Tumeacha kutetea bandari zetu sasa tunatetea mwekezaji muislam, waziri muislam na rais muislam!

Tumeacha kutetea bandari zetu sasa tunatetea mwekezaji muislam, waziri muislam na rais muislam!

Wee mwislam?
Sasa kama mwananchi wachini hana maamuzi katika nnchi atafanya lipi wao ndio wapangaji na ndio wapanguaji sisi ata wakiuza nchi tutasubiri kuambiwa tuna hamia wapi
 
Ni rahisi sana kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao na CCM wanalifahamu vizuri jambo hili.

Hata kama kuna jambo baya sana kwa maslahi ya nchi yetu ukitaka likubalike basi wewe lipake rangi ya dini flani utaona mara moja watazuka watu na kulitetea kwa nguvu zao zote kwasababu tu jambo hilo lina rangi ya dini yao!

Suala la mkataba wa bandari limeonesha kuwa watanzania hawana misingi ya kusimamia isipokuwa mafungamano na dini zao.

Ni ajabu kubwa kwamba watu wapo tayari kuuza nchi yao kwa kuaminishwa kwamba hili ni jambo la kidini! CCM wanajua fika jambo hilo na wanalitumia sasa kama walivyolitumia kwenye chaguzi zilizopita dhidi ya CHADEMA na CUF.

Suala la bandari lilianza kujadiliwa vizuri kwa uzalendo lakini watu flani walipogungua linagusa dini yao sasa wamebadili hoja zao na bandari imekuwa suala la kidini.

Sakata la bandari sasa limekuwa suala la Uislamu; mwekezaji muislam, waziri mwislam na rais mwislam!
Na uarabu umegeuzwa uislamu. Hawa waarabu pamoja na uislaam wao walitutia waafrika utumwani na kutuuza kama wanyama. Walitutendea ukatili mbaya sana kinyume kabisa na maagizo ya uislaam na mtume wake. Leo wasituvuruge eti uislaam na waarabu ni kitu hicho hicho? Hapana.
Tutalinda bandari zetu waondoke huko.
 
Mbona nyie watu mna vichwa vigumu nani amewakataa DPW kinachokataliwa ni namna mkataba ulivyo.
Hii nchi una watu wa ajabu sana
Kwanza jifunze kutofautisha kati ya "MKATABA" na "MAKUBALIANO" au "MoU".
maana kama hujui tofauti ya maneno hayo huto elewa chochote, sio kosa lako, endelea kujifunza utaelewa.
 
Tujadilini mambo ya msingi mambo ya dini hayahusiki hapa. Tukigawanywa kwa misingi ya dini tutaibiwa kila kitu.
Sidhani kama ni sahihi kuacha kujikita kwenye contents na kuangalia suala gani limeletwa na mtu wa dini gani.

Dini yetu kubwa hapa iwe ni kuitetea Tanzania yetu. Dini tubaki nazo kama imani tu.
 
Ni rahisi sana kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao na CCM wanalifahamu vizuri jambo hili.

Hata kama kuna jambo baya sana kwa maslahi ya nchi yetu ukitaka likubalike basi wewe lipake rangi ya dini flani utaona mara moja watazuka watu na kulitetea kwa nguvu zao zote kwasababu tu jambo hilo lina rangi ya dini yao!

Suala la mkataba wa bandari limeonesha kuwa watanzania hawana misingi ya kusimamia isipokuwa mafungamano na dini zao.

Ni ajabu kubwa kwamba watu wapo tayari kuuza nchi yao kwa kuaminishwa kwamba hili ni jambo la kidini! CCM wanajua fika jambo hilo na wanalitumia sasa kama walivyolitumia kwenye chaguzi zilizopita dhidi ya CHADEMA na CUF.

Suala la bandari lilianza kujadiliwa vizuri kwa uzalendo lakini watu flani walipogungua linagusa dini yao sasa wamebadili hoja zao na bandari imekuwa suala la kidini.

Sakata la bandari sasa limekuwa suala la Uislamu; mwekezaji muislam, waziri mwislam na rais mwislam!
Na Ndio silaha pekee waliyobaki nayo watawala! Unfortunately ..it temporary and highly vulnerable risk🤔!
Hiki kitu kimepangwa...Ndio maana hata Haji Manara alipoongelea Sakata hili kwajicho la kikabila na kikanda hakuna aliyekemea!
 
Kwa hiyo Mkataba wa Bandari upo vizuri Kwa muktadha wa kiislam!
 
Yaan kuna wakati nafikia nachukia dini. Sio ya kiisalmu tu hata yangu ya kikristo. Naona kama zililetwa kutupumbaza hivi.
 
Reasoning yako ni ya kijinga sana, DPW kutojenga msikiti UK na kwingineko, sio lazima wasijenge pia huko Mbeya.

Huu upeo wenu ndio unasababisha wengine wajishushe kifikra ili kwenda nanyi sawa, mnajiona mnaonewa kwa kutumia mifano ya kitoto kabisa kujenga hoja zenu, na nyie kuachwa bila kuambiwa ukweli, tutaliharibu hili taifa.
✔️✔️✔️✔️
 
wacha ubaguzi.
mimi ni mkristu lakini nakubaliana na uwekezaji wa DPW naamini kuna wakristu na wasio na dini wengi wanakubali jitihada za Mhe. Rais na Serikali yake katika kukuza uchumi wa nchi.

lakini wapo baadhi wachache, wanao ingiza chuki ya kidini kwenye suala hili la uwekezaji, huo ni upuuzi na kamwe usipewe nafasi, Serikali isonge mbele isiwasikilize wapuuzi.
Kenya imeingia mikataba ya uwekezaji na nchi ya kiislamu ya IRANI lakini huwezi kusikia huu upuuzi, tuache ujinga.

Mama asibabaishwe wala kuyumbiswa na wanafiki....asonge mbele kwa masilahi ya Taifa letu.
😀😀😀. Mud weeee
 
Kipindi cha "Yohana" ndio kipindi pekee Maaskofu waliulizwa uraia wao mpaka kupelekea kuulizwa vyeti vya kuzaliwa vya bibi zao.
Ulikuwa unanyonya kiasi hayo hukuyashuhudia!!??
Kipindi cha "Yohana" ndiyo kipindi tulijua kuwa hawa viongozi wetu wa madhehebu ya Kikristo walivyo na PhD. za kweli kupitia "Waraka/Nyaraka" zao na maandiko yao mbalimbali katika kupinga nchi ilivyokuwa inaendeshwa.

Huyu "Yohana" kwa mujibu wa bandiko lako, atakuwa alikuwa ni mvaa kobazi, kwa mujibu wa bandiko lako.
Hapo ndio uone hapa wavaa kobazi ni watu wajinga haswaa
 
Dini ya kweli ni ukweli wenyewe ambao hauwezi kupatikana kwa asilimia 100 kwenye dini zetu.
Uhusiano wako na Mungu ni wa moja kwa moja na siyo lazima upitie dini.
Fikiria katika kweli na haki kwa faida yako, wananchi wenzako na taifa kwa ujumla.
 
Miaka yote haya mambo ya udini hujitokeza pale anapotokea mtawala dhaifu, asiyeweza kuenenda vyema na majukumu yake ya kiofisi, hasa anapoanza kuharibu kwa ujinga wake mwenyewe, na nchi kuanza kumshinda.

Ndipo wanajitokeza wajinga wenzie wa imani yake na kuanza kumtetea, huwa wanafanya hivyo kwasababu wamezoea kuchanganya hisia na facts, kwangu ni vitu viwili ambavyo haviendani kabisa, kwani suala la imani na ubovu wa mkataba, ni mambo mawili tofauti.

CCM nao, kwa kutambua huo ujinga wao, huanza kuitumia karata ya udini pale wanapoona utetezi wao mwingine wote tumegoma kuusikiliza, hapo ndipo hugeukia kwenye dini kama karata yao ya mwisho, ila bahati mbaya kwao this time, kwenye hili suala la bandari zetu watanganyika, udini wao nao umegoma.

Hapa niwaase wale jamaa ambao hujidai kuogopa kujadili jambo lenye muelekeo wa kidini, wakijiona wastaarabu sana, kwa kuhofia kuwakwaza wa imani tofauti.

Watambue kwa kufanya kwao hivyo, ndipo wanawapa CCM na uhuni wao ushindi, jambo lolote lenye muelekeo wa kidini lazima lijadiliwe kwa umakini, penye ukweli usemwe with facts, pasiwepo unafiki, tusifichane. Muhimu heshima iwepo mwiongoni mwetu, ili siku nyingine CCM washindwe kuitumia hii karata yao pendwa ya turufu kutupoteza.

Sasa hapa ni kuamua, ama kusema kweli ituweke huru, tujikomboe kifikra, na tulikomboe taifa, au tufichane kwa hofu ya kuogopa dini zetu hivyo tusiambizane ukweli, ili CCM iendelee kutuchezea milele kwa kujua na kuutumia udhaifu wetu, kwa maslahi yao, chaguo ni letu..
Yaani CCM turufu ya mwisho kuzima suala la uuzaji wa bandari, ni kuchomekea UDINI, lakini wapi, suala ndo kwanza linapamba moto. Kinacholifanya lipambe moto ni pale walipoziengua bandari za Zanzibar zisiwemo, hivyo kutoa hasira kama mkataba huu ni mzuri kwa Nini bandari za Zanzibar zisiwemo?
 
Tatizo nchi hii akiongoza mvaa kobasi kuna watu roho zinawawasha ata awe mwema kiasi gani,Mwalimu Nyerere alilia kuhusu ubinafshaji wa mashirika ya Umma lakini tulibinafsisha. Miaka kadhaa nyuma tumesaini mikataba ya reli SGR na bwawa la Mwalimu Nyerere rufiji,Tuna mkataba wa mradi wa umeme pia maporomoko ya Rusumo(Tanzania,Burundi na Rwanda) walalamikaji wa sasa hawajawai kulalamika popote na wala awahoji.
Tupendane
Hawa wamepewa kazi ya ujenzi siyo kudishiwa au kubinafisishwa
 
ni akili za kijima kabisa!!

hivi majuzi tu Rais wa Kenya kampokea Rais wa nchi ya Kiislamu ya Irani na wameigia mikataba kadhaa ya uwekezaji nchini kenya.
wenzetu wemelenga uwekezaji sisi tunahangaika na chuki za kidini!!

naishauri Serikali yetu chini ya Rais Samia kusonga mbele na uwekezaji, kamwe wasisikilize wapuuzi wenye chuki za kidini.
Hivi nyie mbugila hamuelewi kinacholeta utata? Hakuna anayekataa mwekezaji, kinachokataliwa ni masharti yaliyomo, mfano kama mkataba ni mzuri, kwa Nini bandari za Zanzibar zisiwemo kwenye mkataba huo? Kwani wao hawataki kunufaika? IBARA 4 (2) ya mkataba huu inasema endapo Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi, kwa Nini nchi huru ikaombe ridhaa Dubai? Tena kwa mali zake? Mkataba wa Kenya una masharti hayo ya Kimangungo?
 
Ni rahisi sana kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini zao na CCM wanalifahamu vizuri jambo hili.

Hata kama kuna jambo baya sana kwa maslahi ya nchi yetu ukitaka likubalike basi wewe lipake rangi ya dini flani utaona mara moja watazuka watu na kulitetea kwa nguvu zao zote kwasababu tu jambo hilo lina rangi ya dini yao!

Suala la mkataba wa bandari limeonesha kuwa watanzania hawana misingi ya kusimamia isipokuwa mafungamano na dini zao.

Ni ajabu kubwa kwamba watu wapo tayari kuuza nchi yao kwa kuaminishwa kwamba hili ni jambo la kidini! CCM wanajua fika jambo hilo na wanalitumia sasa kama walivyolitumia kwenye chaguzi zilizopita dhidi ya CHADEMA na CUF.

Suala la bandari lilianza kujadiliwa vizuri kwa uzalendo lakini watu flani walipogungua linagusa dini yao sasa wamebadili hoja zao na bandari imekuwa suala la kidini.

Sakata la bandari sasa limekuwa suala la Uislamu; mwekezaji muislam, waziri mwislam na rais mwislam!
Mtatoka tu mafichoni na nia zenu ovu, yaani ni kama vile mnavyotetea na kufaidika na bandari ndio hivyo hivyo na wao wanataka kufaidika, jiulize kwanini maaskofu na mapadri wamejivika siasa na kulisemea hili tena ya uongo na uongo uliopindukia? Ili tu mafanikio yasije?
Imeisha hiyo tukutane tarehe 1/9

Nyie ni wadini kuliko, ila 2030 tutamuweka kiboko yenu ili mkome kabisa
 
Hivi nyie mbugila hamuelewi kinacholeta utata? Hakuna anayekataa mwekezaji, kinachokataliwa ni masharti yaliyomo, mfano kama mkataba ni mzuri, kwa Nini bandari za Zanzibar zisiwemo kwenye mkataba huo? Kwani wao hawataki kunufaika? IBARA 4 (2) ya mkataba huu inasema endapo Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi, kwa Nini nchi huru ikaombe ridhaa Dubai? Tena kwa mali zake? Mkataba wa Kenya una masharti hayo ya Kimangungo?
hiyo ni hoja ya kitoto kabisaa, eti kwa kuwa znz hawajawekeza basi sisi bara tusikubali...ebo! sasa hiyo ni hoja ama utoto?! kwa hiyo kila kinacho wekezwa bara lazima kwanza znz nao wakubali kwanza?! hiyo ni hoja ya kitoto, watu wazima hatuwezi kupoteza muda kwenye hoja hiyo.

kilichopo kwa sasa na "Makubaliano" sio "makataba" hivyo mikataba itakapo sainiwa basi vipengele vya msingi vitazingatiwa.
 
Back
Top Bottom