na wengine mpaka million 200.

Kwenu nyinyi wenzangu tunaoweza kukopeshwa chini ya million 10, hakikisheni kama ndio kwanza tunanza kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara basi tubuni biashara inayoweza anza kwa mkopo ambao unaweza kuulipa kwa kipindi cha mwaka 1 tu deni liwe limeisha. Hii husaidia kupunguza ukubwa wa riba na hata ikitokea biashara imekufa muda wa kusota huwa mfupi sana.

Binafsi huwa na ndoto ya kuwa na mtaji wa hata million 50 lakini hujiambia biashara kubwa kiasi hicho sharti izaliwe na biashara nyingine ndogo niliyo ikopea kwa makato ya mwaka mmoja tu na si vinginevyo.

Kama hatuwezi kuanzisha biashara kwa makato ya mwaka mmoja tu basi hata tukikopa mapesa mengi ya kukatwa mika 4 biashara hiyo haiwezi fanikiwa.

Kama unataka kopa pesa kununua bodaboda ya biashara si kitu kibaya, ila jipime kwanza kama wewe mwenyewe utakuwa tayari kuipigia kazi in case madereva wanakusumbua alafu ukisha kuwa na bodaboda weka mashaliti magumu kwa dereva unayetaka kumkabidhi hasa juu ya upotevu kama itatokea.

Madereva wengi hupoteza bodaboda kizembe sana hivyo ni bora muandikishiane namna atakavyo wajibika kuilipa iwapo itatokea upotevu wowote ule na kama hajiwezi kabisa basi awe na mdhamini wake. Kumkabidhi mtu pikipiki bila mkataba ni sawa na kutupa pesa chooni.

Binasfi niko mbioni kwenda kopa pesa kununua bodaboda ya biashara lakini kama nitakosa dereva wa uhakika wa kumkabidhi mimi mwenyewe nitaingia barabarani kama ufanisi wangu wa kazi nilikoajiliwa utadhorota kutokana na mimi kwenda kazini nimechoka poa tu sito jali hilo maadam nisipopambana na hali yangu hakuna wa kunisaidia dunia hii.
 
Hao ni matapeli mkuu.
 
Pole mkuu umenisikitisha ulivyomalizia hapo mwisho. Endelea kupambana
 
Kama yaliyonikuta dogo alilukuwa anaishi nikawa natuma hela za kula na kulipia fundi na vifaa ili nikienda nikute mjengo umekamilika.baada ya miaka 3 nikaenda kwa wife na watoto nikijua nafikia kwangu.sikukuta cha mjengo hata tofali moja.

Hasira nilizonazo nilimweka ndani dogo cha kushanganza mother akaja polisi na kuwaambia kwamba yeye ndio alimwambia dogo watumie hizo kwa matumizi mengine kwa sababu mie nakula raha mjini na Huyo mwanamke niliyenaye hivyo kama kuwekwa ndani awekwe yeye dogo atolewe.

Sikuwa na la ziada zaidi ya kuondoka ukizingatia hizo pesa tulikuwa tunachanga na wife wote tulikuwa wafanyakazi uamizi niliofanya ni kujenga ukweni ambao hawakuwa na mchezo mchafu kama wa kwetu SAA hizo kunibeza na kunilaumu nitajengaje ukweni inaonekana nimelishwa dawa
 
Duuh pole sana kijana mwenzangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…