Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Ikiwa watakidhi vigezo mimi binafsi sioni shida kwani tunataka watu wa kuwatumikia watanzania na si vinginevyo. Mbona wakati wa uchaguzi maaskari na wanajeshi kutoka bara wanakwenda Zenj kuimarisha usalama?
 
Muulize Jasusi Evarist Chahali kuhusu idadi ya waislamu na Wakiristu nchini na ishu ya imbalance katika teuzi hizi zinazoinvolve watu wa dini hizi—Alikuwa, anafanyia PhD suala hili.

By the way, huwezi kujua idadi ya Waislamu na Wakiristo nchini bila sensa

Sensa ninayoifahamu mimi iliyokuwa na kipengele cha dini za watu ni sensa ya mwaka 1954 iliyoonyesha Waislamu ni wengi zaidi.

Kwa sasa ni vigumu kujua idadi ya waislamu na wakiristo nchini mpaka labda ingekuwepo sensa inayoangalia kipengele hicho!
 
Mama alishasema sifa za mtu hasa utendaji( mzuri / mbaya) ndo inampa nafasi zaidi ya kuwa sehemu fulani
 










Mkuu#@Missile of the Nation...kabla atujaendelea jibu hoja hizi zilizoibuliwa na wadau kutokana na uzi wako.mim ntataja 1 tuuuu...
a)kigezo cha uwiano wa kidini zanzibar haupo,je hili unalizungumziaje? Je unakubali dini zingine zianze kudai uwiano?na kama ndivyo matokeo yake unadhani yatakuwa na faida kuliko hasara KWA ustawi wa nchi yetu?....mkuu na hapa kwenye faida na hasara ya unachosisitiza..... mifano hai tunayo so ni vizuri ulete facts(nakukumbusha tuuu).....

mkuu kumbuka udini,ukabila,ukanda ni watoto wa baba na mama mmoja CHUKI NA MATENGANO

Jibu la swali lako:tukisema tuesabu watu KWA njia ya udini ni mwanzo wa machafuko KWA sababu
itajenga chuki:dini moja inaweza kukuta inawawakilishi wengi au wachache katika nafasi mbalimbali za nchi nakujiona inatengwa,inabaguliwa au kunyanyaswa kitu ambacho KWA hali ya tanzania si kweli.... na dini ambayo itakuwa na wawakilishi wengi inaweza kudharau dini nyingine na kuibua haki ya kuwa na dini moja....minorities au majorites(dini) wenyewe nao wanaweza kutaka kujitenga(mkuu mifano tunayo kwani hakuna jipya chini ya jua)

Ndio maana nyerere alikemea sana ukabila udini ukanda unzanzibari na utanganyika KWA kuwa alijua kuwa huo ni mwanzo wa taifa kuanguka na kama si hivyo ndo itakuwa ni fursa nzuri wa maadui wa nje na ndani kuibia na kunyonya utajiri wa nchi usika na kuwaacha wazawa kwenye mapambio ya unzanzibari utanganyika udini ukabila

Dunia kuwa moja imeshindikana,imebaki utaifa..tukitoka kwenye utaifa na kuingia udini na ukabila...dunia hapatakalika...

Mkuu hoja yako si mbaya sanaa...najua ni KWA nia nzuri tu ILA angalia negative impacts zilivyokubwa...ndo maana wadau humu wanakupinga KWA kuwa mwisho wa siku tutaingia kama mkuu ngosha wa mwanza alivyosema kwenye komenti yake ya pili...

NB:JIBU HOJA YA HAPO JUUU ILI TUNAPOKUJIBU TUJUE UELEWA WAKO UPO LEVEL GANI MKUU WANGU
 
Mkuu tuwainclude kivipi?unamaanisha tuwachukuwe wote ama?
Maana nachokijua ni kuwa ndani ya serikali hawapo wakristo na waislamu tu... Baliinclusion imejumuisha dini zote dini nyingine
Labda mwenzetu unanjia ya kuinclude tofauti na hii..ebu tujulishe
 
Yap....Naunga mkono hoja
 
Mimi kwangu awe Muislamu,Mkristo, Hindu e.t.c ninachopenda kuona ni
1.Katiba kuheshimiwa
2.HAKI isiwe jambo la hisani ya Kiongozi
3. Taasisi imara zisizoingiliwa na mhimili wowote kimaamuzi.

Kubwa zaidi watu waishe kwa furaha.
Kweli mkuu mambo ya udini hayatuhusu
 
K
Kiongozi kuna mambo bado hujayachambua kwa kina... MIMI SIO MDINI ila naandika kile kilichopo katika jamii yetu kwa sasa...
1. Wanafunzi wengi waliopo shule za kata niwa dini ya Kiislamu.... kwa shule za binafsi asilimia kubwa ni wakristo... ( tafakari hapo kiongozi)
2. Idadi kubwa ya vijana wakike na kiume waliopo mtaani niwadini ya kiislamu... matokeo yake Vijana wa kike wanazalishwa wengi wao wakiwa shuleni au mtaani ili hali hawana mafanikio yoyote ya kiuchumi kuweza kujikwamua au kuwapeleka shule nzuri watoto... wanaishia shule za kata....
3. Hata huku kwenye roots ya elimu kuanzia elimu msingi na vyuo, walimu wengi staff niwa kristo.
4. Kibaya zaidi hata hao wachache iwe ni walimu, madaktari etc huwa hawana misimamo mikali ya imani iwe kuangalia eti huyu mkristo au muislam ( big up Mama Samia chagua kwa kuangalia utendaji wa mtu)
5. Mfano Mazingira ninayoishi, majirani zangu kila siku visomo na mambo mengine ya ushirikina... kiongozi haya yana athiri sana... elimu ya vijana mashuleni.
6. Fuatilia mashuleni haswa msingi na sekondari kila siku watoto wanadondoka mashetani 100% niwa wanafunzi wa kike wa dini ya Kiislamu... hii ina athiri sana elimu ya watoto....
Kwa ufupi kiongozi elimu ndio kila kitu... pamoja na utendaji wa mtu. Naamini watu hao wapo kwa dini zote mbili... ila ukweli ni kuwa wakristo mpaka sasa wanaongoza kwa wasomi....
Note: Shule nyingi za wakoloni ( zilikuwa zipo kikristo zaidi) viongozi wako mfano Mzee Makamba alisoma shule za mission.... lakini mzee makamba sio mdini... Kiongozi Achana na Mawazo ya Udini angalia utendaji wa mtu anafaa mpe kazi hafai achana naye. ACHA UDINI.
 
If moderators hamuwezi kumfungia huyu punguani na mada zake za uchochezi?
Kila akijamba ni udini,
Fungieni huyu mpuuzi anayeangalia jina la mtu kujua dini ya mtu.
Hajui kuna jamaa yangu Hamisi Khalfani ni mgalatia na kuna Jesse Joseph ni mjahidina.
Ndugu acha upuuzi.
Najua unatumwa na wenzako wa ndani ya sistim
 
Unarudi pale pale kwanini qualifications ratio yake ni biased? Je! Kuwepo na empowerment ya upendeleo ili pawepo na balance.
 
Ubaguzi ni hali/kitendo cha kumnyima/kutompa mtu kitu/haki yake au huduma anayostaili kutokan na hali yake yaweza kuwa ya kisiasa(minajili ya kichama,kiideology),kijamii(ukabila udini ukanda ) au kiuchumi(masikini tajiri)....Ndo maana hilo swala halipo na halijawahi kutokea kuchangu wote wa dini moja...so mfano wako ni mfu na si hai....hauakisi ualisia wa mambo
 
Africa ya kusini: elimu nzuri ya vyuo vikuu wanayo wazungu na ufundi wanao wazungu! Weusi kazi zao ni kucheza ngoma na kuoa wake wengi hivyo. Unapo Ajiri ajira zote uwape wazungu tu waafrika was ipewe maana walikuwa wapi wakati wazungu wanasoma? Ukielewa hilo utaelewa na ubaguzi wa hapa Tanzania
 
Shida ya waislamu huana haya wanapopewa mamlaka makubwa kama hivyo. Huyu Mama sio kama hajui anajua vyema msuguano uliopo baina ya imani hizi, ila basi tuu kapuuzia kwasababu anazozijua yeye mwenyewe. Hivi kweli ndio hakuna waislamu wa kutosha wenye elimu na ujuzi wa kuwekwa ngazi ya utawala wa katibu mkuu walau kufanya ile ratio iwiyana walau kwa 40% hadi 50%. Basi tuu ufedhuli wa wenye mamlaka na dharau. Ndio mwisho yanatokea ya Mozambique halafu mnasema wamekosa ustahamilivu.
 
Mkuu...achana na huyu jombaa ni mdini....anashindwa kukontrol hisia na mapenzi kwa dini yake...anataka kutumia kigezo hicho kugawa watu....huwa hatutumii personal feelings kuendesha nchi
 
Mkuu na si KWA mama tu...nchi zote ambazo azifungamani na dini zina system hiii....huyu jamaa Analake jambo
 
Yap umenena vyemaa....sidhani kama amekuelewa......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…