Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Nilidhani unajibu hoja za kisheria za Lissu juu ya mgombea wenu kumbe tunasumbuliwa na supu ya utumbo baada ya kupokea buku saba Lumumba
Lissu ana hoja gani kwa mfano?? Lissu anayejiita Wakili msomi ambae inatakiwa awe mfano kwa kuheshimu mahakama sehemu ambayo ni kama ofisi yake sehemu ambayo sheria zinapata tafsiri yeye ndo amekuwa mvunja sheria mkubwa na mdharau mahakama ngoja uchaguzi uishe aje ajibu kesi zake za Jinai
 
Nawashauri Tume ya Uchaguzi wazungumze na Lissu na wahusiane naye kwa heshima, wakitaka kuendesha Uchaguzi kama Ndugai alivoendesha Bunge ama kama Magufuli anavoendesha Serikali bila kuzingatia Sheria za nchi watapata tabu sana..

Itafika siku ya Uchaguzi Tume wako hoi kwa sababu wataelezewa kuwa hawana Uadilifu wa kutosha kusimamia Uchaguzi, na Mgombea wa Tume pia ataelezewa kuwa Hana Uhalali wa Kisheria kushiriki Uchaguzi...

Yan kwenye Uchaguzi huu Mgombea wa Tume atakuwa kama Mwanafunzi anayehudhuria Lectures Chuo lakini Hana admission, au Basi ana admission lkn hajakamilisha Usajili...so anapoteza muda tu.

Hata akishinda Ushindi wake utapingwa mahakamani kuwa Hakuwa na Uhalali Kisheria kushiriki Uchaguzi, So ni Mgombea Fake.

Kufika Tarehe ya Uchaguzi Tume will be battered na Mgombea wa Tume atakuwa Rais dhaifu mno kiuhalali wa Mamlaka ya cheo chake Ikitokea akatangazwa kwa Lazima kuwa kashinda Urais, atakuwa kama Dr.Shwein katika Awamu yake ya 2.
Mimi nikajua wagombea wote ni wa tume,kumbe kuna wa tume na wasio wa tume
 
Lissu ana hoja gani kwa mfano?? Lissu anayejiita Wakili msomi ambae inatakiwa awe mfano kwa kuheshimu mahakama sehemu ambayo ni kama ofisi yake sehemu ambayo sheria zinapata tafsiri yeye ndo amekuwa mvunja sheria mkubwa na mdharau mahakama ngoja uchaguzi uishe aje ajibu kesi zake za Jinai
Sasa kinachokuliza nini ?
 
Nakujibu

Mosi sio kuleta drama bali ni kusimamia sheria inavyosema na kama umekiuka sheria maana yake umetenda kosa na hilo kosa lina adhabu ambayo ni kukatwa na kama sio kosa basi hakuna adhabu kuna msemo wa kilatini unasema nulla poena sine lege yaani hakuna sheria hakuna kosa hivyo basi kama sheria ya uchaguzi imesema ni kosa basi kosa hilo litolewe adhabu.

Lissu mwenyewe ndiye aliyeona zimepigwa upande mmoja otherwise zilete na sisi tuzione sio kweli kwamba hakuna sheria ya passport ipo inaitwa 'Tanzania passports and travel documents act cap 42'.

picha za passport hicho ni kiingereza kiswahili chake ni kwamba wagombea walete picha yenye ukubwa wa picha ikiyo/inayofanana kwenye hati ya kusafiria.

Mimi nasema huwezi kupiga picha ya kuweka kwenye hati ya kusafiria ikiwa iko upande ni lazima macho yaonekane yote na masikio yaonekane yote.
 
K
Wanazidi kutushangaza!Tungekuwa na Tume Huru, huenda Magu asingekuwa mgombea leo.

Kwa mujibu wa Lissu, Tume ndio iitoa maelezo yanayopingana na sheria, na mgombea uraisi Magufuli, akafuata maelekezo hayo yanayopingana na sheria, maelezo ambayo Lissu yeye alikataa kuyafuata na fomu zake akataka zikahakikiwa na NEC kama sheria inavyoelekeza(alisoma kifungu husika kwa wanahabari)...
Kwani Magufuli, Lipumba na Lissu walirudisha fomu siku tofauti? mbona sisi sote tuliuatilia na tunajua kwamba fomu za wagombea wote zilirudishwa siku moja? au siku hizi tumejitoa akili tunamsubiri Lissu aseme ndo tudandie?

Kama ni uhakiki wa fomu za wagombea pale Tume, kwa nini Lissu alikuwa analalamika kwamba kawekwa muda mrefu kusubiri uhakiki wa fomu lkn Magufuli yeye hakuchelewa na vyama vingine pia havikuchelewa ilhali akijua kwamba zinapaswa kuhakikiwa na tume? Lissu asubiri sanduku la kura litaamua nani Rais tumtakaye
 
Sijui kwa sababu hakuna ushahidi wa kuwa kuna wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa. Jana tume ya uchaguzi ilitahadharisha kuwa hakuna mgombea yeyote aliyekwisha pita bila kupingwa. Hata hivyo ikionekana wana CHADEMA wamazikosea sheria na kanuni hizo, basi sheria itachukua mkondo wake...

Narudia tena, huu mchezo wa wagombea wa ccm kupita bila kupingwa ni tabia binafsi ya Magufuli toka akiwa mbunge. Toka ameingia madarakani ndio imekuwa mbinu kuu ya ccm kutangazwa washindi bila kushindana.

Kama kweli lengo ni mgombea kupita kwa ridhaa ya wananchi, iweje uchaguzi wa SM 70%+ ya wagombea wa ccm walitangazwa washindi kwa kuwaengua wapinzani kwa sababu ndogondogo hivyo?

Hao tume wametangaza kuwa hakuna mtu amepita bila kupingwa, maana wameona wanaccm pia wamewekwa mapingamizi yanayofanana na sababu zilizowatoa wapinzani.
 
Kutokana na pingamizi alilopeleka Lissu kutupiliwa mbali na NEC, hii inaonyesha jinsi gani anaanza kugaragazwa mapemaa october
 

Attachments

  • Screenshot_20200827-112251.png
    Screenshot_20200827-112251.png
    105.9 KB · Views: 1
Hivi nikuulize tu kifupi rafiki
Akijaza fomu zingine usiku huu akaweka na kila kitu zikagongwa mihuri yote ya mahakama na tume kwa tarehe za nyuma na kwenda kubandika kwenye notisi bodi. Yeye Lisu akabaki na picha ya zamani ataitumia kama ushahidi?
Na unadhani itamsaidia?

Aanze kampeni aache kupoteza muda kwenda kwenye kesi la sivyo atanaswa mtegoni kupitia mbinu zake. Mwisho ziwe kesi za kimahakama halafu anze kupangwa kila baada ya siku mbili inasikilizwa au atawaleta Robert & Amstredam nao wanawekewa zengwe pia
Amsterdam akija Kwanza karantini siku 14, zikiisha yuko positive
 
Msikilize vizuri Lisu alisema JPM hakurudisha form Kama sheria za uchaguzi zinavyosema unaweza ukamwona mtu ndani ya dakika 30 Kama ulivyosema ila hakukidhi vigezo vilivyotakiwa kwa maana hiyo hajarudisha form.
Nimekuelewa ila naomba tusijaribu kufikirishwa na hawa wana siasa bali tuwe tuna fikiri wenyewe kulingana na facts zilizopo'
 
Zero kabisa wewe!Picha aliyoweka haikuwa sahihi na ni zile picha zilizoko kwenye mabango yake humu mitaani.
Kwa hiyo siyo picha zake kabisaa? Hazimtambulishi si ndiyo?

Kapimwe akili kama Don Nalimison kisha tuje kudebate hapa
 
Ewe mungu, Tumemvumilia Magufuli kwa miaka 5 kwa shida na tabu nyingi sana tulizozikabili, Nakuomba Usituletee tena kwa Miaka mitano ijayo,Tutaangamia kwa mwendo aliokwenda nao. Bali mapenzi yako yatimizwe hata kama ni kumpumzisha kwa amani ili aje Yulee atakaye tuhurumia na kutuenzi kama raia tulio huru katika nchi huru.
Amin

Ewe Mola ,Umeziona Hila na vitimbwi tunavyofanyiwa wapinzani, iIlhali wewe ni Mungu mwenye kuona na Kusikia. Tuhurumie sisi wanyonge na ututetee vile unavyoona wewe inafaa. Hakika wewe umeahidi Kuwa ''Dhalimu hachumi ila Hasira yako na hasara yake ya milele'' Basi Mungu Mkuu Twakuomba waja wako wanyonge,sisi hatuwezi ,lakni Wewe watutosha.

Amin.
Ewe Mungu, Tazama Pemba ,Tazama Mtwara, tazama Tanga, Tazama Morogoro, Tazama Lindi.tazama Tanzania kila pembe, watu wako wanavyotendewa.

Hivi hizi taratibu na sheria si wamepanga CCM wenyewe? Mbona wanazikiuka kwa woga,? wakamate wanafiki hawa wasiofanya uadilifu. Kwani wewe ni Muadilifu

Ni nani basi awezaye toka mikononi mwako pale utakapomshika? Nyoosha Mikono yako yenye Nguvu uwadhibiti mafedhulu wale wanaowadhalilisha watu wako.

Tusamehe kwa udhaifu wa matende yetu, lakini tutetee kwa maduizetu, kuwani sisi ni waja wako usiwaache CCM watuangamize.
Amin
 
...
Sitaki kuamini CCM ni borq zaidi au hatuwezi kusonga zaidi bila wao kua madarakani HAPANA mabadiliko ni lazima yawepo lkn hao wanaotaka hayo mabadiliko wanatuaminishaje kwamba na wao Upinzani ni watu sahihi?????????!!!!!!!!! Hayo ni mawazo yangu binafsi nami naishi hapa hapa Tanzania na kila siku naona na kusikia kinachiendelea hapa kwetu JMT.

Nimependa hoja yako hiyo inahitimisha matakwa ya WaTz
 
Narudia tena, huu mchezo wa wagombea wa ccm kupita bila kupingwa ni tabia binafsi ya Magufuli toka akiwa mbunge. Toka ameingia madarakani ndio imekuwa mbinu kuu ya ccm kutangazwa washindi bila kushindana. Kama kweli lengo ni mgombea kupita kwa ridhaa ya wananchi, iweje uchaguzi wa SM 70%+ ya wagombea wa ccm walitangazwa washindi kwa kuwaengua wapinzani kwa sababu ndogondogo hivyo? Hao tume wametangaza kuwa hakuna mtu amepita bila kupingwa, maana wameona wanaccm pia wamewekwa mapingamizi yanayofanana na sababu zilizowatoa wapinzani.
Clouds imefungiwa kwa kusema uwongo huo wa kupita bila kupingwa kabla tume haijafanya uamuzi wake. Ni watu kama wewe ndio mnaoeneza hayo ya wabunge wa CCM kupita bila kupingwa kabla facts hazijatoka
 
Clouds imefungiwa kwa kusema uwongo huo wa kupita bila kupingwa kabla tume haija fanay uamauzi wake. Ni watu kama wewe ndio mnaoeneza hayo ya wabunge wa CCM kupita bila kupingwa kabla facts hazitjatoka

Waliotangaza ni wakurugenzi wa uchaguzi ambao ni maafisa wa tume kisheria. Hao clouds wametangaza baada ya kusikia hao wakurugenzi. Haya yanayofanyika sasa ya kufungia vyombo vya habari, ni mambo ya kawaida kabisa kwenye nchi za kidictator na viashiria vyake. Msidhani hatujui kinachoendelea au labda ni jambo jipya sana. Ni jambo jipya hapa nchini, ila sio mambo mapya kwenye dunia hii.
 
Back
Top Bottom