Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Pole sana ndugu!

Hadi umri huu sina historia ya ajali iwe ya gari binafsi ama magari ya abiria......

Sijajua ni kwasababu sisafiri sana, ama ni uoga wangu nikiwa barabarani ama ni kwakuwa nimejifunzia gari ukubwani...


Naogopa sana ajali.
Nikuombaa MUNGU tuu ajali inakufuata mahali popote pale wakati wowote. Unaweza tembea au kuendesha kwa tahadhar lakin akatokea mtu na yake akakuvaa. Hivii vitu havinaga mjanjaa
 
Mshana bwana !natamani nikuone live yaani hapo inamaana kunapepo la ajali ila sababu wewe mtu mzito ulilikwepa ndio unamaanisha.
Ngumu kusema kwa hakika ni nini kilitokea kumbuka ilikuwa usiku
 



duhh km movie aic ,na bora usiruk ungeruka ungekuwa marehem aic,pole sn aic shukuru Mungu
Dah una mbwembwe sana kijana. Mimi nilipata ajali mpaka leo nina kumbukumbu ya chuma mkono wa kushoto.
View attachment 525278 View attachment 525279
Dah una mbwembwe sana kijana. Mimi nilipata ajali mpaka leo nina kumbukumbu ya chuma mkono wa kushoto.
View attachment 525278 View attachment 525279




yaan had nimesisimka aic duh mm hii ningekufa tu kuuangalia huo mshono uwii,,kweli umshuru MUngu dah
 
Poleni sana mliopatwa na masaibu ya ajali mungu atuepushe maana nasoma Uzi mpaka nasisimka ukizingatia sijawahi hata kuona ajali labda kwenye mitandao ,sio kwamba Mimi ni bora au sina dhambi nikwa Neema tuu


yeah sure
 



hahhaah eti una 50/ hhahah pole aic mie kubiringita gari kwakweli naonaga kwenye muvi dah
 
Mwaka sikumbuki nilipata ajali ya Pikipiki dereva alifunga breki za ghafla na kupelekea Pikipiki kuluka juu na kutuangusha barabarani na kuingia uvunguni Wa pikapu ya upande mwingine ,dereva Wa pikapu alinichungulia kwa halaka chini na kukwepesha taili ya mbele kidogo kwahiyo taili ya nyuma ikasogea kidogo ndipo ikakanyaga nywele za lasta nilizokuwa nimesuka .Watu walipiga kelele za mshangao zile za watu Wa barabarani wanazopenda kupiga sababu ilikuwa shekilango kwenye magereji walifikili nimekanyangwa kichwa, mwenzangu alitupwa upande hulehule Wa barabara na yule dereva Wa pikapu baada ya kunyosha kama alipokuwa anakwenda yeye aliingia mtaani kwakasi alifikili ameua .Nashukulu nilitoka salama ata mchubuko huku nimeshikilia pochi yangu inapesa nyingi kwakweli baadae nilijicheka sana jinsi nilivyodondika huku nimekumbatia pochi yangu .
Watu walitusogeza pembeni sababu tulikuwa na kiwewe na kuchanganyikiwa mwenza wangu alivyoinuka yuko palepale chini anajizoazoa barabarani ananiuliza uko salama ujaumia? Mimi sikujibu nilikuwa na wenge balaaa mpaka hapo akili ivyokaa sawa baada ya kutolewa barabarani .wakatujalia watu na kuniambia wewe ukachinje kuku au utoe sadaka .kwakweli wakati wako kama bado uwezikufa mpaka wakati ufike sio kwa mapenzi yake Bali ajapanga nife siku ile ila nitakufa tu wakati ukifika ukuta.
 


jicho lilipona?duh hatari kweli kweli
 



hahhaha lazima una uchaga ndan pichi hukuiaCHIA ?TEH TEH pole sn ,ndo nmaana mwaka umesahau lol
 


hahahah na mara nyingi tunarudi kwa MUNGU wakat huo umenusurika ukipona unasahau,mby sana
 
2014 nilikuwa ndani ya bunda bus ile iliyogonga treni pale Manyoni. Nilishtuka watu wanapiga kelele kabla sijatafakari vizuri nikasikia kishindo na kujikuta nimerushiwa juu ya siti za upande wa pili. Namshukuru Mungu nilitoka salama ila aliyekuwa kakaa siti ya pembeni yangu alifariki [emoji22][emoji22][emoji22]
 
Mbona waliopata ulemevu nao wamesimulia humu.. Au leo umeamka vibaya?
 
Hamna hata aliyefariki humu?
Wote mlipona duh
Poleni sana kwa yaliyowakuta
Mimi ajali pekee niliyopata ni kujikwaa na kujikata kidole cha mguu mbaka leo kidole changu cha mguu kipo nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…