Tuliozaa nje ya ndoa tukutane hapa, tujadili changamoto tunazokutana nazo

Tuliozaa nje ya ndoa tukutane hapa, tujadili changamoto tunazokutana nazo

Sasa hivi kuna mwingine tena anasema anataka azae amekaa sana kusubiri kuolewa haoni sasa na pln huyu akijifungua huyu nae abebe mimba nyingine dhambi ni kukataa mtoto tu ila kama unakubali na iko wazi kitanda hakizai halamu ...twende kazi
Muhimu kwa kila mwanamke wa nje usizae nae zaidi ya mtoto mmoja; vinginevyo atataka kulimiliki jimbo.​
 
Kuna baba yetu mkubwa kwenye ukoo. Watoto huwa wanamtafuta wenyewe wameshakuwa na wengine kuoa ama kuolewa na anakuwa kasha wasahau wamama alio watia mimba. Jibu lake huwa ni moja tu kama alikuambia mimi ndo baba yako ni sawa mimi mama yangu hadi anafariki hakuwahi kuniambia baba yako ni yupi. Hajawahi kataa mtoto
 
Umesahau kusema watoto wengine wapo kwenye ndoa za mama zao. Ile ya kitanda hakizai haramu
ha ha ha
dna.jpg
 
Ndani 2 (Ke + Ke)

Nje 2 (Me + Ke)

Diaspora 1 (Ke)

Hata kama nitakufa leo, basi nitakuwa nimetimiza agano la kuzaa na kuijaza dunia.
Hakuna namna mkuu, wakati mwingine kuwa mbali na familia inachangia hii kutokea
 
Chukulia hao wanawake wangekuwa ni uwekezaji umefanya, halafu geuza story yako yote ikae kwenye mfumo huu halafu utupe majibu
Huo ni uwekezaji, hao watoto nitawahitaji sana katika uzee wangu, ata kwa kunipikia chai.
 
Kuna kipindi nilidhamiria kuwa na mtoto/watoto nje ya ndoa. Yule mwanamke anaringa sana, hata sasa nadhani bado anaringa sana. Nilivyoona mambo yatakuwa mengi nikaahirisha hadi leo wazo langu limekufa na halifufuki tena.

My love Atoto umeshalala?
Ikitokea ukawa mbali na familia kikazi, inaweza kupelekea hii hali ya kuwa na watoto nje.
 
Kuzaa ni baraka, nawashanga na namshngaa mleta uzi, eti kuzaa nje ya ndoa! Unamfahamu Suleman wa Biblia? Unamfahamu uzao wa Yuda, unayosikia mfalme wa Yuda, kizazi cha Yesu mwenyewe, kwa ulokole wenu, mnaweza sema ni dhambi tupu! Hakuna dhambi kwenye kuzaa! Zaa tunza watoto.

Unachokosea ni kutowaunganisha watoto wajuane wakiwa wadogo! Wachangamane! Bila hivyo huko mbeleni, linaweza kukufadhaisha sana.
Ukiwakutanisha sasa hivi, inaweza kuleta mgogoro kwenye ndoa
 
Bado logic ya kumficha mkeo siioni.
Ujue nini mkuu, hao watoto ni damu yako, sasa unapoficha ficha ni kwamba unamgwaya mkeo atakutenga?
Hatuna mwamana na Sir god kuhusu kifo.
Likitokea hilo huwaga kuna fujo sana kwenye misiba ya washikaji, ama hao watoto kutotambuliwa kuwa ni wa kwako. Jitahidi sana kiongozi.
Unajua mkuu, tunachepuka kwa sababu nyumbani kuna utulivu; kukishakuwa na migogoro nyumbani inaweza kupelekea kuwa na athari mbali mbali,ikiwemo uchumi, kiakili n.k
Ni bora kuwa kimya kwanza huku tukisoma mazingira.​
 
Kuna baba yetu mkubwa kwenye ukoo. Watoto huwa wanamtafuta wenyewe wameshakuwa na wengine kuoa ama kuolewa na anakuwa kasha wasahau wamama alio watia mimba. Jibu lake huwa ni moja tu kama alikuambia mimi ndo baba yako ni sawa mimi mama yangu hadi anafariki hakuwahi kuniambia baba yako ni yupi. Hajawahi kataa mtoto
Haitakiwi kukataa mtoto
 
Katika ujana wangu, nilikuwa mlafi sana; nilikuwa nikiona tu pisi kali inayoshawishi na kuuteka moyo wangu, nitaanzisha naye mahusiano na hatimaye tunajikuta tayari tuna mtoto; ingawa tangu mwanzoni huwa nawaambia mimi ni mme wa mtu,lakini wao hawajali.

Hii imenipelekea kuwa na watoto 6 nje, kila mmoja na mama yake; wapo walimbwende walionizidi urefu, wengine wana viuno vya nyugwi (umbo namba 8) n.k;

Kutokana na uzuri wao, nilikuwa natumia gharama kubwa angalau niweke alama ya mtoto, ili huko mbeleni iwe rahisi kupasha kiporo pale ninapohitaji.

Changamoto ninazokutana nazo:-​
  • Hawa wazazi kutaka tuendelee kula bata kama nilipokuwa kijana, wakati sasa na uzee wangu huu majukumu yameniandama na kuamua kupunguza baadhi ya starehe. Hii imepelekea wengine kuvunja mawasiliano na mimi; ingawa najua huko mbeleni watoto wakikua watanitafuta.​
  • Wengine wanataka wapindue ndoa ili wao watambulike kama mke, bahati nzuri hilo nimeweza kulidhibiti (hapa nimeweza kuwazidi wavamizi wa M23).​
  • Wengine kuzidisha bili kwenye mahitaji ya mtoto, lakini hili pia nimeweza kulidhibiti.​

Mafanikio:-​
  • Bi mkubwa hajui kama nina watoto nje; na hii nataka iwe siri mpaka hao watoto wote wawe sekondari nasi tukiwa kwenye umri wa busara ndio tuweze kuzungumza.​
  • Nategemea huko mbeleni nikiwa mzee sana, nitakuwa nimezungukwa na vijana wangu wasiopungua 11.​
  • Kupata huduma ya tendo iwapo mmoja wapo ataamua kuzingua.​

Karibuni kwa uzoefu​
Pumba tupu
 
Sidhani mkuu. Maana kwanza hao mama zao hata mimi hawakutaka nijue kwamba wale ni wanangu, sema tu mimi kuna "features" nikiziona kwa mtoto najua tu hili lakwangu 😀
Ulianzishaje mahusiano na hao wamama tupe experience!!?

Je hao wamama ni wazuri? Wana mvuto?
 
Back
Top Bottom