Mademu bwana mingo zenu huwa mnazijua wenyewe.
Sasa naamini kuwa hii ndio mentality ya wanawake wengi.
Honestly nipo kwenye situation kama hiyo na manzi mmoja. Analaumu kuwa kila siku yeye ndiye anayeanza kutuma meseji.
Anajihisi kuwa anajipendekeza na kwamba upendo umeoungua au hisia zimeisha.
Lakini kikawaida mimi nisipokuwa na chakusema huwa sisemi (hii najizungumzia mimi)
Kuanza tu kupiga simu au kutuma meseji sijui "mambo, niaje, uko poa" bila kuwa na maada muhimu ya kufanya mazungumzo yawe na tija, kiukweli siwezi.
Na sio kwamba nafanya hivyo labda nimemchoka, hapana.
Saizi tuko katika ulimwengu ambao shughuli zetu za kutafuta kipato zinaweza kukunyima fursa ya kushika simu muda mrefu.
Sasa mimi naweza kuwa niko na free time lakini kusema nimtumie mtu meseji yenye lengo la kupiga stori, kiukweli huwa napata tabu ku imagine kuwa muda huu utakuwa ni muda rafiki kwa huyo mtu kuweza kushika simu kwa conversation ambayo haihusiani na mchongo wa hela au jambo lolote la kidharura?
Lakini nilichokuja kubaini ni kwamba, wanawake wanapenda ku cope lifestyle za mahusiano za mashosti zao.
Unakuta yeye anaona mashosti wake wako bize kutumiana meseji na boyfriends zao, emojis za kutosha basi na yeye anatamani na kuona kama style hiyo ndio ishara ya upendo.
Halafu mara kadhaa ambayo nimekuwa katika stori naye, unakuta yeye tena ndio anabaki kuwa msikilizaji, hachangii chochote anabaki tu kuitikia tu.