Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Nilidhani unajibu hoja za kisheria za Lissu juu ya mgombea wenu kumbe tunasumbuliwa na supu ya utumbo baada ya kupokea buku saba Lumumba
Lissu ana hoja gani kwa mfano?? Lissu anayejiita Wakili msomi ambae inatakiwa awe mfano kwa kuheshimu mahakama sehemu ambayo ni kama ofisi yake sehemu ambayo sheria zinapata tafsiri yeye ndo amekuwa mvunja sheria mkubwa na mdharau mahakama ngoja uchaguzi uishe aje ajibu kesi zake za Jinai
 
Mimi nikajua wagombea wote ni wa tume,kumbe kuna wa tume na wasio wa tume
 
Sasa kinachokuliza nini ?
 
Nakujibu

Mosi sio kuleta drama bali ni kusimamia sheria inavyosema na kama umekiuka sheria maana yake umetenda kosa na hilo kosa lina adhabu ambayo ni kukatwa na kama sio kosa basi hakuna adhabu kuna msemo wa kilatini unasema nulla poena sine lege yaani hakuna sheria hakuna kosa hivyo basi kama sheria ya uchaguzi imesema ni kosa basi kosa hilo litolewe adhabu.

Lissu mwenyewe ndiye aliyeona zimepigwa upande mmoja otherwise zilete na sisi tuzione sio kweli kwamba hakuna sheria ya passport ipo inaitwa 'Tanzania passports and travel documents act cap 42'.

picha za passport hicho ni kiingereza kiswahili chake ni kwamba wagombea walete picha yenye ukubwa wa picha ikiyo/inayofanana kwenye hati ya kusafiria.

Mimi nasema huwezi kupiga picha ya kuweka kwenye hati ya kusafiria ikiwa iko upande ni lazima macho yaonekane yote na masikio yaonekane yote.
 
K
Kwani Magufuli, Lipumba na Lissu walirudisha fomu siku tofauti? mbona sisi sote tuliuatilia na tunajua kwamba fomu za wagombea wote zilirudishwa siku moja? au siku hizi tumejitoa akili tunamsubiri Lissu aseme ndo tudandie?

Kama ni uhakiki wa fomu za wagombea pale Tume, kwa nini Lissu alikuwa analalamika kwamba kawekwa muda mrefu kusubiri uhakiki wa fomu lkn Magufuli yeye hakuchelewa na vyama vingine pia havikuchelewa ilhali akijua kwamba zinapaswa kuhakikiwa na tume? Lissu asubiri sanduku la kura litaamua nani Rais tumtakaye
 

Narudia tena, huu mchezo wa wagombea wa ccm kupita bila kupingwa ni tabia binafsi ya Magufuli toka akiwa mbunge. Toka ameingia madarakani ndio imekuwa mbinu kuu ya ccm kutangazwa washindi bila kushindana.

Kama kweli lengo ni mgombea kupita kwa ridhaa ya wananchi, iweje uchaguzi wa SM 70%+ ya wagombea wa ccm walitangazwa washindi kwa kuwaengua wapinzani kwa sababu ndogondogo hivyo?

Hao tume wametangaza kuwa hakuna mtu amepita bila kupingwa, maana wameona wanaccm pia wamewekwa mapingamizi yanayofanana na sababu zilizowatoa wapinzani.
 
Kutokana na pingamizi alilopeleka Lissu kutupiliwa mbali na NEC, hii inaonyesha jinsi gani anaanza kugaragazwa mapemaa october
 

Attachments

  • Screenshot_20200827-112251.png
    105.9 KB · Views: 1
Amsterdam akija Kwanza karantini siku 14, zikiisha yuko positive
 
Msikilize vizuri Lisu alisema JPM hakurudisha form Kama sheria za uchaguzi zinavyosema unaweza ukamwona mtu ndani ya dakika 30 Kama ulivyosema ila hakukidhi vigezo vilivyotakiwa kwa maana hiyo hajarudisha form.
Nimekuelewa ila naomba tusijaribu kufikirishwa na hawa wana siasa bali tuwe tuna fikiri wenyewe kulingana na facts zilizopo'
 
Zero kabisa wewe!Picha aliyoweka haikuwa sahihi na ni zile picha zilizoko kwenye mabango yake humu mitaani.
Kwa hiyo siyo picha zake kabisaa? Hazimtambulishi si ndiyo?

Kapimwe akili kama Don Nalimison kisha tuje kudebate hapa
 
Ewe mungu, Tumemvumilia Magufuli kwa miaka 5 kwa shida na tabu nyingi sana tulizozikabili, Nakuomba Usituletee tena kwa Miaka mitano ijayo,Tutaangamia kwa mwendo aliokwenda nao. Bali mapenzi yako yatimizwe hata kama ni kumpumzisha kwa amani ili aje Yulee atakaye tuhurumia na kutuenzi kama raia tulio huru katika nchi huru.
Amin

Ewe Mola ,Umeziona Hila na vitimbwi tunavyofanyiwa wapinzani, iIlhali wewe ni Mungu mwenye kuona na Kusikia. Tuhurumie sisi wanyonge na ututetee vile unavyoona wewe inafaa. Hakika wewe umeahidi Kuwa ''Dhalimu hachumi ila Hasira yako na hasara yake ya milele'' Basi Mungu Mkuu Twakuomba waja wako wanyonge,sisi hatuwezi ,lakni Wewe watutosha.

Amin.
Ewe Mungu, Tazama Pemba ,Tazama Mtwara, tazama Tanga, Tazama Morogoro, Tazama Lindi.tazama Tanzania kila pembe, watu wako wanavyotendewa.

Hivi hizi taratibu na sheria si wamepanga CCM wenyewe? Mbona wanazikiuka kwa woga,? wakamate wanafiki hawa wasiofanya uadilifu. Kwani wewe ni Muadilifu

Ni nani basi awezaye toka mikononi mwako pale utakapomshika? Nyoosha Mikono yako yenye Nguvu uwadhibiti mafedhulu wale wanaowadhalilisha watu wako.

Tusamehe kwa udhaifu wa matende yetu, lakini tutetee kwa maduizetu, kuwani sisi ni waja wako usiwaache CCM watuangamize.
Amin
 

Nimependa hoja yako hiyo inahitimisha matakwa ya WaTz
 
Clouds imefungiwa kwa kusema uwongo huo wa kupita bila kupingwa kabla tume haijafanya uamuzi wake. Ni watu kama wewe ndio mnaoeneza hayo ya wabunge wa CCM kupita bila kupingwa kabla facts hazijatoka
 
Clouds imefungiwa kwa kusema uwongo huo wa kupita bila kupingwa kabla tume haija fanay uamauzi wake. Ni watu kama wewe ndio mnaoeneza hayo ya wabunge wa CCM kupita bila kupingwa kabla facts hazitjatoka

Waliotangaza ni wakurugenzi wa uchaguzi ambao ni maafisa wa tume kisheria. Hao clouds wametangaza baada ya kusikia hao wakurugenzi. Haya yanayofanyika sasa ya kufungia vyombo vya habari, ni mambo ya kawaida kabisa kwenye nchi za kidictator na viashiria vyake. Msidhani hatujui kinachoendelea au labda ni jambo jipya sana. Ni jambo jipya hapa nchini, ila sio mambo mapya kwenye dunia hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…