Katika suala hili nadhani umefika wakati sana chama kwa maana ya Viongozi wake wakuu wakalitolea ufafanuzi wa kina tena bila kuacha alama yenye mashaka yoyote suala la matumizi ya RUZUKU na michango ya Wabunge namna ilivyotumika na mpaka sana au muda tuhuma hizi zilizotolewa BUNGENI chama wana akiba kiasi gani.
Ikiwa wabunge walichangia chama nafikiri si kosa lakini kama yapo matumizi ya hovyo kama alivyosema Mbunge kwa hakika anguko kubwa linakuja ingawa si kitu ambacho ningependa kukiona tena katika uhai wangu.
NCCR walituangusha sana waTanzania kipindi kileeee,baada ya kushindwa kutoa upinzani wa maana tulikuja kushuhudia viwanda na makampuni ya umma yakiuzwa kwa bei ya kutupwa kwasababu hapakuwa tena na sauti ya kuusemea umma.Ni vyema Mwenyekiti pamoja na team yake wakaachana na suala la CORONA kwakuwa tayari wananchi wengi wanaona serekali ipo sahihi.