Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Mkuu unaongea nadharia mlizofundishwa pale Mikocheni.JPM hakuvurunda. Nina hisi wengi hampo karibu na habari. Mara kadhaa alikuwa anawakanya TRA wawe wastaarabu. Uzuri mimi Tax pia ni field yangu. Tax ni Sheria na Imetungwa na Bunge. Hata Rais hawezi ipangua mpaka iende Bungeni. Tatizo la TRA ni kutoa elimu kwa mlipa kodi na pia kuto kuwa rational katika kufanya maamuzi. Unaweza kuta wanakataa kitu ambacho mbele ya macho ni cha ukweli. Lakini pia ukionewa kwenye kodi unatakiwa kufanya pingamizi ndani ya siku therathini au zaidi. Ni sheria haibadiliki kirahisi mpaka bunge liseme. TRA wawaelimishe watu. Wafanyabiashara wanaotumia wahasibu wabobezi ya tax consultants kwao kuna unafuu maana TRA na hawa wataalamu huzungumza lugha moja.
Unyang’anyi mkubwa umefanyika hasa miaka hii miwili au mitatu.
Task Force za mitutu ambazo zilikuwa na afisa Usalama, TRA na polisi, nani alizianzisha?
Kufunga account na kuchota fedha nani alianzisha?
Kubambika watu kesi za uhujumu uchumi, na kkuwaachia wafanya biashara baada ya kukubali na kusign kuachia fedha yote au kiasi, nani kazianzisha?
Haya yote yanafanyika na TRA?
Inabidi ukweli usemwe ili tusahihishe.