Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Tumebakisha siku 4 kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.a.w): Niulize chochote kuhusu Mtume Muhammad (S.A.W.) Nitakujibu

Hujajibu swali nililo kuuliza. Jibu lake nimeliona.

Ndiyo maana nikakupa angalizo usije kuuliza tena maswali ambayo umejibiwa

Kingine jitahidi sana uwe mtafiti wa mambo siyo unachukua chukua kisha unajenga hoja kwayo.
Kama uliona, kwanini hukumuuliza huyo aliyejibu?

Maana ulitakiwa ushangae kwanini ameonekana kujua nilichokiuliza tafsiri yake anajua mahali nilikopatia hilo swali
 
Kwanini mnaadhimisha Maulidi (Mazazi) ya Mtume ?
Lengo ni kuongeza mapenzi yetu kwa Mtume, Mtume (saw) alisema, "Hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa na imani mpaka anipende mimi kuliko baba yake, watoto wake na wanadamu wote. .

Kulingana na mila ya Kiislamu, wanyama, miti na hata vitu visivyo na uhai kama milima vilionyesha upendo kwa Nabii Muhammad (saw), na pia aliwaonyesha upendo pia. Kwa hivyo, kuongeza upendo wetu kwake na kuionyesha ni sawa na maumbile yote na hutuunganisha na nishati ya kiroho ya ulimwengu.
 
Kama uliona, kwanini hukumuuliza huyo aliyejibu?

Maana ulitakiwa ushangae kwanini ameonekana kujua nilichokiuliza tafsiri yake anajua mahali nilikopatia hilo swali
Sababu unauliza maswali ya kijinga kiasi ambacho huonyeshi kama unataka kujua zaidi ya kupotezea watu muda.

Kingine,nimuulize aliye jibu kwa minajili gani ?
 
Hivi manabii waliwahi kuonana na kuongea?
Ndio, mtume wetu alikutana na manabii karibu wote kwenye safari yake ya kwenda Mbinguni, na pia alikutana na nabii Ibrahim, na hadi leo sisi waisilamu tunamtakia rehema nabii Ibrahim kwasababu alimuagiza mtume kutusalimia, hivyo salamu zake tulizipata na tunamuitikia kila baada ya sala.
 
Jibu swali nililo kuuliza,nitajie sifa unalets ngonjera.
Nimekuambia sifa zile zile unazotumia wewe kupinga uhalisia wa habari kutoka kwenye maandiko mengine ya dini tofauti na yako, ndio hizo hizo sifa zinazoweza kutumika kupinga uhalisia wa tukio lolote lile kutoka kwenye dini yako
 
Lengo ni kuongeza mapenzi yetu kwa Mtume, Mtume (saw) alisema, "Hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa na imani mpaka anipende mimi kuliko baba yake, watoto wake na wanadamu wote. .
Kwani kumpenda mtume ni kufanya ambayo hajayafundisha au kutenda yale aliyo yafundisha ?

Uko wapi na aya hii ya Allah :

31. Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. (al-Imraan : 31)

Hii ndiyo maana halisi ya kumpenda Mtume. Swali je utampenda vipi nje yale amambayo hakuyafundisha na utampenda vipi Mtume bila kumfata ?

Kwani Maswahaba hawakusherehekea Maulidi ? Je wao hawakuwa wakimpenda Mtume ? Hili unalizungumziaje ?

Unajua kama Maulidi zilianza karne ya 5 Hijiriya katika dola ya Faatwimiyyah dola ya Mashia ?
 
Sababu unauliza maswali ya kijinga kiasi ambacho huonyeshi kama unataka kujua zaidi ya kupotezea watu muda.

Kingine,nimuulize aliye jibu kwa minajili gani ?
Kwa minajili ya kupata kujua, kwasababu kaonesha kulielewa swali langu. Go ask him
 
Kwani hii thread umetoa wew alieandika kasema uliza chochote na icho kinachoulizwa ni chochote kwaiyo maswali ya kejeli unayoyaona hujibiwa kwa fact zile konki muulizaji atakimbia mwenyw ndio maana ya mjadala wa maswali na majibu,,,, NB fatilia mihadhara utaona how Muslim walivo na kejel sio vimaswali by humu ambavy havina kichw wal miguu na unaita kejeli

Nimekuelewa vizuri
Kweli mjadala wa maswali na majibu yako hivyo kama ulivyoainisha
Ila sio vizuri kukashifu
Kuna mdau asie na maadili toka makuzi yake amenijibu kwa matusi
Asante
 
Nimekuambia sifa zile zile unazotumia wewe kupinga uhalisia wa habari kutoka kwenye maandiko mengine ya dini tofauti na yako, ndio hizo hizo sifa zinazoweza kutumika kupinga uhalisia wa tukio lolote lile kutoka kwenye dini yako
Zitaje,upingaji wangu na upingajia wako ni ardhi na mbingu hatufanani hata chembe.

Sasa usitafute kichaka,nasubiri jibu la hizo sifa. Usipoteze muda kijana. Huu mjadala wa kielimu usilete utoto na kukinbia maswali.
 
Kwa minajili ya kupata kujua, kwasababu kaonesha kulielewa swali langu. Go ask him
Sasa nijue mara ngapi ? Hujaona nilipo kwambia kama unauliza maswali ya kijinga maswali ambayo laiti kama ungekuwa unatafakari au kufanya utafiti hata wa kiwango kidogo sana usingeuliza maswali kama unayo uliza.

Yaani unaleta habari za makatuni unakuja kujengea hoja katika uhalisia ?

Hivi hukuwahi kusoma somo la "Adabu za kujadiliana na kufanya utafiti" ?
 
Bi hadija alikuwa mkubwa kwa mtume kwa miaka 15
Hili unatakiwa kulifanyia utafiti wa kina japo katika ulimwengu wa kiislamu katika fani ya uhakiki wa habari ni kuwa kauli yenye nguvu ni kuwa Mtume alikuwa na miaka 25 na mama Khadija alikuwa ana miaka 28. Na mapokezi ya miaka 40 hayana nguvu.
 
Yeye (Muhammad Ibn Abdullah) alizaliwa katika nyumba ya ami yake, Abu Talib, katika “mtaa wa Bani Hashim” huko Makka, tarehe 12 Rabil-awal ya ule Mwaka wa Tembo, tarehe ambayo inaoana na tarehe 8 Juni 570.

Mama yake na mtume Muhammad (s.a.w), Bi Amina, alituma habari za uzazi huu wa kheri kwa babu yake na Muhammad, Mzee Abdul Muttalib, ambaye alikuja, akamchukuwa mikononi mwake, na akampa jina hili la Muhammad.” Lenye maana ya MSIFIWA.

Nawakaribisha kuuliza maswali kuhusu mtume wetu huyu MUHAMMAD "amani na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake".

View attachment 1975182
Je unaamini kua Mtume (S.A.W.W) alituachi vitu viwili vizito ambavyo ni kitabu cha Mwenyezimungu na watu wa nyumba yake?
 
Baba wa mtume alikuwa akiitwa Abdullah ibn Abd al-Muttalib Alikuwa mtoto wa Abdul-Muttalib ibn Hashim na Fatimah binti Amr wa ukoo wa Makhzum. Hawa walikuwa wakifuata mila za Nabii Ibrahim, bila shaka walikuwa waisilamu
Kabla ya mtume uislam haukuwepo mkuu,
Kabla ya waislam kuanza kumuabudu ALLAH walikuwa na miungu kama 300 hivi ,ila Mungu prominent wa eneo ambalo uislam uliibuka alikuwa akiitwa HUBAL.
 
Je unaamini kua Mtume (S.A.W.W) alituachi vitu viwili vizito ambavyo ni kitabu cha Mwenyezimungu na watu wa nyumba yake?
Ni sahihi kabisa, Mtume alituachia vizito viwili (Thaqalaini) tukishikamana navyo hatuta potea. Navyo ni kitabu kitukufu na Ahlulbayt wake, japokuwa kuwafuata Ahlulbayt imechukuliwa sana na upande wa Shia, na kwa upande wa Sunni, inapendelewa hadithi ya mtume kutuachia Qur'an na Hadithi.
 
Back
Top Bottom