Tafuta mwingine upate UTI nauza AzumaHabari za usiku
Mimi napitia changamoto ya kimahusiano. Tumenyamaziana na mwanaume niliyekuwa na mahusiano hii ni week ya 4.
Kusema ukweli sina kosa lolote nililolifanya ila ni yeye ndio alikuwa na vitu alipaswa kuniambia (siwezi kuviweka hapa maana mhusika anaweza kuwa humu)
Nilijipa siku 3 za kujipendekeza kumtafuta kila siku ni mimi naanza nilivyomaliza hizo siku 3 nikauchuna; huwezi amini na yeye akakaa kimya ni ku-view status na ku-like. Hakuna kuongeleshana
Sihitaji kumtafuta.. na kama hatonitafuta nitafanya maisha yangu
Sasa nauliza; tumeshakaa mwezi hatuongeleshani - je naweza kuanzisha mahusiano mapya au bado mapema?
Na unampenda milile, haya pole mamaNampenda ila hanipendi
Dah hajatambulishwa, hawajui🤣Kamsemee kwa ndugu zake
Futa namba hiyo huko kuendelea kuona status kunawapoteza, futa namba tulia zako, mpaka unawaza mahusiano mapya nna imani tayari kuna mtu ushamuona anafaa zaidi na tayari ana percent kubwa sana ya kuwa nawe.Daah mimi nipogo hivo tu sijawahi kufuta namba ya mtu labda huyo mtu afute yangu
Hii huwa inaua mahusiano mengi sana tena mengine ni mazuri ila viburi vya uzima vinawaachanisha.Unakuta na yeye kimoyomoyo anatamani akutafute ila anajizuia, anatamani wewe ndo uanze kumtafuta,
Mkiendelea hivi mmoja asipojishusha, mwishowe wote mnasahauliana
Hiyo status mbona wairudia sana. Ndiko mlipendania huko status? Msubiri aje huko status mkutano myajengeMwezi mmoja sasa yupo kimya anaweka status anaview zangu na like juu yaani ni first viewer kwenye status zangu ila ku Nicheck kipengele
Na ukishakula ukakapotezea ndio utaona kanakomaa kukutafuta.Naamini mpaka unafuta namba ya mtu, inamaanisha bado unajali ila unajikaza usionekane mnyonge
Kama kuna kadada kamoja kana tabia izo, nsipomtafuta hanitafuti, kila siku shobo nianze mimi, kiuhalisia kibinadamu inauma kila siku wewe ndo umtafte mwenzio, mwenzio hata hainui kidole kukukumbuka, hapa najifanya mjinga ajichanganye nile mzigo, baada ya hapo mbona atafurahi mshamba_hachekwi
Naita utoto, silent treatment ni emotional abuse , the best way ni kusema unataka moja mbili tati, akishwindwa muachaneKuna mdada mwingine kwenye confession page alisema aliachana na wanaume wa 3 tofauti, hawakugombana, ila tu ni ile silent treatment, mtu anajiona akimtafuta mwenzake atakuwa anajishusha, mwishowe uhusiano unakufa.
Mahusiano mengine mengi ya sasa, hamna anayetaka kuonekana mnyonge kwenye mahusiano, mnaweza mkawa wote moyoni mnapendana, ila kuonesha upendo ndo kipengele, mwishowe mahusiano yanakufa, mnabaki single.
Watu wengi wanataka kuoneshwa upendo, ila wao kuonesha upendo ni kipengele
Hakuna mahusiano bila mawasiliano. Njia ya kuua mahusiano ni kukaa kimya, jamaa kaitumia hiyo njia na kawini.Habari za usiku
Mimi napitia changamoto ya kimahusiano. Tumenyamaziana na mwanaume niliyekuwa na mahusiano hii ni week ya 4.
Kusema ukweli sina kosa lolote nililolifanya ila ni yeye ndio alikuwa na vitu alipaswa kuniambia (siwezi kuviweka hapa maana mhusika anaweza kuwa humu)
Nilijipa siku 3 za kujipendekeza kumtafuta kila siku ni mimi naanza nilivyomaliza hizo siku 3 nikauchuna; huwezi amini na yeye akakaa kimya ni ku-view status na ku-like. Hakuna kuongeleshana
Sihitaji kumtafuta.. na kama hatonitafuta nitafanya maisha yangu
Sasa nauliza; tumeshakaa mwezi hatuongeleshani - je naweza kuanzisha mahusiano mapya au bado mapema?
NAKAZIAAnzisha mahusiano, achana na mnunaji
Nadhani wewe ni wale watu ambao kiasili hampendi mawasiliano si kwa sababu ya ubusy wa kazi ila basi tu, ninavyojua mimi mtu hata awe busy vipi hawezi kukosa nafasi ya kuwasiliana na mwenza wake. Inabidi upate mwenza mwenye tabia kama yako vinginevyo mahusiano yatakua kipengele.Mademu bwana mingo zenu huwa mnazijua wenyewe.
Sasa naamini kuwa hii ndio mentality ya wanawake wengi.
Honestly nipo kwenye situation kama hiyo na manzi mmoja. Analaumu kuwa kila siku yeye ndiye anayeanza kutuma meseji.
Anajihisi kuwa anajipendekeza na kwamba upendo umeoungua au hisia zimeisha.
Lakini kikawaida mimi nisipokuwa na chakusema huwa sisemi (hii najizungumzia mimi)
Kuanza tu kupiga simu au kutuma meseji sijui "mambo, niaje, uko poa" bila kuwa na maada muhimu ya kufanya mazungumzo yawe na tija, kiukweli siwezi.
Na sio kwamba nafanya hivyo labda nimemchoka, hapana.
Saizi tuko katika ulimwengu ambao shughuli zetu za kutafuta kipato zinaweza kukunyima fursa ya kushika simu muda mrefu.
Sasa mimi naweza kuwa niko na free time lakini kusema nimtumie mtu meseji yenye lengo la kupiga stori, kiukweli huwa napata tabu ku imagine kuwa muda huu utakuwa ni muda rafiki kwa huyo mtu kuweza kushika simu kwa conversation ambayo haihusiani na mchongo wa hela au jambo lolote la kidharura?
Lakini nilichokuja kubaini ni kwamba, wanawake wanapenda ku cope lifestyle za mahusiano za mashosti zao.
Unakuta yeye anaona mashosti wake wako bize kutumiana meseji na boyfriends zao, emojis za kutosha basi na yeye anatamani na kuona kama style hiyo ndio ishara ya upendo.
Halafu mara kadhaa ambayo nimekuwa katika stori naye, unakuta yeye tena ndio anabaki kuwa msikilizaji, hachangii chochote anabaki tu kuitikia tu.
Atatambulishwa akishakuwa single mother 😂Dah hajatambulishwa, hawajui🤣
Noma sanaAtatambulishwa akishakuwa single mother 😂
Mhmm basi kuna watu tutayashindwa tuMahusiano na mawasiliano ni barabara mbili ziendazo sambamba ikiwa tofauti na hapo ujue unapoteza tu muda. Kwa mlipofika utaamua wewe kama uendelee kumbembeleza mtu ambae ashakuonesha dhahiri huna maana kwake ama ushike 50 zako.