Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Status
Not open for further replies.
Kuna watu humu hata hawaelewi theories wala mifumo ya governance duniani ilivyo, wanataka waibue yao wao tu wanavyoona. Hili jukwaa sasa linaanza kuharibika kwa kweli, hakuna hoja tena ni utani, kejeli na maudhi tu. Michango ya kitoto imetawala jukwaa sasa, basi ni aibu tupu...
 
Kweli haya nayaunga mkono pia.
kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri ni kitu ambacho hakina logic. Mambo ya umri wa uraisi sio màmuzi mazito kwan lilikuwepo hata kwenye katiba ya sasa. Mambo ya msingi na mazito ni kuhusu mamlaka ya urais kama taasisi na sio mtu, watueleze matumizi ya rasilimali zetu, muundo na uendeshaji wa muungano, uhuru, haki na wajibu wa raia wetu, mipaka ya uwajibikaji katika taasisi za kiserikali, itikadi na falsafa ya taifa letu na pia muundo na muingiliano wa nguzo kuu za dola. Hatutaki porojo.
 
Kuna watu humu hata hawaelewi theories wala mifumo ya governance duniani ilivyo, wanataka waibue yao wao tu wanavyoona. Hili jukwaa sasa linaanza kuharibika kwa kweli, hakuna hoja tena ni utani, kejeli na maudhi tu. Michango ya kitoto imetawala jukwaa sasa, basi ni aibu tupu...

Kaka yangu Hk, nisaidie ni theory ipi ya governance unaona inatoa nafasi zaidi kwa mihimili yote mitatu kusimamiana vyema?
 
Aisee, hii nimeipenda, namuaminia sana mkuu Molemo,,,
 
Kama kuna kitu tume itafanya niisifu basi ni kufuta nafasi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya. Second ni kufuta mbunge kuwa waziri.

Mkuu captain kesho sii mbali tusubiri tuione rasimu yote ya katiba.
 
Last edited by a moderator:
Aisee, hii nimeipenda, namuaminia sana mkuu Molemo,,,

Mkuu Fekifeki hii habari imeripotiwa na gazeti makini la Tanzania Daima.Na limesema hii habari ni ya kuaminika kutoka ndani ya Tume.Rasimu yote ya Katiba itakuwa hadharani kesho.
 
Last edited by a moderator:
Tume ya Katiba inayoongozwa
na Jaji Joseph Warioba inatarajiwa kutoa Rasimu ya Katiba kuanzia kesho
Jumatatu.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya tume hiyo zinasema wajumbe wa tume
hiyo wameamua kuweka itikadi za vyama pembeni na kuibuka na rasimu ya
Katiba yenye mambo mazito na makubwa.

Kati ya yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ni Uanzishwaji wa Serikali ya
Tanganyika,Tume huru ya uchaguzi na pia kupiga marufuku wabunge kuwa
mawaziri.Pia tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia
miaka 40.

Wachambuzi wa mambo wanasema haya yatakuwa ni maamuzi magumu na mazito
yamefanywa na tume na pia itakuwa imeondoa kabisa uwezekano wa Chama cha
CHADEMA kuongoza watanzania kuipinga katiba hiyo kama walivyokuwa
wameahidi awali.

Source: Tanzania Daima Jumapili UK. 2

inawezekana kwani nakumbuka siku moja nilibabahatika kukutana na Prof Baregu, baada ya kuongea nae alinihakikishia kuwa katiba itakuwa bomba wananchi wasubiri, kweli ngoja tusubiri!
 
inawezekana kwani nakumbuka siku moja nilibabahatika kukutana na Prof Baregu, baada ya kuongea nae alinihakikishia kuwa katiba itakuwa bomba wananchi wasubiri, kweli ngoja tusubiri!

Wazee hawa wameona haina maana kuendekeza itikadi huku Taifa likiangamia.
 
Mkuu mimi sio mtaalamu wa mambo ya katiba ila ninavyojua ideology ni suala la kichama zaidi kuliko la Katiba ya Nchi. Pamoja na Katiba ya nchi kuwa ndio msingi mkuu na sheria mama ya uendeshaji wa nchi, bado kwa kiasi kikubwa nchi huathiriwa na ideology ya chama kilichoko madarakani.

Chifu, hata mimi siyo mtaalamu wa mambo ya katiba; ila kwa hayo uliyoyaandika naweza kuchangia kidogo.

Nichukulie mfano wa UK: chama kinachoongoza serikali ni Conservative chini ya David. Ideology za conservatives naamini unazimanya. Ni kinyume na liberals. Lakini sasa, ikaja tokea kiongozi wa chama ambaye ni kiongozi mkuu wa serikali, akasapoti mitazamo ya liberals katika suala la LGBT!

Sasa hapo utasemaje?

Mwisho, mimi naamini ni vyema taifa likawa na itikadi; itikadi ndiyo inatoa msingi wa masuala mazima ya kiuchumi, kijamii na kimaendeleo kwa ujumla.

Nipo tayari kukoselewa; ila hilo ndilo naona linafaa.
 
kama ni hivyo basi hakuna kupiga kura imepita.
 
Kuna watu humu hata hawaelewi theories wala mifumo ya governance duniani ilivyo, wanataka waibue yao wao tu wanavyoona.

Chifu, ebu nisaidie hiyo mifumo ya governance duniani ambayo serikali ya CCM inaitumia!!
 
Kwa hiyo hapa rasimu inalenga kuvunja hoja za Chadema Au kukidhi matakwa ya watanzania wenye kiu ya kujitawala na kuwa na nguvu katika umiliki wa rasilimali zao na kuondoa ukiritimba Wa serikali na uhodhi mkumbwa Wa madaraka ya taasisi ya rais?!

Kama hayo tu ndio maamuzi magumu basi hii rasimu bado tutaipinga sana
 
hayo yote mi nilitoa maoni yangu ingawaje kuna moja ile ya WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUCHAGULIWA NA WANANCHI SIJAIONA HAPO sasa sijui ndio imeshapigwa chini by the way tunategemea mambo mazuri kutoka katika katiba mpya ijayo.
 
Aiseee! Ngoja tusubiri, Kinana kawaruhusu? Na fastjet a.k.a msaidia mateja wenye macho mlegezo, paja zenye tattoo na kiuno chembamba NA siyo akina Ngwair?

hahaaaaa yuko singapore leo eti kwa ziara ya kikazi
 
Mkuu nyakageni umegusa patamu sana.
Lakin bwama mkubwa alimsaidia huyo mwenye sifa ulizotaja kama msani tu au kuna cha ziada?
 
Mbona hakuna maamuzi mazito hapo.....hayo yalikuwa ni lazima yawepo kwenye katiba....la sivyo isingekuwa mpya...!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom