Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Kulingana na utafiti uliofanywa na Twaweza,MISA-TAN,Jamii Forum na TAMWA asilimia 50% ya waandishi wa habari hukumbana na vitisho,ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.

Ila hili la mwisho si walisema yameisha na JPM? siku hizi watu wote wanaimba kumbaiya ...
 
Erythrocyte ama ChoiceVariable ni waandishi?

Nawaulizeni wajuvi.

Kunguru?
 
Safari ya maendeleo Tanzania bado ni ndefu sana. Wewe unasema hivi, mwingine atasema "nilivyohangaika kusoma kwa tabu kwanini nianze kuikosoa serikali?, na mwingine atasema "nilivyohangaika kupata kazi hivi kwanini niikosoe serikali?, na wahadhiri wa vyuo vikuu wakisema "ya nini kuandaa bongo za wanafunzi kuwa critical thinkers waje wahoji utumbo wa serikali?...Tukienda hivi check and balance itatoka wapi? Bila check and balance hakuna kitakachofanyika nchi itabaki hivi hivi
 
Investigative journalism ni ngumu sana kwa mazingira yetu na ukizingatia kwamba sheria nazo sio rafiki kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari.
 
Investigative journalism ni ngumu sana kwa mazingira yetu na ukizingatia kwamba sheria nazo sio rafiki kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari.
Lakini hapa katikati kulifanyika investigave journalism ya hali ya juu sana. Enzi za MwanaHalisi nani anaweza kusahau; hata enzi za This Day....
 
Vyombo vya habari vimetukana weee hamjaridhila tu bado. Mama ameruhusu endeleeni kutuka a yeye kimyaaa. Mnataka nini tena. Au uhuru ni upi kwenu. Mnataka mpaka muingie chumbani kwake ndo mjihisi mko huru
 
Moja ya maandiko ya hovyo kabisa kuwahi kutokea ardhini na mbinguni. Sujui hii ni akili gani. Au ulikuwa umelewa
 
Kuna brother yangu aliwahi nidaka humu JF nikamkatalia sio mimi japo nilikuwa ni mimi alinidaka baada ya kunifanya profiling.Pia alimtambua mzee mwanakijiji ni Ndugu ...........
 
Ila hili la mwisho si walisema yameisha na JPM? siku hizi watu wote wanaimba kumbaiya ...
Kuna watu kwa makusudi kabisa,wanatumia namna utawala wa JPM ulivyo kuwa kuficha yale yanayo endelea sasa nchini.Na wakati huo waandishi wamekuwa katika hali tete katika awamu zote hapa nitataja matukio machache~

Mwaka 2012 mwezi Septemba tarehe 2,vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania viliripoti juu ya kifo cha Mwandishi wa habari wa kituo Cha channel Ten,Daudi Mwangosi kilicho tokea katika kijiji cha Nyororo mkoani Iringa na Mwandishi aliye husika kupiga picha kipindi jeshi la police likifanya mauaji hayo Joseph Senga hakuachwa salama naye alitangulizwa mbele ya haki.Hiki ni kipindi cha JMK.

Bila kusahau kifo cha utata cha Mwandishi wa habari za kichunguzi bwana Stan Katabalo juu ya sakala la Loliondo,kipindi cha mzee Mwinyi.

Hata kipindi cha BWM,hakuwa na mahusiano mazuri na waandishi wa habari,sababu ya dharau zake za wazi wazi ,ndio maana aliwahi kunukuliwa akisema "Waandishi wa habari wa Tanzania hawajui kiingereza".Hili hata mara kadhaa Jenerali Twaha Ulimwengu amezungumza sana tu.

Ni juzi tu hapa,Mwandishi aliye andika habari kuhusu RC kumnajisi mwanafunzi chuo cha SAUT-MWANZA kasha kamatwa,hivyo basi kumpa lawama zote JPM si Sawa,licha kwamba katika kipindi chake kulitokea hali ya sito fahamu kwa baadhi ya waandishi,lakini kitendo cha wachache kumuona yeye ndo mkosaji mkubwa kuliko wengine ni kujivika kiremba cha unafiki na kilele za uzadiki mkubwa.
 
Magroup ya vyuo vingi yanaweka kabisa masharti kuwa ni marufuku ku-discuss siasa. Na hamna group maalum Kwa siasa,na uki-discuss wenzako wanakuona wa ajabu sana nawenye ujasiri wa kipekee Ilihali utakuta mtu kaongea kitu Cha kawaida kabisa na hapo hapo utasikia unamwanasheria kaka?,kaka Kunawatu wanaku-zoom tu humu.Siasa itakusaidia nini wewe?

Kwahiyo lazima uwe muoga tu kujihusisha kivyovyote vile na habari za kisiasa.(Huo ni kwaupande wa vyuoni)
 
Investigative journalism ni ngumu sana kwa mazingira yetu na ukizingatia kwamba sheria nazo sio rafiki kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari.
Wala sio ngumu, tuna outlet media za kutosha ndani ya nchi na nje ya nchi. Sema ni vile tu watuna waandishi wanaojitambua.

Kwa dunia ya sasa ya kidijitali huwezi kuwa na habari moto na ukawa unawalipua watu.

Kigogo na Mange waliweza vipi kuwa wanatoa habari za ndani.
 
Vyombo vya habari vimetukana weee hamjaridhila tu bado. Mama ameruhusu endeleeni kutuka a yeye kimyaaa. Mnataka nini tena. Au uhuru ni upi kwenu. Mnataka mpaka muingie chumbani kwake ndo mjihisi mko huru
No rahisi zaidi kumvumilia mtu akutukane kuliko mtu anayekusukuma kwa fimbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…