Tuna hatari zaidi kwa Vyombo vya Habari kuliko wakati mwingine...

SI wahadhiri, si wanafunzi, wote ni wafu wanaotembea.
Sikajiona chuo chenye elites wa kuongea ama kukosoa jambo lenye manufaa kwa nchi. Ni chawa na waganga njaa wakubwa!
Na hilo ni tatizo kubwa sana tulilonalo na ambalo wengi hawajalitambua.

Kwa kuwa neno uwajibikaji haupo katika serikali na vyombo vyake, ni vigumu sana kwa mwandishi wa IJ kufanya kazi yake maana atakapoanza kufanya uchunguzi wake atahitaji vifaa au "tools" au ufundi yaani "technical".

Kuna mambo kama kanzidata ambayo ina taarifa zote anozihitaji, awe na vyanzo vya siri au anonymous ambao waitwa "whistleblower" na si mtu tu kaiba taarifa. Hawa WBs waweza kuwa bado wako kazini au wameacha kazi lakini wana ile techinical knowledge ya mahali wanapozungumzia.

Na pia zipo mbinu zingine kadhaa ambazo siwezi kuziweka hapa zote lakini ni muhimu kwa mwandishi wa IJ.

Kwahiyo kusomea uandishi wa habari pekee hakukufanyi kuwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi, ni lazima uingie kujifunza namna ya kufanya kazi za uandishi wa habari za kiuchunguzi kwa kukaa tena darasani.
 
Hakuna intellectuals wa kukosoa vitu; wamebakia legends kama kina Ulimwengu, Prof. Shivji, na wachache wao. Walioko vyuoni sasa hivi hawawezi kuthubutu.
Na si kukosoa tu kwa mfano katika IJ hiyohiyo kuna matawi kama "Preventive Journalism".

Hii PJ ni uandishi wa habari ambao umelenga kutoa taarifa ya kuvijulisha vyombo vya serikali au jamii juu ya tatizo linoanza kujitokeza au litalojitokeza endapo hatua hazitachukuliwa.

Kwa kuwa kuna mawasiliano mazuri kati ya serikali na waandishi wa IJ utakuta serikali yachukua hatua mara moja kwa kutambua mchango wa waandishi wa IJ.

Lakini juzi mwandishi kamamatwa polisi kwa kuandika taarifa juu ya RC alijigonga kwa mwanafunzi. Ila kwenye jamii lipo tatizo la watu kulawitiwa na wengine kuumizwa.

Kulawiti ni kosa la jinai kwani ni kumuingilia mtu kwa nguvu bila ridhaa yake khasa watoto wadogo kama yule wa Arusha.

Hili ni tatizo la kijamii na kwa kuwa jamii yatambua kuwepo kwa tatizo hili ni fursa nzuri kwa mwandishi wa IJ kuandika kwa kina akitumia vigezo vyote ili kuitaarifu serikali ambayo kazi yake ni kuchukua hatua.

Kwa kuwa mwandishi alieandika juu ya RC hana sifa za kutaarifu habari za IJ polisi kwa sheria zao wakaamua kumkamata.
 
Asante
 
Kulingana na utafiti uliofanywa na Twaweza,MISA-TAN,Jamii Forum na TAMWA asilimia 50% ya waandishi wa habari hukumbana na vitisho,ukatili na unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Na wale 50% waliobaki ? Nadhani tukileta hizi excuses tutakuwa hatuendi hii kazi sio rahisi na mpaka ujitoe huko ni kwamba unaiweza.., sasa kama ikawa ngumu kuliko kugeuka kuwa cheerleader au kasuku bora uje huko kijijini tulime mihogo (hapo tutakuwa tunawatendea haki watanzania kwa kuwapatia chakula na sio kuwalisha matango pori)
 
Perception ni muhimu sana mnaweza kuangalia kitu kilekile lakini wewe ukadhani kwamba ni manyuzi nyuzi meusi wakati mwingine akaona kwamba ni nywele....

Kuna faida gani kwa mwananchi (mlaji) kama anaendelea kulishwa propaganda na hapati ukweli au uhalisia..., kama yule alitumia mabavu (very bad) lakini huyu anayetumia pesa zako (Kodi) kufanya kilekile ni kama kupe anayekunyonya ili uendelee kuambiwa kwamba nyekundu ni nyeusi....

 
Mkuu anzisha media yako kutekeleza malengo ya check and balance. Unafeli wapi?

Nyie mnawachochea wenzenu tu halafu mko pembeni mnakula kuku kwa mrija
 

Anyway, lets not lose hope. Kusema kweli, haya uliyoandika yapo
 
Umesema sahihi, halafu Mwanakijiji amesahau alivyokuwa wakala wa JPM wa kuua ajenda za wananchi, wanachofanya wenzake yeye Mwanakijiji ndio muasisi
Huyu mzee Mzee Mwanakijiji ni TAFSIRI sahihi ya UNAFIKI ndiyo maana nimempa FRONT kuwa aanzishe chombo chake ndiyo kifanye hizo mavitu. Kukosoa vyombo vya watu ambavyo wame sacrifice kuanzisha kwa jasho na damu katika kutengeneza mtaji siyo sahihi.

Wakati wa Magufuli huyu mzee alikuwa CHEERLEADER wa sera za Dikteta za ukandamizaji demokrasia, kulitawqla bunge kwa remote control, kutishia mahakama na kukosekana kwa utawala wa sheria.

Hatukuwahi kumsikia Mzee Mwanakijiji akikemea tabia ya hovyo ya Magufuli ya kuvitishia vyombo vya habari na kubana uhuru wa maoni.

Kwenye JF Mwanakijiji anajidhirisha kabisa kama kinara wa Sukuma Gang
 
Kama wewe hukuwahi kusikia haina maana inawezakana masikio yako yanachagua cha kusikia. Kuna link ipo kwenye posting ya kwanza soma usiseme vilivyo kichwani tu.
 
Inawezekana umesahau kabisa kilichotufanya wengine tuigeuke Chadema. Nasubiri.
 
Kwani nchi hii wamiliki wake halali ni kina nani? Tusiache mbachao, kwa msala upitao
 

Inataka ujasiri kubadili yanayoendelea. Maana uozo uliopo umepitiliza kina na kiasi. Ila si busara kukata tamaa. Kwenye giza totoro, ni dalili kuwa kunakucha
 
Aahaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…