HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 722
- 971
kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri ni kitu ambacho hakina logic. Mambo ya umri wa uraisi sio màmuzi mazito kwan lilikuwepo hata kwenye katiba ya sasa. Mambo ya msingi na mazito ni kuhusu mamlaka ya urais kama taasisi na sio mtu, watueleze matumizi ya rasilimali zetu, muundo na uendeshaji wa muungano, uhuru, haki na wajibu wa raia wetu, mipaka ya uwajibikaji katika taasisi za kiserikali, itikadi na falsafa ya taifa letu na pia muundo na muingiliano wa nguzo kuu za dola. Hatutaki porojo.
Kuna watu humu hata hawaelewi theories wala mifumo ya governance duniani ilivyo, wanataka waibue yao wao tu wanavyoona. Hili jukwaa sasa linaanza kuharibika kwa kweli, hakuna hoja tena ni utani, kejeli na maudhi tu. Michango ya kitoto imetawala jukwaa sasa, basi ni aibu tupu...
Hapo kwenye tanganyika nimepapenda
Ardhi inayotumika iwe mali ya mtumiaji na isiyotumika ndo iwe mali ya Taifa
Tume ya Katiba inayoongozwa
na Jaji Joseph Warioba inatarajiwa kutoa Rasimu ya Katiba kuanzia kesho
Jumatatu.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya tume hiyo zinasema wajumbe wa tume
hiyo wameamua kuweka itikadi za vyama pembeni na kuibuka na rasimu ya
Katiba yenye mambo mazito na makubwa.
Kati ya yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ni Uanzishwaji wa Serikali ya
Tanganyika,Tume huru ya uchaguzi na pia kupiga marufuku wabunge kuwa
mawaziri.Pia tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia
miaka 40.
Wachambuzi wa mambo wanasema haya yatakuwa ni maamuzi magumu na mazito
yamefanywa na tume na pia itakuwa imeondoa kabisa uwezekano wa Chama cha
CHADEMA kuongoza watanzania kuipinga katiba hiyo kama walivyokuwa
wameahidi awali.
Source: Tanzania Daima Jumapili UK. 2
inawezekana kwani nakumbuka siku moja nilibabahatika kukutana na Prof Baregu, baada ya kuongea nae alinihakikishia kuwa katiba itakuwa bomba wananchi wasubiri, kweli ngoja tusubiri!
Mkuu mimi sio mtaalamu wa mambo ya katiba ila ninavyojua ideology ni suala la kichama zaidi kuliko la Katiba ya Nchi. Pamoja na Katiba ya nchi kuwa ndio msingi mkuu na sheria mama ya uendeshaji wa nchi, bado kwa kiasi kikubwa nchi huathiriwa na ideology ya chama kilichoko madarakani.
Kuna watu humu hata hawaelewi theories wala mifumo ya governance duniani ilivyo, wanataka waibue yao wao tu wanavyoona.
Tanganyika ni "Yeltsin" wa Muungano! Time will tell!
Aiseee! Ngoja tusubiri, Kinana kawaruhusu? Na fastjet a.k.a msaidia mateja wenye macho mlegezo, paja zenye tattoo na kiuno chembamba NA siyo akina Ngwair?