Tuliozaa nje ya ndoa tukutane hapa, tujadili changamoto tunazokutana nazo

Sasa hivi kuna mwingine tena anasema anataka azae amekaa sana kusubiri kuolewa haoni sasa na pln huyu akijifungua huyu nae abebe mimba nyingine dhambi ni kukataa mtoto tu ila kama unakubali na iko wazi kitanda hakizai halamu ...twende kazi
Muhimu kwa kila mwanamke wa nje usizae nae zaidi ya mtoto mmoja; vinginevyo atataka kulimiliki jimbo.​
 
Kuna baba yetu mkubwa kwenye ukoo. Watoto huwa wanamtafuta wenyewe wameshakuwa na wengine kuoa ama kuolewa na anakuwa kasha wasahau wamama alio watia mimba. Jibu lake huwa ni moja tu kama alikuambia mimi ndo baba yako ni sawa mimi mama yangu hadi anafariki hakuwahi kuniambia baba yako ni yupi. Hajawahi kataa mtoto
 
Ndani 2 (Ke + Ke)

Nje 2 (Me + Ke)

Diaspora 1 (Ke)

Hata kama nitakufa leo, basi nitakuwa nimetimiza agano la kuzaa na kuijaza dunia.
Hakuna namna mkuu, wakati mwingine kuwa mbali na familia inachangia hii kutokea
 
Chukulia hao wanawake wangekuwa ni uwekezaji umefanya, halafu geuza story yako yote ikae kwenye mfumo huu halafu utupe majibu
Huo ni uwekezaji, hao watoto nitawahitaji sana katika uzee wangu, ata kwa kunipikia chai.
 
Kuna kipindi nilidhamiria kuwa na mtoto/watoto nje ya ndoa. Yule mwanamke anaringa sana, hata sasa nadhani bado anaringa sana. Nilivyoona mambo yatakuwa mengi nikaahirisha hadi leo wazo langu limekufa na halifufuki tena.

My love Atoto umeshalala?
Ikitokea ukawa mbali na familia kikazi, inaweza kupelekea hii hali ya kuwa na watoto nje.
 
Ukiwakutanisha sasa hivi, inaweza kuleta mgogoro kwenye ndoa
 
Unajua mkuu, tunachepuka kwa sababu nyumbani kuna utulivu; kukishakuwa na migogoro nyumbani inaweza kupelekea kuwa na athari mbali mbali,ikiwemo uchumi, kiakili n.k
Ni bora kuwa kimya kwanza huku tukisoma mazingira.​
 
Haitakiwi kukataa mtoto
 
Pumba tupu
 
Sidhani mkuu. Maana kwanza hao mama zao hata mimi hawakutaka nijue kwamba wale ni wanangu, sema tu mimi kuna "features" nikiziona kwa mtoto najua tu hili lakwangu 😀
Ulianzishaje mahusiano na hao wamama tupe experience!!?

Je hao wamama ni wazuri? Wana mvuto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…