Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

Moja ya maandiko ya hovyo kabisa kuwahi kutokea ardhini na mbinguni. Sujui hii ni akili gani. Au ulikuwa umelewa
Ni rahisi zaidi kukebehi hoja kuliko kujibu hoja... Mtu anakwambia "kaka shati umevaa nje ndani" Unageuka unajibu "We mjinga sana we shati linakuhusu nini". Unajisikia hadi mtu mwingine akuambie au ujione kwenye kioo.
 
Kigogo na Mange wana vyanzo au "source" za habari zao ila hawa hawawezi kujiita ni waandishi wa IJ.

Wanokifanya wao chaitwa kuvujisha habari au "information leakage" ambapo vyanzo hutoa taarifa za siri kutoka ndani ya taasisi kwa kufahamu (with knowledge) au kwa kutokufahamu (unintentional) kwenda kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Na kwa kuwa vyombo hivi vyabanwa na sheria za TCRA nakadhalika, ndo maana huruka maili kadhaa na kutua kwenye mitandao ya kijamii kwa Kigogo au Mange.

Hii ni moja ya silaha za kwanza na muhimu sana kwa mwandishi wa habari yoyote yule wa IJ ni vyanzo vya kuaminika.

Tofauti kubwa iliopo kati ya waandishi wa kwetu na wale walioko huko duniani ni kwamba wale wana vyanzo, wana mtandao yaani "network", watambulika kwa uwezo wao wa kitaaluma na kiuandishi na pia wanaheshimika.

Tukija kwenye IJ ni kwamba hawa wa huko duniani kabla hawajatoa habari yoyote ambayo yahusu IJ hutoa angalizo kwa wahusika kwamba kuna spana yaja na yatoka siku fulani, hivyo wajiandae kisaikolojia. Wakati mwingine kutokana na umuhimu wa IJ huitwa majina kama "watchdog reporting" au "accountability reporting" ikiwa na maana kwamba kinoripotiwa ni kitu muhimu na kinohitaji "attention" ya wahusika au vyombo vya serikali.

IJ ni ghali sana na huchukua muda kuandaa taarifa moja tu kabla ya kuiweka hewani hivyo hatuwezi kusema fulani na fulani ni waandishi wa IJ kumbe ni wapasha habari tu. Hata vyombo vingi vya habari hukwepa sana IJ kwani huitaji masuala kama matangazo na gharama za utayarishaji.

Hivyo bado kabisa Tanzania haijapata waandishi wa IJ ambao wameiva kwa kazi hiyo na siku wakipatikana utaona tofauti ya habari zao na zile za kuvuja.

Hapa nilipo nimewahi kutembelea chuo kikuu cha Missouri ambacho kina kitovu cha IJ mahsusi kwa wale wanotaka kujifunza IJ.

Chuo hiki naweza sema ni chuo bora kabisa duniani kwa ufundishaji IJ na wana taasisi kabisa inohusu waandishi wa habari za uchunguzi na wahariri inoitwa IRE-Investigative reporters and editors.
 
Safi sana! Attachment haifunguki mkuu.
 
Wenye vyombo vya habari ndio wanakiri wako salama sasa kuliko tuliiotoka(awamu ya 5),wewe chawa wa Mwendazake huna lolote unaloongea la msingi Kwa hiyo Tulia endelea kuomboleza.

Mumeambiwa awamu yenu ndio imeleta uandishi wa maigizo ya kusifia sifia hovyo ambao haukuweoo kabla.
 
Kila kitu kina utaratibu, huwezi andika chochote ilimradi.

By the way wenye vyombo ndio wanaotakiwa kusema sio nyie mataga wa Mwendazake
Kwa ivo wenye vyombo vya habari wanamiliki vyombo hivyo Kwa ajili ya nani!?

Umewahi kuona leseni yoyote ya chombo Cha habari???

Chombo Cha habari kinawajibika Kwa umma na ndiyo maana Kuna Sheria ya maudhui ya vyombo vya habari.
 
Shida inaanzia kwenye Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, 2016. Mwandishi akisoma masharti na adhabu zilizomo anabadili gia angani. (1) EACJ iliainianisha vipengele visivyopungua 17 vinavyolakamikiwa na wadau waliofungua shauri kwenye hiyo mahakama. (2) Baada ya kuvipitia, mahakama ikabaini vipengele visivyopungua 16 ni kweli vina shida, kipengere kimoja ilikiacha. (3) Serikali ya Tanzania ikaelekezwa ivirekebishe. (4) Mwaka jana serikali ilifanya marekebisho kwenye hiyo sheria katika sections 5, 38, 50, 51, 53, 54, 55, 63 & 64 (yaani jumla ya sections 9). (5) Lakini wadau walilalamikia sections: 7(3)(a), (b), (c), (f), (g), (h), (I) & (j); 13, 14, 19, 20 & 21; 35, 36, 37, 38, 39 & 40; 52 & 53; na 58 & 59. (6) Katika sections zinazolalamikiwa na wadau marekebisho yamegusa sections 4 tu (yaani, 38, 50, 53 & 54). (7) Lakini sections 5, 51, 55, 63 & 64, licha ya kwamba hazikulalamikiwa na wadau, nazo zimefanyiwa marekebisho na kufanya jumla ya sections 9 kuwa zimefanyiwa marekebisho. (8) Kwa hiyo, kati ya sections 17 (kwa mujibu wa EACJ sections 16) zilizolalamikiwa ukitoa 4 (zile zinazoendana na zilizolalamikiwa na wadau), bado sections 13 (na kwa mujibu wa EACJ, sections 12) hazijaguswa, licha ya kulalamikiwa.
 
Umesahau juzi juzi ulipokuwa unatumika na jiwe kumpamba akiwa anachinja watu na kufanya udikteta?
 
Kwa ivo wenye vyombo vya habari wanamiliki vyombo hivyo Kwa ajili ya nani!?

Umewahi kuona leseni yoyote ya chombo Cha habari???

Chombo Cha habari kinawajibika Kwa umma na ndiyo maana Kuna Sheria ya maudhui ya vyombo vya habari.
Sasa Umma ndio unahariri maudhui ya chombo Cha habari?
 
Umesema sahihi, halafu Mwanakijiji amesahau alivyokuwa wakala wa JPM wa kuua ajenda za wananchi, wanachofanya wenzake yeye Mwanakijiji ndio muasisi
 
Sasa hii njaa huwa inaisha kwani? Maana wakati wa JF tuliambiwa waunga juhudi wote wanashikishwa...walikuwa na njaa
Ulitaka kusema wakati wa JPM?

Ila naona hadi sasa msimamo wako ni uleule wa kutomkosoa JPM, kwako hadi leo JPM hakuwahi kukosea popote .
Kipindi hiki naona unajaribu kujitokeza kuipinga serikali, wakati wa JPM hukuona shida ulimtetea zaidi na mwisho ukaamua kukaa kimya kuliko kumkosoa Homeboy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…