Tuliposema Emmanuel Nchimbi hana Ushawishi tulipuuzwa, Sasa angalia hii

Hakuna utaratibu kama huo kwenye ajira wa mimi kwenda kwa lazima kwenye mkutano wa katibu mkuu wa CCM tena siku ya Jumamosi. mmewakuta maboya ndio mnawapelekesha hivyo, yeye afanye vikao na hao wajuu HRO huko.
 
Hakuna kitu kama hicho kwenye standing order, labbda kama hujui maana ya majukumu mengine utakayopangiwa. Huwezi nilazimisha kwenda kwenye mkutano wa kiongozi wa chama cha siasa ambacho mimi siwajibiki kwake moja kwa moja kama mwajiriwa. Hizo sheria sijui mnazisomea wapi.
Umeajiriwa kama mtu wa IT alafu bosi anakupa jukumu la kumuandalia chai, na wewe unakubali kwa sababu ni mojawapo ya majukumu mengine!!! utakuwa mpumbavu wa kiwango cha juu sana.
 
wakuu wa idara wachukue mahudhurio🤣🤣🤣🤣🤣 bora ukafugr kondoo ujue moja yaani unakuta baba mwenye watoto naye anahesabishwa namba 🤣🤣🤣🤣
Huwezi fukuzwa kazi kwa sababu kama hiyo, sana sana utakuwa unafanyiwa figisu za chini kwa chini. Haya mambo wala hayajaanza leo, hata miaka 20 iliyopita yalikuwepo na sijawahi kufanya huo ujinga. Hata Mei mosi kuna waajiri walikuwa na tabia ya kuchukua maudhurio na sijawahi kwenda, plus mikusanyiko ya mwenge.
 
Akague na pimbi wenzake,yeye hanilipi mshahara,sina muda wa kusikiza vilaza
Ujinga ulinifundisha weww
 
Akague na pimbi wenzake,yeye hanilipi mshahara,sina muda wa kusikiza vilaza
Ujinga ulinifundisha weww
Ukiwa seerikalini ukipenda usipenda unafanya kazi kwa kutelekeza ilani na sera za chama tawala, si unakifahamu chama tawala?

CCM ndiyo inayodhibiti pesa zote za serikali zinazotumika nchi hii, pamoja na unazolipwa wewe, kumbuka hilo.
 
Hakuna tatizo hapo! Watumishi wa umma ni watekelezaji wa Ilani ya Chama kilichoko madarakani so lazima wakasikilize mwenye Ilani.

Wao ni watumishi wa serikali ya CCM. Kumbuka lengo namba moja la Chama chochote cha siasa ni kushika dola na pili ni kuunda serikali so hap ni watumishi kwenye serikali ya CCM waende wasikie mwenye duka anasemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…