Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

Nikiwa nimeachowa nyumba na wadogo zangu wazee walikuwa wameenda msiban. niIiwasikia mapema wakiwa huko nje nikaenda kujibanza nyuma ya mlango nikafungua komeo taratiibu. Ile wanahesabu 1, 2,3 nikafungua mlango paap jiwe likapitiliza. Aisee walikimbia balaa.
Chai

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka 2012 nikiwa na rafki angu tulipewa mtaji na mwl wetu wa sekondari baada ya kuhitimu kidato cha nne,,Basi tulianza biashara ya kununua samaki.
Siku moja majira ya saa nane usku tulitoka ziwan na samaki wengi karbia wa laki sita tumefunga kwenye baiskel zetu kila mmoja,
Gafla tulikula fimbo,,ngumi na mapanga kumbe ni majambazi tulipigwa sawa sawa aisee sitasahau
 
Mimi nakumbuka miaka ya nyuma nimemaliza kidato cha sita, nimetoka kwenye mishe zangu usiku saa tisa, halafu napita eneo la makaburini. Ghafla kwa mbali nikawa nasikia harufu ya moshi wa sigara mchanganyiko na bangi, kucheki naona kundi la watu wanapuliza wamekaa juu ya makaburi. Kipindi hicho watu walikuwa wanapigwa sana na nondo, na wiki kadhaa nyuma kuna jirani yetu aliuawawa. Kurudi nilikotoka njia ni ndefu mno, na kwenda mbele lazima yale manjemba yangenifanya kitu mbaya.

Ile akili sijui hata ilitoka wapi, sijui ni mihadarati. Nilichofanya ni kuvua nguo zote na kuzishika kwa nyuma halafu nikaanza kuelekea usawa wao, niko uchi wa mnyama. Uzuri kulikuwa na mbalamwezi. Jamaa walivyoniona wakaanza kuuliza kwa mbali, wee nani. Mimi kimya nasonga mbele tu, ile kunisogelea na marungu yao na kuniona vizuri kuwa niko uchi, jamaa walipigwa na ganzi. Kilichofuata ni kutukana na kuanza kukimbia vibaya mno kila mtu njia yake.

Kila nikikumbuka huwa najionea sana huruma na kuwaza endapo kama yale manjemba yasingekimbia.
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.......
Mkuu we kiboko aisee
 
Mi nlipoona wanahangaika na mlango, nikalala chini huku nau'face mlango.kimyaaa!! tuliii!!
ile wamefanikiwa tu..nikaanza kuimba nao za kichwa tu
Ni za kichwa tu hamna vurugu
 
Mimi nakumbuka miaka ya nyuma nimemaliza kidato cha sita, nimetoka kwenye mishe zangu usiku saa tisa, halafu napita eneo la makaburini. Ghafla kwa mbali nikawa nasikia harufu ya moshi wa sigara mchanganyiko na bangi, kucheki naona kundi la watu wanapuliza wamekaa juu ya makaburi. Kipindi hicho watu walikuwa wanapigwa sana na nondo, na wiki kadhaa nyuma kuna jirani yetu aliuawawa. Kurudi nilikotoka njia ni ndefu mno, na kwenda mbele lazima yale manjemba yangenifanya kitu mbaya.

Ile akili sijui hata ilitoka wapi, sijui ni mihadarati. Nilichofanya ni kuvua nguo zote na kuzishika kwa nyuma halafu nikaanza kuelekea usawa wao, niko uchi wa mnyama. Uzuri kulikuwa na mbalamwezi. Jamaa walivyoniona wakaanza kuuliza kwa mbali, wee nani. Mimi kimya nasonga mbele tu, ile kunisogelea na marungu yao na kuniona vizuri kuwa niko uchi, jamaa walipigwa na ganzi. Kilichofuata ni kutukana na kuanza kukimbia vibaya mno kila mtu njia yake.

Kila nikikumbuka huwa najionea sana huruma na kuwaza endapo kama yale manjemba yasingekimbia.
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.......
Ukatembea ukuni nje bro
 
L

Eeeeh pole sana man.....mim walitakaga kunivamia nipo maskani peke nyeke kina maza wamekwenda mkoa acha kabisa klichonisaidia lile geti dogo la mlangoni lilikua imara hapo ndani nishajikojolea nishalia nishaomba Mungu nampgia maza cm hata hapokei
Kuna jirani yetu mmja alikua ni tajiri mtaa mzima alisikia kelele basi bn alipiga risasi mbili sijui ni baruti zile uwanjani kwake wahuni wote wakatoka mkuku
Baada ya muda ndio majirani wanasogea hapo nishalia kama zombie wakaja majirani wengine kurekebisha rekebisha getini wakabaki wawili mmja wa kike mwingine brother hivi akalala na panga hapo ndani

Ya pili ilitokea nikiwa na sister angu yani milango ya home kwetu nahisi ni ya mkoloni miguu balaa
Tumelala usiku sa tisa mara tunasikia mlango wa sebuleni na mlango wa jikoni unagongwa kwa nguvu na kutikiswa sister angu akaniamsha vaa suruali nkavaa a buti chini yani wakiingia ndani nashawaza kabisa hapo ntakimbia kama chizi hadi nyumbani kwa Diwani basi sister angu alikua na Bwana ake mwarabu mmja mgumu kinoma kwanza anaendesha Subaru yule msela akatoka ndani na wenzie kama kumi na usher nilijiuliza sana hawa waarabu hapo ndani wanalala vip maan sio kwa idadi hyo.........Mwizi mmja alikamatwa walichomfanya wakaenda mchomea moto katikati ya barabara polisi tunawapgia simu wanasema ety mmalizieni kabisa walikuja kubeba nyama choma
Waarabu walitokea wapi vile
 
Back
Top Bottom