Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Tumeachana rasmi kwa kuwa mimi si Mchaga

Kuna kaukweli hapa...ipo hata kwa wanawake kama anapata bwana sio mchaga kwao wanaleta ubaguzi.
 
Mimi mchaga na babangu ananikazia lazima nioe mchaga nikitaka kuoa.japo babangu ni muislamu pure alieshika dini



Ila mimi ni mchaga rebel sina kabisa mambo yao ya kichaga na nitaoa yoyote sitaki limit kwenye maisha yangu.
Hongera kwa kuwa Mwanaume badala ya Mvulana.
 
Shukru Mungu wachaga wabinafsi sn umeepushwa na mengi Mungu atakupa mwingine wa kufanana nawe
Kaka yangu m1 hivi anamiliki kiwanda flani hapa TZ, mkewe ni meneja mkuu ktk hicho kiwanda, basi huweziamini kajaza Wachaga tupu kwenye hicho kiwanda hadi wasio na CV na wakienda ndugu wa kaka yangu hata wakiwa na CV zote kuajiriwa ni kukataliwa mbele kwa mbele tu mpaka wakati mwingine ndugu hutamani hicho kiwanda kife.
 
Be strong, utampata alie sahihi kwako toka kabila lolote likiwemo hilo hilo la kichaga
 
Kwa kweli dunia ina mambo ya ajabu sana. Exboyfriend wangu ni Mchaga wa milimani. Tumedumu naye katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitano. Lakini katika muda huo kumekuwa na ups and down nyingi sana ambapo tukikaa tunarekebisha maisha yanaendelea.

Kwao natambulika ingawa si rasmi. Na swali la kwanza waliloniuliza kwao mimi ni kabila gani.

Wakaonyesha kunipokea na kunijali ingawa haikuwa utambulisho rasmi.
Baada ya miaka yote, nimegundua mwenzangu ameanzisha mahusiano na binti wa kichaga, yupo chuo mkoani.

Nikajaribu kuongea na mwenzangu ambaye aliniambia hayupo serious naye na ndio maana muda wote yupo na mimi na hawezi kuniacha hata itokee nini.

Baada ya siku chache tena mwenzangu akawa anaendeleza mahusiano hadi kupigiana simu zao mbele yangu.

Nilichokifanya ni kumlazimisha jamaa kuchagua jambo moja, mimi au Mchaga mwenzake wa huko chuo.
Mwenzangu alionyesha ugumu sana sana sana kuniacha ila pia kule kwa Mchaga mwenzake pia hataki kuacha.

Anachonieleza ni kuwa amenizoea, namjali, mimi ni part ya maisha yake, hivyo hataki niondoke ila wazazi wake wanataka apeleke mtu Mchaga na si kabila lingine.

Nimeamua kuondoka katika maisha yake ingawa mpaka sasa mwenzangu analeta ugumu sana katika kuchukua vitu vyangu nilivyoacha kwake. Ananidanganya na kunizungusha sana lakini kiukweli maisha anayotaka niyaishi, si maisha ninayoyataka.

Nimehuzunika tu kwa kuwa tumefika mwisho kwa sababu mimi si MCHAGA. Ubaguzi ambao Wachaga wengi wanao.

Nashukuru Mungu kwa kunipa pumzi hii hata nimeweza kulitoa dukuduku hili kwa ndugu zangu wana JF.
Pamoja na comment za kibabe ila kiukweli huwa ninafarijika sana ninaposhare na kukosolewa au kuonyeshwa njia sahihi.
Pole sana
 
Pole sana, uko sawa kuacha sehemu ambayo haina mwelekeo wa maisha...miaka mitano yote🤔🤔
Ipo siku utapata wako.
 
Hapo kwenye mizigo hapana, strictly Machame tu[emoji23][emoji23][emoji23] ila kwa rangi na ngozi laini ni hapo Marangu mangi[emoji122][emoji122][emoji122]
Naona una uzoefu sana na hao wachaga na umenena vyema sana wala haujadanganya kabisa Chifu.
 
Tukiachana na mada ya huyu msichana.sisi si tunakaa na wachaga?

Ninawafahamu vzr Sana .

Nyie ni wabaguzi,wakabila,wezi,wenye roho mbaya na siku hiz wadada wenu wanajiingiza kwenye umalaya Sana kupitiliza
Nani kakuambia mimi ni mchagga?
 
Haya mapalestina ni bora muyaachage yaoane yenyewe kwa yenyewe tu...tena afadhali yako maana mwanaume ndo alikua mchaga ndo maana ukapata hata hiko kinafasi cha kutambulishwa ukweni
Mahusiano ambayo mwanamke ndo mchaga na mwanaume ni kabila jingine ndo yanakuwaga magumu balaa!!
Ni nadra sana mwanaume asiye mchaga (CHASAKA) kukubaliwa kuoa uchagani maana wanahofiaga kumpoteza member wa ukoo wao.
Kiufupi wachaga ni wabaguzi sana na wana ukabila kiwango cha SGR

i agree
 
Back
Top Bottom