Ajabu sana kwamba humu Jf hakuna hata member mmoja ambaye ana ndugu katika hao wagonjwa wengi wa corona tunaofichwa na serikali wala hakuna member aliyefiwa na ndugu wala rafiki kwa kifo chenye kuhusishwa na corona. Yani humu wote tunasikia tu wagonjwa wa corona ni wengi na vifo ni vingi.
Kwa maandishi haya unaweza ukadhani umejibu hoja ya kuwepo au kutokuwepo wagonjwa wengi na vifo vingi zaidi ya hao/hivyo vinavyotangazwa na serikali, lakini ukweli ni kwamba hujibu chochote.
Sio kazi ya members wa JF kutafuta wagonjwa au vifo; hii ni kazi ya serikali.
Kwa mtu mmoja mmoja, vifo viwili au vitatu kijijini kwa siku haviwezi kuweka tofauti kubwa na vile vya siku zote. Lakini hivi vikijumuishwa na vifo vya mkoa au nchi nzima kwa siku, hapo ndipo unapoweza kujua tofauti iliyopo.
Hii haiwezi ikafanywa na mtu aliyepo JF.
Kwa hiyo usifanye kupoteza lengo la takwimu. Ukweli ni kwamba wapo wagonjwa wengi zaidi ya hao waliopimwa na kuonekana ugonjwa wao ni COVID-19, hiyo ndio maana ya kupima.
Pangekuwepo na uwezo mkubwa wa kupima watu wengi, namba hiyo inayotangazwa kila siku ingekuwa ni tofauti.
Hali kadhalika, vifo pia vinavyotokana na corona vitakuwa ni tofauti na hivyo vinavyojulikana serikalini.
Kutokuwa na uwezo wa kutambua, hakuwezi kuwa halali kujumuisha kwamba vifo au wagonjwa ni wachache.